Katuni ya Masoud Kipanya inamaanisha nini?

Katuni ya Masoud Kipanya inamaanisha nini?

Magufuli alikuwa hataki shobo nao ndo maana walikuwa wanamuogopa ...wanajua uwezo wa kuchukua madaraka hawana ndo maana wanataka kula sambamba na watawala
 
Wengi wameshindwa kuielewa katuni na tafsiri yake.

Kwa fikra za mwandishi, mbwa amejishusha kwenda kwa chatu kumwomba ammeze. Chatu naye hammezi, anaanza kwanza kutafakari.

Kisha chatu akammeza mbwa. Lakini mbwa baadaye akamtoboa tumbo. Chatu akabaki kufurahia kuwa amemeza mbwa asijue kuwa tumbo lake limetobolewa.

Hata hivyo hizo ni fikra za mwandishi, si lazima zibebe ukweli wa kile kilichopo.
 
Kwahiyo kale ka mbwa kamemezwa? Ndo maana siskii kelele na haikua kawaida ya kale ka mbwa kukaa kimya.
 
Wengi wameshindwa kuielewa katuni na tafsiri yake.

Kwa fikra za mwandishi, mbwa amejishusha kwenda kwa chatu kumwomba ammeze. Chatu naye hammezi, anaanza kwanza kutafakari. Kisha chatu akammeza mbwa. Lakini mbwa baadaye akamtoboa tumbo...
Kuna uzi mbili zimeungwa.

MODS wangesubiri mpaka hapo baadae. Ndio unaona purukushani.

Wanaboa saa nyingine.
 
Wengi wameshindwa kuielewa katuni na tafsiri yake.

Kwa fikra za mwandishi, mbwa amejishusha kwenda kwa chatu kumwomba ammeze. Chatu naye hammezi, anaanza kwanza kutafakari. Kisha chatu...
Maanake kama mbwa ametoboa tumbo la chato kwahiyo madhara yake chato atakufa kwa kumeza mbwa? Hili ni gumu CCm haiwezi kufa kwa ajili ya kuridhiana na chadema
 
Kwisha habari yao...

Sasa hivi hawana tofauti na Prof wa Uchumi, au Rangi ya zambarau kamw sio Mzee Momose...

Una weza kutoa mifano kibao kushadihisha hili

Kifo cha mende, Chaliii. kwa sauti Prof wa Uchumi
uvccm mlishapata sonona na mtaendelea kupata sonona mpaka akili mfe wajinga nyinyi, toka muanze kusema kwisha leo ni miaka mingapi ujinga mzigo.
 
Si kweli,CCM kubwa ndo maana JPM kaondoka bado chama hakijateteleka na samia nae akiondoka bado chama imara ila chadema akiondoka mbowe tu ufa mkubwa utatokea
kama CCM ilivyo jeshi la Samia, ukimuweza samia basi wengine ni "takataka",
 
Kipanya haya ni mawazo yake, he is at liberty to thik the way he thinks. Sawa na humu JF waliosema , tena wengi sana kuwa mawakili wa Chadema kuacha maswali ya dodoso kesi ya la akina Halima Mdee ni wazi kuwa jana 8/3/2023 wangelisamehewa na kuendelea kuwa wabunge. Jibu wamelipata jana! johnthebaptist
Jibu wamelipata jana![emoji818][emoji817]
 
Wengi wameshindwa kuielewa katuni na tafsiri yake.

Kwa fikra za mwandishi, mbwa amejishusha kwenda kwa chatu kumwomba ammeze. Chatu naye hammezi, anaanza kwanza kutafakari. Kisha chatu akammeza mbwa...
Na Chatu ukishamtoboa umemmaliza
 
Mama hatumii nguvu kuwakamata, anawarushia mtama wanaingia wenyewe kwenye tundu.🤣🤣🤣
na sio mamayenu kuwa kamezwa etii kwa akili ya kawaida nani amemezwa au hao wafuas wa ccm wanapochora katuni mnajifariji waambien waitishe mikutano bas tuone nani kamezwa maana wananchi ndo waamuz.
 
Raia wa Tz wali msariti mbowe kwa miezi 9 alio kaa jela bila mandamano au mgomo, hana jinsi bora aungane nao, raia wenyewe anao pigania hawaeleweki na ni waoga.
Usilaumu raia kwa kutia umoja wakati wafuasi wake wana chadema walikuwepo je walifanya nini? Maana nje ya chadema na upinzani wote waliyobaki wanaonekana ni CCM na sukuma gang, sasa hao chadema na upinzani kwa ujumla wao mbona hawakuandamana?
 
Picha ya kwanza maadui wamekua marafiki tena mnyonge ndie kasalim amri urafiki wa kinafiki huo.

Picha yapili ni huyo adui kamgeuka kameza inaonekana ule urafiki ulikua ni njia ya kumfanya msela awe karibu ili aliwe bila kutumia nguvu na kweli adui kameza kitoweo bila hata kumkimbiza

Picha ya tatu ni adui kaonyesha uhalisia wake meno njee nani ataongea tena?

Hapo ilo mbwa ni kama vyama vya upinzani na chatu ni ccm haya maridhiano ni njia ya kuwavuta wapinzani na kuua upinzani kisha upinzani ukishakua umemezwa na ccm ndiipo sasa mr chatu anakua kwenye uhalisia wake maana hakuna tena upinzani.

Kuua upinzani kuna mmoja alitumia nguvu sasa anatumia akili
 
Back
Top Bottom