Uchaguzi 2020 Kauli mbiu ya Uhuru na Kazi yampaisha Tundu Lissu

Uhuru upi?

Hivi mwananchi wa nanjilinji kule ukiongelea juu ya uhuru si anakushangaa?

Hilo la uhuru atawapata viongozi wenzie wa pale ufipa
 
Nchi hii inabidi tupiganie uhuru kwa mara nyingine baadaya kupoteza uhuru wetu kwa utawala.
 
Lissu ahangaike tu ila hana uwezo wa kuvaa viatu vya magufuli, Nyerere tu ndo anaviweza
 
Uhuru upi?

Hivi mwananchi wa nanjilinji kule ukiongelea juu ya uhuru si anakushangaa?

Hilo la uhuru atawapata viongozi wenzie wa pale ufipa
Huko kijijini si ndiyo zaidi? Wanamwelewa sana
 
Bado shughuli haijaanza viongozi msipofushwe na wingi wa watu.
Huu uwe ni wakati wenu kupanga mikakati ya ushindi kuanzia madiwani, wabunge na hatimae uraisi.
Mjue uraisi bila wabunge ni mzigo.

Tahadhari; Ukimya wa ccm msiuchukulie poa, wekeni mipangilio... hii ni vita na vita ni mbinu.
 
Kwa kweli hata mimi nahitaji uhuru , mtu anayenizuia hata kumwombea mtu aliyepigwa risasi 16 nitampaje kura yangu? Heri nilale njaa ila niwe huru.Siku zote wanadamu timamu wanausaka uhuru.Sitachoka kuusaka na kuupigania uhuru.
Ni sawa na kujidanganya kuwa wana mazuri utumwani.
ETI wangefurahi sana maisha hayo yaendelee kwani "........yule Baba huwa anatugawia nguo........"
AMEN
 
Ni ukweli uliowazi Sasa kwamba mgombea Urais kupitia Chadema Tundu Lissu ni kama amewameza wagombea wenzake na hawasikiki tena.
Kipenga cha kuanza mbio (za kampeni) hakijapulizwa. Yeye kaishaanza kukimbia ovyo ovyo. Wenzake wametulia wakiangalia silaha alizo nazo (anazotumia kuwashawishi wananchi wampe kura).

Hivyo washindani wake anawapa fursa ya kuzijua silaha alizonazo (weakness zake) na na hivyo kuwapa fursa ya kupanga aina ya silaha watakazotumia kumwangamiza (kujibu mapigo anayofanya sasa hivi). Kwanza kipenga cha kuanza mbio hizo kitakapopulizwa jamaa huu atakuwa tayari ameshachoka ile mbaya na alishamaliza silaha zake zote.

Hivyo subiri kuona jinsi kipenga cha kuanza mbio hizo kitakapopulizwa atakavyoangamizwa kwa silaha nzito nzito, hapo washindani wake watakapoanza kujibu mapigo (ya kushawishi kura za wananchi). Mbaya zaidi washindani wake wako 16 kutoka majeshi (vyama) mbali mbali. Hashindani na jeshi la ccm pekee bali na majeshi (vyama) 16! Kuna majeshi ya Bernard Membe (Jasusi mbobezi), Lipumba (Professa mbobezi wa Uchumi wa dunia), Mbatia ( mbobezi wa majanga ya dunia) na mabobezi mengine ya kadhalika na kadhalika ya dunia! Yaani jamaa ajiandae tu kurudi ughaibuni kuendelea na matibabu yake na kuichafua nchi yetu mbele ya jumuiya za kimataifa kama alivyozoea kutufanyia. Ila urais haiwezekani hata kidogo. Ubunge nao wakina Ndungai walishamalizana naye!
 
Mkuu hizi nguo nimeona zikigombewa kama njugu mahali fulani lakini sikuelewa , kumbe ndio ziko hivi !

Yatakuwa kama ya wimbo wa taifa, kesho utasikia mgombea kafanya kosa kwa kuandika jina Jezi ya Taifa.

Ni kama Utoto ila yanaweza tokea, Hii nchi akili kumkichwa na ujinga pia kumkichwa
 
Kipenga cha kuanza mbio (za kampeni) hakijapulizwa. Yeye kaishaanza kukimbia ovyo ovyo. Wenzake wametulia wakiangalia silaha alizo nazo (anazotumia kuwashawishi wananchi wampe kura).

Lissu anazunguka mikoani lengo sio kuomba kura ila ni kuondoa hio dhamira mbovu ya kumkata ambayo sisiemu wanafikiria.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…