Upinzani imara unaifanya Serikali iliyoko madarakani kutokuwa lege lege ( By Mwalimu Nyerere).
Serikali iliyoko madarakani inafanya jambo jema sana kutokumbughudhi Tundu Lissu katika harakati zake za kutafuta wadhamini.
Si lazima Tundu Lissu awe Rais wa Inchi ila muhimu ni yeye kuleta Uhai wa Demokrasia bila kuvunja upendo na Amani ya Inchi.
Misahafu Takatifu inasisitiza sana Amani na upendo kuliko utajiri .
Utajiri, madaraka nk. vyote vitapita lakini kiongozi anayedumisha amani na upendo jina lake halitapita kamwe..
Hata watu wako wakiwa maskini lakini wako huru na wana furaha ni bora kuliko kitu chochote.
Yesu Kristo aliweza kugeuza mikate 5 na Samaki wawili kutosha kuwalisha watu 5000 na kubaki vikapu 12.
Yesu Kristo hakuwahi kumiliki nyumba, shamba au mifugo. Hata yule punda aliyempanda wakati anaenda kuteswa hakuwa wa kwake. Sisi waumini tunajua alikoteswa na kuuwawa Yesu Kristo. Sisi waumini tunajua mahali alipozikwa Yesu Kristo.
Hadi Sasa Yesu Kristo anakumbukwa kuliko kitu chochote Duniani bila kujali imani ya mtu.
Tusitangulize sana ustawi wa uchumi ila amani,
upendo na uhuru.