- Thread starter
-
- #141
Uliloandika hapa ndiyo msimamo wa Tundu Lissu Rais mtarajiwaDhana ya Uhuru zaidi kujiamulia mambo yao wenyewe ni dhana yenye maana pana sana. Watu jamii ya waislam wanaamini nadharia ya Serikali kutokuwa na dini ni nadharia iliyowekwa ili kuzuia ustaarabu wa dini yao kustawi.
Tundu anapaswa kusema bila kutafuna maneno endapo ataendeleza ukandamizwaji huo au kuweka wazi ili apate kura za wenye dini inayokandamizwa.
Huwezi kuwakandamiza watu kwa muda mrefu pasipo wao kuzinduka. Binafsi najaribu kuwaza ni jinsi gani CHADEMA itatatua tatizo hili. Watu wanajifunza asili yao na pale wanapojihisi wanabaguliwa huwa tayari kutetea haki zao na ikibidi ghasia hutokea.
Kwani watu hubadilika na kamwe hawatoridhika kujiona wao no jamii ya daraja la pili iwapo kuna chama kinaweza kuwapa Uhuru wa kujiamulia mambo hao ikiwemo utamaduni wao.