Kauli ya Chongolo ni ufedhuli kwa wasomi wa vyuo vikuu. Ipingwe!


Siku hizi elimu inadharaulika kuliko maelezo kisa ajira. Wapo wengi tu wanaelimu ya chuo kikuu wamejiajiri na wengine wameajiriwa, tusidanganyane kwa mifano midogo, wakati serikali ndio chanzo Cha yote haya.
 
Nimewatungia kitabu cha ujasiriamali cha kimombo ambacho unakisoma unaweka kwapani na kuanza kufanya biashara kwa mafaniko changamoto itakuwa mazingira ya kufanyaji bisahara yamedumazwa kila mtu anapambana kivyake
 

Please, kwani hao wanaotengeneza gesi walifundishwa wapi Kama sio vyuoni? Acheni kushusha elimu ya chuo kikuu.
 
Huu ni kuonyesha uduni wa upeo ulionao kuhusu mambo haya.

Ndiyo maana unatumia maneno ya kipumbavu kujibu hoja usiyo na uwezo wa kuijibu.

Kwa hiyo wewe hapo unaona "uhasibu au ununuzi" ni fani za kipekee sana kwamba walio na digrii hizo hawawezi kufanya kazi nyingine nje ya kuajiriwa?

Hii inaonyesha hata kama una digrii katika maeneo hayo hiyo digrii haikukusaidia kitu chochote. Hujawahi kuona wahitimu wa eneo hilo waliojiajiri badala ya kuajiriwa?

Halafu unajipachika u-'Sir' kuonyesha ujinga mkubwa unaokusumbua.
 
Siyo Tanzania pekee mkuu, ni dunia nzima.
Huko nchi zilizoendelea kuwa na digrii hakumfanyi mtu awe wa kipekee kuliko wengine..
 
Unataka mtu aliyesoma Political science, Medicine, au Accounting akafanye kazi za fundi bomba au fundi ujenzi?
Kama hakuna ajira kwenye maeneo ya alikosomea, 'why not'?

Hivi watu mbona hizi digrii mnaziona kuwa za ajabu sana? Kuwa na digrii yoyote, maana yake ni kumpa uwezo zaidi aliyo nayo, ili kuweza kutatua matatizo yake kwa kutumia elimu hiyo aliyonayo, hata katika maeneo mengine yasiyohusika na digrii yake.

Ulaya tumeona watu wakiendesha taxi na digrii zao. Hapa kwetu bado ni kasumba tu ndiyo imajaa vichwani.

Lakini nikuulize. Ni kipi cha maana zaidi, kuwa na digrii halafu huna kazi, au unayo digrii na unao ujuzi nje ya digrii yako unaokuwezesha kuendesha maisha yako?

Hapa si swala la kuwa na digrii, bali ni swala la kuwa na ajira, iwe ni yako mwenyewe kwa kujiajiri au uwe umeajiriwa.

Daktari, Mhasibu au mwenye digrii nyine yoyote kama hana ajira kwenye fani yake, na wala hakuna uwezo wa kufungua ofisi yake katika eneo hilo analolijua na kujiajiri, lakini eneo la fundi bomba au ujenzi kuna kazi kuajiriwa au kujiajiri, kwa nini asiifanye, kwa vile tu kasomea udaktari au uhasibu?
 
Huko kote ni mwendo wa "What is the........"

Hakuna vitendo
 
Ni wapi aliposema "Anataka vijana wote wa vyuo vikuu wawe mafundi mchundo"
Maneno hayo pekee yanakufanya uonekane kutokuwa mtu makini katika kufikiri kwako

Hiyo 'mantiki' ya hoja uliyoiona wewe ni ipi hasa, mbona ni kama unajisemea tu maneno bila ya kujua maana yake ni nini?

Mkuu 'DEJAN7, sijui kama kweli nawe unayo digrii katika eneo lolote, na kama unayo, na umeajiriwa kutokana na hiyo digrii, basi hizi digrii hazina maana tena.
 
Sasa kama wewe uko huko na ki-digrii chako ka 'political science, lakini huna ajira, utamvimbia nani? Si mwisho wa siku utamtegemea huyo fundi wa Veta akulishe?
Hizi digrii watu bado mnayo kasumba ya ajabu sana juu yake.

Sawa, pata digrii yako, kama inakuwezesha kupata ajira hakuna atakayekuuliza.
Lakini huku unayo digrii, unailea tu miaka minne au zaidi huna kazi, unatembea nayo tu digrii yako mitaani. Hiyo digrii inakusaidia kitu gani?
Kwa nini upoteze muda wako wote huo, ambao ujuzi wa Veta ungekuwezesha kujifanyia shughuli zako mwenyewe na hata kupanua wigo wako wa akili kutazama fursa zaidi ya hiyo inayokuwezesha kuishi kwa heshima.
 
Hao VETA wanafundishwa na wahitimu wa vyuo vikuu, sasa sijui unongea Nini. Tatizo mnashabikia kauli za wanasiasa bila kufanya utafiti.
Tatizo haujenda shule unaongea mambo ya mitaani, pia haujawahi kuajiriwa viwandani ambako ungeona kama kuna mhitimu wa chuo kikuu anayeshika spana na nyundo.
 
Sina uhakika kama unaelewa hata maana ya private "sector" ni nini, Maana naona hapa unaongelea mtu akaanzishe private sector!
What is the Private Sector?

The private sector is the part of the economy that is run by individuals and companies for profit and is not state controlled.

Types of Private Sector Businesses

The private sector is a very diverse sector and makes up a big part of many economies. It is based on many different individuals, partnerships, and groups.

Kati ya mimi na wewe sijui ni nani sasa hajui maana.[emoji23][emoji23][emoji23]
 
Hao watu wanahusika katika kuandaa na kushauri kuhusu miradi mbali mbali, kwahiyo, watu wa fani hiyo wanaweza kujiajiri kwa njia hiyo ya kutoa ushauri.
[emoji23][emoji23][emoji23] Kwa hiyo wanaweza kuandaa maandiko ya miradi na kuwauzia watu siyo!?.
 
Oke twende taratib Kwa hoja. Tatizo la ajira ni tatizo la jamii au la mtu binafsi?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…