Kauli ya kuitwa 'wanyonge' ndio silaha hatari wanayoitumia viongozi ili wananchi wasitoke nje ya boksi

Miaka zaidi ya 55 toka uhuru bado wa Tz tunaitwa wanyonge na tumeridhika, hii ni dharau kubwa sana.

Nalichukia sana jina hili na silipendi abadani. Endapo unyonge ukiisha hawa viongozi wa wanyonge watakosa wa kumuongoza.

Ili waendelee kutawala lazima wanyonge waongezeke zaidi na zaidi, ili wanyonge wawe wengi inabd kuwaua kiuchumi wawe tegemezi.
 
Nakubaliana na wewe. Nimekuwa nikijiuliza swali hilo hilo. Iwapo kiongozi anakuwa wa wanyonge tu, je sisi wengine ambao si wanyonge tupo wapi na viongozi wetu ni wapi? Kwa hakika mnyonge hana haki kwani haki zake zote zinaminywa na hao wanaojinasibu nao.
 
Ukiwa dhaifu automatically unakuwa mnyonge! Nashangaa kwa nini yule jamaa anatoa povu kwa kuitwa dhaifu wakati serikali yetu ni ya wanyonge
 
jamani tusijisahau mwanasiasa nae anategemea siasa yake impe maisha..so kabla hajakumbuka hao wanaojiita wanyonge lazima ajikumbuke yeye kwanza atatue changamoto zake then ndo awakumbuke hao wanyonge

hao wanaojiita wanyonge ,,ni wanyonge sababu wamekubali unyonge wao, wamekubali kukabidhi changomoto zao zitatuliwe na mtu huyo mwanasiasa ambaye nae ana changamoto zake ...tujiulize first priority itaangukia wapi?

Mwanasia mtu wa ajabu sanaaa atakuja na list ya changamoto nyingi zinazo wakumba watu na kutuaminisha yeye ndio Mungu mtu atakaye tatua hizo changamoto huku nayeye nae anategemea kupata pesa hapo hapo.....TUUKATAE UNYONGE NA TUJIKOMBOE WENYEWE
 
Kwa hiyo lengo la Kiongozi wa Wanyonge ni kuhakikisha kila mmoja anakuwa Mnyonge, maana Wanaoongozwa wakierevuka watalazimika kutafuta Kiongozi wao Mwerevu.
 
kuukataa unyonge ni kutowapa mamlaka wanaotudhalilisha kwa kauli za kitumwa
 
uzi Huu nauweka kwene thread bora kabisa nilizowahi kuziona.
hatupaswa kuitwa wanyonge nchi yenye utajiri wa kutosha
 
Hii kauli huwa naishangaa Sana eti wananchi wetu wanyonge kwa iyo yeye ni nani? Wakiitwa wao wanachukia ama kweli kuongoza nchi hii ni rahisi mno yani wao kila siku ni kutuita sisi wanyonge ila wakiitwa wao ni tusi mambo mengine bwana mpaka unaweza juta kuzaliwa TZ
 
w
wao sijui kwanini hawataki kujiita wanyonge akati wanategemea mumo mumo kuiba ili wakomboe familia zaoo
 
 
"





Kwanza hiyo tafsiri yakohapo juu napingana nayo,viongozi wanaoitumia kauli hii wako sahihi na wanaitumia lugha hii kulingana na mahitaji ya wakati tulio nao.

Kiukweli nchi ya Tanzania kipindi kilichopita ilitengeneza matabaka ya walionacho na wasiokuanacho, dhulma ilitamalaki,uonevu,kukosekana huduma za haki za kisheria,huduma za afya zilitolewa kibaguzi,
wananchi kupokwa haki ardhi kwa kua tu hawana nguvu za kiuchumi,

Hali hii ikatengeneneza "wanyonge" kwa tafsiri sahihi ya kiswahili ni watu waliokosa msaada,

Kilichofanyika katika awamu ya tano ya rais Magufuli ni kulipa kipaumbele kundi hili la wanyonge kwa lengo la kuliinua .

Kuimalisha huduma za kijamii,kuhakikisha mfumo wa utoaji haki hauna upendeleo, kuwasikiliza kero zao na kuzitatua,kuwapa elimu bure,kwa sababu elimu iligeuka biashara badala ya huduma kwa jamii,na mengine mengi yenye lengo chanya kuwainua kiuchumi.

Hivyo kauli hii hua ni msistizo wa viongozi ya kua ipo na kundi hili kubwa pamoja nalo katika kuliinua kwa kuliwezeshea miundo mbinu bora,na wala si dhihaka,au tusi,
 
Viongozi wanajifichia kwenye kivuli cha kusema tz ni nchi ya amani.
ila kiuhalisia lengo la kauli hiyo ni wanataka wananchi tubaki kwenye kivuli cha unyonge.
 
Ni jambo la aibu sana mtu kujisifia kuwa yeye ni kiongozi wa wanyonge, nchi yetu iko huru na watu wake ni huru huyo anayetaka watu wawe wanyonge ana lake jambo. Watanzania tukatae kuambiwa sisi ni wanyonge katika nchi yetu kwanini tuwe wanyonge ni nani huyo anayetufanye tuwe wanyonge hatutaki kabisa hiyo sifa ya kutaka tusiweze kusema matakwa yetu. Hakuna mwananchi mnyonge. Mimi nitashangaa sana nikisikia tena kuna Kiongozi akijiita kiongozi wa wanyonge wakati hakuna mtanzania mnyonge katika nchi yake iliyopata uhuru miaka 55 iliyopita. Ni aibu sana kuitwa mnyonge.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…