Kauli aliyoitoa Mgulu Jana kwenye kipindi cha Dakika 45 cha ITV ni ya kifedhuli, Kijinga na haivumiliki.
Hii ni dharau kubwa kwa Rais Mama Samia Suluhu Hassan, nidharau kwa wananchi, naamini hata enzi za mwendazake kamwe asingevumilia kauli hii ya kilevi.
Ni kauli ambayo mtu yoyote timamu hawezi kuivumilia, Wananchi wana haki ya kuhoji na kitoa maoni yao kwa jambo lolote ambalo linagusa maisha yao ya kila siku.
Rais ni mwakilishi wa juu kabisa wa mwananchi, anapoona wananchi waliomchaguwa wanadharauliwa na mteuzi wake ni sawa sawa kabisa na kumdharau Rais Mwenyewe.
Hii imeonyesha jinsi gani mwigulu amefail kuongoza wizara ya fedha na hafai kukali hicho kiti hata kwa masaa 24 yajayo.
Ni mtake Mama yetu Mpendwa ampige chini fasta, Kuendelea kumbakiza hapo wananchi tutajua ile kauli ina baraka zako.