Kauli ya Mwigulu kuhusu Burundi ni hatari kwa Usalama wa Taifa. Serikali ijitenge nae!

Kauli ya Mwigulu kuhusu Burundi ni hatari kwa Usalama wa Taifa. Serikali ijitenge nae!

CCM na baraza lao la mawaziri Walishamdharau Mama, Ndio Maana huyu Mashamba Anatuambia Tuamie Burudi Kama Hatukubaliane na Utopolo wake wa Kodi za huduma za Kielectronics.
 
ITV ni kituo kikubwa,sijaona sababu ya kurusha kipindi ambacho walikuwa wanajua kuna mabadiliko baada ya Rais kuingilia na walimsikia hata Mwigulu akiongea pia. ITV wamefanya hivyo makusudi ili kumchonganisha Waziri na Umma.Poor ITV
 
Mh Rais Mama Samia suluhu Hassan bado hujastuka tu kuwa mtu huyu ni hatari katika utawala wako? Waziri wako anadharau amri ya Rais ambayo jana tu asubuhi umemuagiza yeye mwenyewe atwambie kwamba umesikia manung'uniko yetu na kwamba umeziagiza wizara zikae zishughulikie malalamiko yetu wananchi, Kisha siku hiyo hiyo jioni katika kipindi cha tv anazungumza haya?....
Huyu Waziri hafahamu Sheria za nchi,anavaa tai ya Bendera ya Taifa la JMT kila uchao lakini hana huruma/mapenzi na Watanzania wenzake.Ana mamlaka ya ku-Deport Watanzania kwenda Burundi?

Warundi ndiyo huwa hawalalamiki ama hawalipi tozo halali kwa nchi yao?Hili linatia shaka hata ya Udaktari wake wa uchumi.

Katiba hii iliyopo inasemaje kuhusu au sheria zetu zinaweza kutafsirije kauli kavu kama ya Dr Mwigulu?May be Mh.Diallo was right!
 
Kama Kuna watu wenye bahati juu ya uso wa nchi basi ni huyu Mwigulu Nchemba.
Mie sijawahi kabisa kuona uelewa wa mwigulu. Iwe ni siasa, uzalendo ambao Kila mara anavaa bendera, na hata kujieleza tu. Siasa zake siyo za kiitikadi( ideology Bali za fursa) ndo maana baada ya kuwa shabiki wa hayati Magufuli alimgeuka Kwa kukandia utawala wake pindi tu alipokufa...
Hana bahati yoyote nivile anajua kuramba makalio ya wateuzi
 
Mh Rais Mama Samia suluhu Hassan bado hujastuka tu kuwa mtu huyu ni hatari katika utawala wako? Waziri wako anadharau amri ya Rais ambayo jana tu asubuhi umemuagiza yeye mwenyewe atwambie kwamba umesikia manung'uniko yetu na kwamba umeziagiza wizara zikae zishughulikie malalamiko yetu wananchi, Kisha siku hiyo hiyo jioni katika kipindi cha tv anazungumza haya?...
Hii nchi bana! Kila mtu ana sharubu.

Hadi Yericko?
 
Mtu anaejua mambo ya miili ya kwenye viroba ni hatari kwa taifa na kwa rais pia
Huyu mtu ni hatari zaidi ndio maana maza kamuacha kiaina
Huyu ni kama makonda kwa magu
Ni ngumu kumpiga chini maana anajua mipango mingi miovu!
So what?Hiyo mipango miovu anayoijua ni dhidi ya nani?CCM mnajitetea au mnajichochea kuni wenyewe kwa kauli zetu.Yaani Mwigulu yupo pale kama hongo asitoe siri za mipango ovu ya nani?
 
Mleta hoja iko hivi.
Kipindi kilichorushwa Jana jioni na ITV nitukio ambalo alikwisha rekodiwa kabla ya maelekezo ya Rais na speech yake ya mchana...
Yes, alitakiwa awaambie wasirushe hicho kipindi kwa sababu kuna taarifa kwa wananchi alizoongea kupitia vyombo vya habari kuhusu tozo. Lakini kuacha kipindi kilichorekodiwa kiende hewani, ni dharau kubwa kwa wananchi na kwa Rais aliyempa maagizo aliyoyasema mchana kabla ya kipindi hiki kuruka hewani jioni.
 
Mh Rais Mama Samia suluhu Hassan bado hujastuka tu kuwa mtu huyu ni hatari katika utawala wako? Waziri wako anadharau amri ya Rais ambayo jana tu asubuhi umemuagiza yeye mwenyewe atwambie kwamba umesikia manung'uniko yetu na kwamba umeziagiza wizara zikae zishughulikie malalamiko yetu wananchi, Kisha siku hiyo hiyo jioni katika kipindi cha tv anazungumza haya?

Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania mko wapi mnaacha mtu kama huyu Waziri anakwenda katika Tv kulichafua Taifa na kumchafua Rais wa Nchi? Miiko ya utumishi wa umma na miiko ya viongozi wa Kiserikali juu ya kwenda katika vyombo vya habari iko wapi? Waziri anaongea kwa dharau kuliko hata kibri walichokuwa nacho Makonda, Mnyeti na Sabaya enzi za udikteta?

Waziri anadiriki kusema WANANCHI ambao ndio msingi wa uwepo wa Serikali wanaolalamika tozo hizi wahame nchi waende Burundi? Hivi Mwigulu anajua athari za kidplomasia kusema wananchi wanaolalamika waende Burundi? Kwamba Burundi ni eneo la kishenzi ambalo halina handhi ya utu hivyo yeyote anayolalamika, anayenung'unika au kufedheheka adhabu yake ni kupelekwa Burundi?

Mama umetoka juzi Burundi katika hatua ya kujenga uhusiano wa kidplomasia na nchi washirika na majirani, Kauli hii ya Waziri ni hatari na inadhoofisha juhudi zako zote za kujenga taifa na ushirikiano.

Mwigulu anatakiwa kuondoka katika ofisi ya umma na Serikali ya Tanzania iombe radhi matamshi haya kwamba si msimamo wa serikali bali wa mtu binafsi. Fikiria kesho waziri wa Burundi atangaze kuwa wanaotaka ushoga wote waende Tanzania huko ndio watakuwa mashoga wenye faida, Au Rwanda iseme majambazi wote waende Tanzania huko ndio watafanya ujambazi kwa amani, Au Somali iseme Magaidi wote waende Tanzania huko ndio watafanya ugaidi kwa amani. Nini matokeo ya kauli hizo?

Mama tunakutahadharisha kwa kila kitu juu ya mtu huyu na kundi lake, Maneno huumba, tumeshazungumza mara sita, amini mara ya saba neno litatimia katika umbo kamili. Mwigulu ni hatari kwako Mama na ni hatari kwa usalama wa Tanzania.

View attachment 1860881
Mwigulu nufaika la ccm, lishashiba pesa, yale maesta bus yote linaachaje kuwa na kiburi.
 
Kuna kauli alitoa eti nisikilize mimi Dr nakuakikishia hii kauli ni yamtu ambaye anajifanya kujua kila kitu na niyakibabe sn
 
Kipindi kiliandaliwa kabla ya jana asubuhi.

Mazungumzo ya jana hayahusiani na kipindi maana kipindi hakikua live jana.

Vitu vingine hutakiwi kua na akili kubwa kujua hilo.
Kwa sababu alijua kina hoja za tozo ambazo tayari ameshapewa maagizo na boss wake (Rais), alitakiwa asitishe kipindi hiki kilichorekodiwa kisiruke hewani, ili hoja alizoongea mchana zibaki kuwa final ili kupisha kikao kilichoitishwa na waziri mkuu kufanyika leo kifanyike na utekelezaji wa maagizo ya Rais ufanyike. Kwa ujumla hicho kipindi kilitakiwa kife kifo cha asili (natural death).

Labda mkuu kama hujui protocols za uongozi wa serikali.
 
Idara ya Usalama wa Taifa Tanzania mko wapi mnaacha mtu kama huyu Waziri anakwenda katika Tv kulichafua Taifa na kumchafua Rais wa Nchi? Miiko ya utumishi wa umma na miiko ya viongozi wa Kiserikali juu ya kwenda katika vyombo vya habari iko wapi?

Waziri anaongea kwa dharau kuliko hata kibri walichokuwa nacho Makonda, Mnyeti na Sabaya enzi za udikteta
 
Back
Top Bottom