Kama umesoma maelezo yangu vizuri utanielewa kipi hasa nacho maanisha swala la maandamano halihitaji ukurupukaji na watu kuingia barabarani pasipo kujua nini hasa wanachopigania. swala la maandamano linahitaji dhamira kwanza ya kweli kwa kila mmoja mmoja kutoka moyoni wajue nini hasa wanachopigania swala la maandamano sio swala la kuamka kesho na kuanza kuandamana peke yako au watu kumi hayo ni maandamano yasiyokuwa na tija swala la maandamano linahitaji vichwa vya watu kufunguliwa kwanza ili waliowengi wapate hamasa ya kupigania wanacho hitaji. maandamano yanaweza kuanza na kuisha ndani ya mwezi moja na mabadiliko yakatokea pia maandamano yanaweza kuchukua miezi miwili, mitatu, mwaka hata miaka ndipo yakatokea kulingana na tawala iliyopo madarakani inachukuliaje hayo maandamano kumbuka katika huo mwezi, miezi, mwaka , na hata miaka Kuna waandamanaji watakamatwa, wengine watapigwa na kuonewa, wengine watafanywa walemavu, wengine hata watauawa lakini Kama wananchi waliowengi karibia robo ya nchi wameandamana haya ambayo yanatokea kwenye maandamano hayatawazuia nyie msiendelee kupigania haki zenu maandamano mtayaendeleza mpaka pale dhamira zenu zitakapo timia haya ndiyo yaliyo tokea Sri Lanka, Ufaransa Afrika ya Kusini, Urusi n.k waandamanaji waliuawa, waliteswa, walipigwa na wengine kuwa walemavu lakini haya madhira hayakuwazuia na kuwa fanya wao waache kupigania haki zao kupitia maandamano bali waliendelea mpaka pale nguvu ya umma iliposhinda. na haya maandamano hayakutokea na kufanyika eti kwa sababu nchi zao zilikuwa na demokrasia inayoruhusu maandamano la hasha bali ulifika muda raia wakawachoka watawala wao hivyo ikawaradhimu kufanya maandamano ya nguvu.