Ben Saanane
JF-Expert Member
- Jan 18, 2007
- 14,580
- 18,230
Nianze kwa kunukuu kauli za mwanafalsafa wetu nguli Aristotle alopenda kuitumia
"It is a mark of an educated mind to be able to intertain thought without accepting it"
Kwamba nyakati nyingi bongo Za watu wanaojidhania wana darasa hupenda sana kunasabisha mawazo flan ingawa Kwenye mioyo Yao wanajua fika wako Mbali nayo.
Zitto waraka huo wa siri umekuweka pabaya, mbaya zaidi ni pale viongozi waandamizi wa Chama chako wametoka nje hadharani wakanawa mikono Yao juu ya sakata hili Na umejikuta huna wa kumrukia. Kila unayemsaka umrukie kiulainii anakukwepa. Hali hii inakulazimisha ufunge mjadala kitu ambacho hakiwezekani kama kuna ukweli.
Niwazacho Na nionacho ni Kwamba story hii ina chumvi kidogo hasa mbwembwe Za Mwandishi alipowakilisha lakini matukio karibia yote yanasound Kweli.. Na Kama yanasound Kweli Basi hofu yako kubwa ni Kwa hao uliofanya nao hiyo siri Na Kumbe kuna baadhi usiowadhania possibly wametorosha taarifa zako. Kuwasakama hao waziwazi huwezi Na ni jambo lisilowezekana utaishia kuwapigia cm tu "jamani mbona mmenifanyia hivi?!?" nao wanakujibu " aisee wala hatujui nani kafichua mpango mzima"
Na Kwa mantiki hiyo silaha yako kubwa ni kupambana ili jamii ielewe story hiyo ni ya kupikwa Na ukiwalenga viongozi wako ndio wanazi wakuu Wa pishi hilo ukilibatizia Kama propaganda Za kuchafuana wakati Chama kinakaribia uchaguzi Wa Ndani. Ukazusha mikutano kwenye kanda ya magharibi ambayo kuna sintofahamu ya Fedha Za mikutano Na nani mfadhili Wa mikutano hiyo maana Chama hakina taarifa nayo, Kwenye mikutano ukatoa matamshi agharabu Kiongozi mkuu Kama wewe kuwatamkia viongozi wenzako hadharani. Hii yote unachokoza kutokee fukuto Kwenye Chama ili wananchi maskini Sie tuelewe ni kweli viongozi wako hawakupendi Na kweli labda wamekupikia inshu.
Mbaya zaidi ni pale viongozi hawa waandamizi wakitoa kauli Za kunawa mikono "komplitili (Kama alivyopenda Kusema idd amini)" . Ripoti wamepinga haijatoka chamani, wameonyesha hawana wala hawajawahi kuwa Na Ugomvi nawe Na wala hakuna aliyekutolea majibizano au munkari. Hali hii inakufanya upwaye, utapetape, unaruka huku Na Kule hakuna anayejali you are doing something to let them react but this pipo gain zero interest from your action. Ni Kama Mtu anayetupa ngumi hewani. Kila unayemshika udondoke naye anakukwepa kimya kiulainii..
Sikiliza Kisima nikushauri, usiendekeze hizi maneno, accept the reality. Hatakama your action 100% was true but Hakuna NASEMA tena hakuna popote Action hizi zimekiyumbisha Chama chako zaidi ya kukiimarisha zaidi. CHADEMA HAIJAATHIRIKA POPOTE..!! So if this is the case badili ukurasa, badili mtazamo, elekezea openly mashambulizi yako Kwa hao uliotengeneza nao dili Na wape makavu laivu kwamba hukumwomba Mtu Pesa, walikutafuta Na kukuletea wenyewe Kwa Ujinga Wa Akili zao. Ata Mimi Mtu akiniletea hela ntazikataa vipi.. Unaji-Obi okonkwo Kwa Kwenda Mbele Kama kauli yetu mbiu Kwamba "Kula CCM Na Kura CDM" kumbuka vya mlevi huliwa Na mgema. Wewe bi jembe, wewe ni mgema hao ni walevi wa madaraka, wanaamini CDM ikifa Basi Na ulevi Wao utaendelea.
Nakushauri wabomoe mapema Na wakiendelea Kutaka kukutumia usikatae hela, hata mie nirushie gawio mwanangumwenyewe.. Nani anaichukia fedha ya bure..!!. Hujaiba Cha Mtu, hujadhulumu Mtu.. Mjingaflan anakuletea hela utaikataaje. Nakumbuka zamani mjibaba unakuita Nyuma ya nyumba yenu hasa nyakati za jioni ,unakukatia mshiko (akikupa shilingi moja inatosha sana bajia Kama ishirini shuleni kesho yake) halafu unakutuma ukamuitie dadako. Unachukua mshiko Wa ----- unaendazako Ndani unaendelea Na hamsini zako.
Usipo wapa makavu laivu, ukaamua kukaa kimya utakuwa Na wakati mgumu sana sana. Wao wanajifanya vinara Wa kuua raia, kunyofoa kucha bila ganzi waache wafanye wawezalo, liwalo Na liwe.. Wewe ni Jembe muhimu la CDM, Achana Na wajingawajinga wamashakuchafua sana Mbele ya Jamii.., timu yote ya watoto wa vigogo Wauza madawa ya kulevya ya Lumumba wanakushabikia wewe unaona kitu hiyo iko Sawa!, mie si shabiki wa mpira ila kama inacheza Yanga na Simba, kisha washabiki wa Yanga kwa nguvu wanamshabikia mchezaji flan mmoja tu wa Simba ambaye hachezi kiwango chake lazima simba wajiulize sana kulikoni huyu mwenzetu anayeshabikiwa na mahasimu wetu?!!. Njoo tumalizie kupanda pamoja mount 2015.. Njoo tuandike historia pamoja ya kufuta kabisa NENO CCM ifikapo 2016 asiwepo hata Mtoto Mwenye ham nayo.. Kumbuka KANU..
Duh........ ..Asubuhi Njema!