Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Safi sana, kuonea raia ifike mwisho.
 
Unaonenyesha wewe ni mjinga, hujui chochote kuhusu mapato ya serikali na matumizi ya mapato husika, nadhani unajua mwanajeshi zile pesa anazolipwa hazitoki pia kwa wananchi wasiokua wanajeshi(yaani kodi zao), na unadhani wanajitolea hawalipwi kwa kazi ya kusubiri vita vitokee miaka ya huko mbeleni.
 
Muro ni muhaya kama sikosei hapo ndipo shida ilipoanza,jamaa majigambo mengi ona sasa kafa kifala mno tena kwa aibu.

"Mwanajeshi auliwa kwa bisibisi."[emoji23]
 
wanajeshi ni wapuuzi sana, wao hata mwenzao akichukuliwa demu wanapiga watu.
siku moja nilikuwa natembea toka makongo kuja kupanda gari pale super. nikakutana na bwana mdogo mooja aliyevelia kiraia. kwakuwa ni usiku nikamuuliza jambo la kawaida ili aweze kunisaidia. alichokifanya mpuuzi yule ni kunishika tanganyika jeck na kuniingiza getini kisha akanipigisha magoti huku akitamka kwa nguvu ... hawa ndiyo wanatuchulia madem zetu na kutuua kule kawe nikabaki namshangaa tu. hadi alipokuja mwenzake mwenye akili kidogo nikamsimulia akaniambia niondoke
 
Hata polisi hasa wale field force unit squads huwa wanajiona ni miungu watu , kila siku wanapasuliwa na chupa huko kwenye mabar kisa ugomvi wa kipumbavu ,kugombea Malaya na raia
 
Angetumia busara haya yote yangetokea wapi sio kila mtu anapenda kuonewa

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Ndo hivo ni hasira baana ya kuzabwa kibao

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
 
Hata polisi hasa wale field force unit squads huwa wanajiona ni miungu watu , kila siku wanapasuliwa na chupa huko kwenye mabar kisa ugomvi wa kipumbavu ,kugombea Malaya na raia
Kwa hio wanajeshi wote unaowana ni sawa na kuanza kuwavimbia na kuwatukana unavyojisikia na kutaka kupimana nao nguvu si ndio?
 
Na sio mara ya kwanza hao wapumbavu kuuawa, kuna mwingine wa cheo cha copral aliwahi kuuawa kule kigamboni, kisa ni huo huo ubabe wa kipuuzi.
 
Mimi ukiniletea useng£ wa kunishambulia , tunazipanga ngumi na nahakikisha nakufumua na kukutoa ngeo ili ikome kabisa , sita angalia umevaa gwanda wala matambala ya batiki , ukinishinda kwenye ngumi hata silaha au nawe natumia mpaka nihakikishe nimetia adabu .
 
Angetumia busara haya yote yangetokea wapi sio kila mtu anapenda kuonewa

Sent from my HUAWEI MLA-AL10 using JamiiForums mobile app
Kuna sababu, hawezi mtu akakuzaba makofi pasinakua na sababu yawezakua wewe ni mtovu wa nidhamu umemtusi km afanyavyo huyu member humu Don Vill hivi huyu aanze kuporomosha matusi mbele ya Askari na kumvimbia unadhani nini kitafuata? Mtu anatukana viungo vya mama yake anavitaja bila kua na staha unahisi nini kitafuata?,
 
Yeye katangaza vita dhidi yenu.
Mimi nawaambia tumieni busara.
Ila ukija kwa shari nakushari pia.
Wala usinitishe.
Form 4 failure unavimba vimba barabarani. Tuheshimiane.
Punguza chuki za kijinga, form 4 failure ndio mlivyokaririshwa kua kila Askari ni form 4 failure? Acha kua mjinga chagua kua mwerevu,
 
Hawez achwa huyo cheo cha kanali jeshin ni kikubwa sana na hpo serikal ishapoteza hela nyngi sanaaa kumsomesha.

Hpo weng watabebwa na weng kurud sjui
Kas0meshwa lakini hakus0ma. Sina huruma na watu kama hawa wana0jina waungu kwa sababu ya che0. G00d riddance
 
Kwa hio wanajeshi wote unaowana ni sawa na kuanza kuwavimbia na kuwatukana unavyojisikia na kutaka kupimana nao nguvu si ndio?
Kujumuisha askari wote, kuwa wana tabia za uonevu, siyo sawa, kuna askari wengine ni wema sana. Elimu inabidi izidi kutolewa kwa askari, namna ambavyo wanatakiwa kujibihevu uraiani, na siyo kufanya ndivyo sivyo.

Watu wengi inaonekana walishajengewa chuki, kwasababu ya yale ambayo walishatendewa au kuyaona yakitendeka kwa wenzao. All in all, elimu iendelee kutolewa kwa askari, ili kuepusha vitu vinavyoweza kuepukika. Inauma sana, askari kapoteza maisha bila kutarajia.

Laiti (askari), anfejua ambacho kingempata, hakika siku ya jana, asingetoka kambini na akaenda kunywa pombe alipoenda. Pole sana kwa ndugu jamaa, marafiki na familia kwa ujumla. Pole sana na kwako pia mkuu, nimeona umejitahidi sana katika komenti zako, kutusihi sisi wananchi tusiokua wanajeshi, kuacha chuki dhidi ya askari, hii inaonyesha wewe ni mtu usiyependa shari.

Tukio la huyo askari, liongezeke kwenye mifano halisi uliyonayo, na likuongezee ari ya kutaka kujua kwanini chuki ipo kati ya wananchi wanajeshi na wananchi wasikokua wanajeshi. Pole sana.
 
Soma CPA kasome defensive factors ambazo zinaweza kukulinda usiwe liable.Utaelewa.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…