Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Kawe leo hii kuanzia Saa 1 hadi Saa 3 Usiku kulitokea nini hadi MP wa JWTZ Kufurika, Kukamata Watu, Kutembeza Kichapo na Kuzua taharuki?

Wanajitolea au wanalipwa?
Mkuu nijuavyo mimi,wanajeshi wanalipwa mishahara na posho kwaajili ya kutimiza majukumu ambayo yanawapasa.Mimi nawewe,tunalipa kodi,ambazo hizo kodi zinalipwa kwa kila askari wa JW na kada nyingine.Ukisema sisi tumelala,wengine wanatulinda,hujui kuna bodaboda wanakesha pia,kutafuta pesa au kuna madaktari wanafanya C-section usiku huu na yawezekana wakakesha,huku baadhi ya wanajeshi ambao hawako shift usiku huu,wamelala au wanalewa?
Heshimu kila mtanzania.Tunaumia kulipa kodi,ili mambo yaende,kila mtu anapambana kwa nafasi yake.


wanajeshi hawalipwi mshahara wanapata posho. kazi ya kujitolea hainaga mshahara.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Basi nae jamaa alikuwa analinda heshima yake.
 
Majeshi ni vyombo vinavyotumia nguvu katika utekelezaji wa dhima ya uwepo wake. Hivyo, ni vema kila raia akawa anatambua na kuliheshimu hilo.

Vilevile majeshi huwa na utaratibu wake wa kulinda taswira na hadhi za majeshi hayo. Hivyo, aina yoyote ya kuyakosea adabu hadharani, ni lazima ile kwako.

Pekee kinachohitaji majeshi haya toka kwa raia ni kuheshimika tu. Ukithubutu kumvunjia heshima Mwanajeshi yeyote yule, Wadepo wenzake hawatakuacha.

Wadepo hubaki kama familia hata kama watapangwa kwenye kambi tofauti. Watakikusanya tu wakujie kwa ajili ya heshima ya jeshi.

Ova
Huu utumbo , mchafu
 
Sema washua wenye mamlaka huwaga wanajisahau sana , Kuna video nmeona mtandaoni Kuna dogo alikua anaendesha ist alichomekeana na land cruiser flan nyeus jamaa akaamza kumletea ubabe wa ki CIA dogo road kila akienda huku jamaa linamzibia njia dogo akaenda TikTok live akawa ana broadcast the whole shit maana alishahis hatari jamaa kufika makumbusho aka block njia akashuka kwa gar akaonekana na suti yake ya uzalendo nadhan alipigia wadau wakatoka mule chimbo lao la idara wakamuongoza dogo kuingia tunduni aku anaendelea kurusha mubashara tukio watu wa mabaka ya kenge wakashtukia kama mwamba anawarekodi ndo nkajua kabisa mwamba kaisha mule ndani kamera hapapatani kabisa na msala wa dogo sidhan ata familia yake kama inaweza kuusovu labda kwa vile sura za wahusika ziko online zinaweza kutumika kwenye mahakama za jadi kupata haki kama hakuachiwa lakin
Wale wana usalama kw mujibu wa report(kama zilikuwa za kweli) walishughulikiwa na vyombo husika "kinidhamu"
 
Hapa najaribu kufikiria wanachomfanya huyo kijana saiv hadi Akili imenikataza kufikiri.
Ninachokijua tu ni kwamba huenda kuanzia leo hata Kuukweka ( Kunya ) akashindwa kwa Siku 7 au 14 zijazo na asiwe na Uwezo mzuri wa Kuona huku Mwili ukiwa Umeumuka ( Umevimba ) sana.

Wewe Umezabwa tu Vibao unakimbilia Bisibisi na kwa Kuongozwa na Bangi zako na Gongo zinakutuma Umchome Mtu ( tena Mjeda na kumsababisha Umauti kama inavyosemekana ) kwanini yasikukute tu?

Mwenyezi Mungu hakuwa Mjinga kutuwekea Mawe ( Vitofa ) kwani hata Nguli ( Legend ) wa Sanaa ya Mapigano ( Martial Arts ) Marehemu Bruce Lee alishasema kuwa ukiona unayegombana nae humuwezi Kimapigano Chagua Vitu Vinne vifuatavyo...1. Kuachana nae huku ukijipanga Kummaliza taratibu Kimafia, 2. Kutoka Baru ( Kukimbia ), 3. Kumng'ata na 4. Kuokota Mawe na Kumpiga nayo kwa Kumrushia ( Palestine Style )

Kama namuona vile huyu Dogo aliko.
 
Nenda kasome jukumu la 3,4,na la 5 la JWTZ
Akasome wapi wamewakuta Raia wapole ingekua kama Disouza watu nao wana siraha wangeenda kupiga watu na mikanda yao Watanzania sio violent hata kwenye haki yake hapo unamkuta abiria mgonjwa hajui hili wala lile nae anapigwa tuu...waendelee kuwapiga ila ipo siku watajuta kufanya huo utoto wao...
 
Sasa amekuchoma na bisibisi umekufa,wakati labda ungemuelimisha tu,kua dogo ngoja nipite,au unatumia saikolojia tu,mnayamaliza.
Ni kweli kabisa,kuna majibizano ya kijinga tu yanaweza kuleta maafa.
Natoa mfano.
Kuna bwege mmoja bouncer hivi ana bibi yake mrangi ni mzuri ila umwangalie sana.
Sasa jamaa akawa anamfata mitaa yake ya kazi(changudoa) tena wale wa barabarani kabisa
Mara siku kuna Mwamba katoka zake huko,
Hakua na huyo bibi,
Bibi yuko mbele jamaa anakuja nyuma yake nae katoka kwingine kabisa.
Yule Bouncer kuona wanakuja wameongozana kajua huyu ndo mgoni wake kwa( changudoa)
Kamrukia mshkaji pigana sana,
Alipoona unga unazidi kavunja chupa kaanza kumchana nayo jamaa tumboni.
Bahati nzuri bibi yake mwenyewe alikimbilia kusema kwa watu kijiweni kuna mtu anauliwa huku
Likaja Nyomi kufanya uokozi.
Bouncer kakimbia.
Yule jamaa katibiwa kapona baada ya muda sana akaenda eneo la tukio ,kamkuta yule mwanamke kwanza kamtafuna na mwanamke akatoa tips zote za jamaa yake.
Yule bouncer kilichomkuta anakijua mwenyewe.
Ndo tunasema usimchokoze mamba akiwa kasinzia.
Akiamka utatafuta pa kutokea.
KAPAFONA
 
Back
Top Bottom