Kaya 644 Magomeni kota zagomea kusaini mkataba kununua nyumba

Sijaelewa,ina maana wale waliokuwa wanamiliki tayari kota zao kipindi hicho katika eneo hilo nao wanalipishwa hyo bei tajwa au wanakabidhiwa tu mijengo yao?
 
Serikali ikubali kuingia hasara wawaache tu waendelee kuishi hapo
Mbaya Zaidi 90% ya hizo Kaya sio wakazi wa Kota.

Hata Mimi muda Fulani niliwambiwa nitoe 1 million ili niandikishwe kama mkazi wa Kota.

Serikali uzeni nyumba hizo kwa bei hizo hizo mlizoelekeza,,

Pana mchezo mchafu hapo Kota.

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
Taslima amesema, "Njia mojawapo ya kuchukua ni kuiomba Serikali au kwenda mahakamani. Bei ya chumba na sebule kwa Sh48. 5 milioni na vyumba viwili na sebule Sh56.8 milioni inaweza isiwe rafiki na mnunuzu asimudu," alisema Taslima.
Ila kuna vitu vinafikirisha sana. Hivi kwa mfano huo mkataba ukasainiwa na wakauziwa nyumba kwa milioni 12. Baada ya mwezi huyo huyo aliekua analia anaiuza kwa bei ya juu kisha anahamia kwenye eneo ambalo wanakaa kwa kutazamana makorido. Watanzania watakaofaidika hapo ni wenye mkono mrefu. Anyway sijui nani alikuja na hilo wazo ila acha ninyamaza
 
Umeniwahi kidogo tu mkuu. Tuna mawazo sawa. Something fishy is going on hapo. Kuna mtu ananyumba hadi zaidi ya tano ila anawasukumizia wazee waseme wataishije. Sasa mzee wa miaka 82 hata akipewa kwa milioni 12 atailipa kwa mda gani?
 
Sijaelewa,ina maana wale waliokuwa wanamiliki tayari kota zao kipindi hicho katika eneo hilo nao wanalipishwa hyo bei tajwa au wanakabidhiwa tu mijengo yao?
Hawakuwahi kumiliki Kota,
Walikuwa wapangaji tena wakikaa miaka mingi Bila kulipa Kodi.

Ifike mahali serikali isimamie inachoamini.

90% ya wakazi wa Kota sio wenyewe halisi..

Wanataka wapewe kwa pesa ndogo na wao wauzie watu wengine.
Kama zilivyokuwa NHC .

Sent from my 2201117SG using JamiiForums mobile app
 
I read sense! Mtu anataka nyumba iliyopo magomeni auziwe kwa 17 milion? Seriously?? Pale si karibu kabisa na mjini. Hata mpiji tu hupati nyumba kwa milioni 10 sembuse magomeni. Wajengewe chanika. Simple
 
True kabisa mkuu ulichosema,thamani ya vile vijumba vya zamani na hz ni tofauti kabisa
 
Tukiweka siasa pembeni hizo nyumba wachague 1 walipe au wapishe wengine wakae.

Sasa tutalaumu hadi lini?
 
Hapo kuna wanasiasa wameingizwa tayari
 
Kumbe ni wapuuzi kiasi hicho,wao wapewe ni nani,kwa nini watanzania wengine wasipewe kama wao kumbe ni wapangaji tu?

Serikali isimamie hapo hapo,haiwezekani wapewe nyumba bure kwa jasho la watanzania wote,hata sisi tunazihitaji pia.

Kama wamepewa favor ya kuuziwa wao kwanza kama wapangaji na hawataki kuitumia,waziache nyumba zetu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…