Nilipohitimu law (Sheria ) nilitamani kubadili Dunia Ila pesa nlikuwa sipati kwa wingi, ilikuwa mshahara tu ,japo enough but sio nyingi .
Miezi miwili baadaye nlipitana na mshkaji hajasoma anapiga Hela ndefu kuniliko , nlibadili Nia . Siku hizi bwana madili ndo kazi za mawakili wengi ,kwa miingiliano yangu na wafanyikazi serikalini nmegundua asilimia 100 wote wezi .
Utapata ofisa TRA kabisa anakuja uumpe ideas on how to legally steal money ,na jinsi gani kuipitisha tax havens Kama cayman asipatikane .
Mfano wa mwisho ,Kuna contractor ,alinijia juzi juzi tu ,jamaa kapewa tender za kazi huko kusini , tender millioni 400 ,hakufanya kazi yyte , bingwa alinipa direct instructions niwash Hela yote kwa banking system mpaka Bahamas ,kumuuliza mbona hafanyi kazi angalau hata Kama sio yote ,alinipa jibu ,wao ndio walimwengu ,mabaharia huruma hawana.
Ila nchi hii inavyoporwa, dadeki, balaa tupu , Ila Nala nao na faida ipo tu .
Utajiri wa haraka Yaani quick riches ,lazima mlango wa nyuma lazima ,na ukiugeukia ndo hazina zipo .
The end justifies the means .