Kazi nilizowahi zifanya na zikanishinda kwenye utafutaji

2014 napiga vibarua vya ujenzi nikakutana na mshikaji wangu mmoja anaitwa baba bahati....baba bahati akanipa connection ya kumwaga zege..
 
Mleta mada amenikumbusha mbali Sana,nakumbuka Nilikuwa ndio kwanza nimemaliza masomo ya 'O' level Niko nyumbani naisikilizia matokeo ya mtihani.

Ghafla nikapata mchongo was kwenda mini kutoka kwa mshikaji wangu mmoja.Akaniambia yupo rafiki Yake anatafuta mhudumu wa bar afu mshahara KSh 5000 kwa mwezi.Jamaa nikajiandaa chap boss akanitumia nauli nikaliamsha kwenda kazini.

Nilifika huko nikakuta mazingira ya kufanyia kazi Ni magumu Sana.Mdosi alinipa tu chumba pamoja na vitu vichache vya ndani Kama bile godoro meza,sahani 2 vikombe 2 na stovu.Kuhusu chakula akanambia kila siku atakuwa ananiachia crate mbili za pombe za viena niwe nauza mida za asubuhi na mchana.Ikumbukwe kwamba kipindi hiko ilikuwa marufu kuuza pombe nyakati za asubuhi na mchana.Pombe ziliruhusiwa kuanzia saa 11 jioni kuendelea.

Sasa mdosi akaniweka kwenye risk,akaniambia niuze kwa umakini Sana nisije nikabambwa na wajeda.Kwa hiyo nikawa nauza hizo pombe ili nipate hela ya kununua chakula,maji,sabuni na mahitaji mengine.
Crate Moja Nilikuwa naiuza kwa jumla ya KSh 1000.Sasa Nilikuwa Nampa mdosi sh' 750 afu zilizobakia 250/- Ni kwa ajili ya matumizi yangu.

Nikiendelea kuuza hizo pombe nikawa napiga hella nzuri Sana maana kwa siku ninaweza kuuza crate mbili maana Yake hapo nitakuwa nimetengeza ksh 500.

FAST FORWARD.Ilifika mahali boss wants akabadilika sana.Akawa Ni mtu wa visirani visirani mixer kunitukana hovyo hovyo.Nakumbuka wakati wa usiku alikuwa anakunywa pombe Hadi zinamlemea afu ananiambia nimsindikize pole pole Hadi nyumbani kwake maana hakuwaga na chombo Cha usafiri kipindi hiko.Sasa jamaa Nilikuwa Natembea masafa ya kilomita Moja usiku saa tano namsindikiza boss wants Kisha nirudi mwenyewe kwenye nyumba yangu.
Hadi ilifika wakati boss akaniachisha kuuza pombe za asubuhi na mchana eti alikuwa anawahofia polisi wanaweza kuja kumtaitisha muda wowote na kumfungia biashara Yake.Jamaa nikaacha kuuza pombe nikawa nasubiri zamu ya jioni tu.

Tangia hapo life lilikuwa gumu zaidi.Hela nilizokuwa nimejisevia zikakata.Nikawa sina uwezo wa kununua chakula Wala maji.Kila nilipojaribu kumwomba mwajiru wangu usaidizi alikuwa ananifokea sana Akakataa kunisaidia hata hela ya advance eti nisubiri mpaka mwisho was mwezi.Nilijikaza kiume japokuwa life lilikuwa gumu Sana.Nilikonda kiaina.

Sasa kilichonifanya nishindwe kuendelea na hiyo kazi Ni pale mwajiri wangu alipoamua kumleta jamaa mwingine wa kusaidiana mazi naye.Cha ajabu,kumbe jamaa alikuwa mwizi Kuna siku alinilia timing wakati nilienda sehemu ya kazi kuchukua stock jamaa naye akatake advantage akaamua kuinua vitu vyangu vyote akaseoa mazima.Nikabaki na nguo za mwilini na simu tu.Nikajaribu kumweleza boss wangu Ila hakuchukua hatua yoyote kunisaidia.

Nilichofanya nilimsihi boss wangu anirudishie kitambulisho changu nirudi kwetu.Ukumbukwe Nilikuwa nimebakiza siku 3 nimalize mwezi.
Mdosi alinipa kitambulisho changu ika hakunipa hata sh' Moja.Kilichonisaidia Ni usiku wa kuamkia hyo siku nilikuwa nimeshinda hela ya mkeks Ksh 4300.Nilitumia kiasi Cha hyo pesa Kama nauli nikarudi kwetu.
 
😂😂😂 umenikumbusha jamaa angu mmoja wa kuitwa bakayoko nakumbukuka aliingia site akiwa nywele fresh tu lakini mpaka kazi ya kumwaga zege inaisha mwamba nywele za katikati ya kichwa akawa hana
 
Pia kingine kazi ya site aseee inataka uzoefu kuna watu ndo life lake kazi nyingine hataki ni mwendo wa site !! Na walio wengi wanakula kijiti
 
Kuna watu wako speed kinoma !! Halafu kwenye kumtwisha mtu naogopa kinoma unaweza ukamtupia mfuko wa cement vibaya ukamvunja !!!
 
Mkuu hiyo inaitwa "KUSOTEA" mwajiri akija mnapigana vikumbo ikifika mida ya mchana kila mtu anasepa kesho mapema tena
 
Kuna watu wako speed kinoma !! Halafu kwenye kumtwisha mtu naogopa kinoma unaweza ukamtupia mfuko wa cement vibaya ukamvunja !!!
Kumtishwa mtu ni kazi ngumu achilia mbali kumtishwa mtu vibaya ila Kuna mziki wa kuvuta mfuko kuanzia katikati mpaka mwanzo wa kontena ni balaa na nusu ni heli wote muingie Kila mmoja ajitishwe mwenyewe
 
Kazi za viwandani sio simple kabisa Kuna movie Charlie Champlin alikuwa anafanya kiwandani if I'm not wrong ilikuwa inaitwa modern times ilikuwa inatakiwa aende na speed ya mkanda matokeo yake alipata pyschology effects.
 
Some time that's nasemega Kama Mungu amekupitisha yote alafu akakufungulia Milango , usijinyime Sana , FANYA maendeleo but pata mda wa kurelax,

Watu ambao tumetokea familia za chini mpaka kutoboa tunayapitia Mengi,
 
Some time that's nasemega Kama Mungu amekupitisha yote alafu akakufungulia Milango , usijinyime Sana , FANYA maendeleo but pata mda wa kurelax,

Watu ambao tumetokea familia za chini mpaka kutoboa tunayapitia Mengi,
Hakika mkuu. Kuna time ukiona mtu anaenda kwa sangoma kutafuta za kichawi muache tu kasota shida sio kitu kizuri.
 
Kumbe jf kuna hadi kazi za hivi, mnatuvuruga kwakweli

Huu ndio Uzi wetu wazee wa kazi, achana na zile mambo sijui range Rover, my house Mara viwanja vikali kumbe hata chai haujaonja, hapa ni wapambanaji. Unasoma nyuzi Hadi unajiona peke Yako ndio umekosea ramani. Watu wote JF mambo matamumatamu.

Nikiweka shughuli zangu hapa jambo letu litaota mbawa, mpango mzima utafariki.
 
Hakika mkuu. Kuna time ukiona mtu anaenda kwa sangoma kutafuta za kichawi muache tu kasota shida sio kitu kizuri.
Kweli mkuu, sisi watu tuliotokea familia za sayari ya tunayapitia Mengi mpaka kutoboa, mbaya unajikuta wewe ndo mtoto wa kwanza,familia ipo na umaskini wa kutupa, unaanza pambana na kukomaa kimaisha hata kabla ya umri,ila bwana Mungu huwa anatupigania
 
Sasa project itakuaje si ulisema una range my wangu
 
is it ok to be A man?

Its not ok,its necessary,

Wha the hell we gona do without Men?
You look around the city here,you see all these buildings go up! Its men that are doing imposible things
They are under the streets working on sewers
They're up on Powerlines,in the storms,in the rain
They're keeping these infrastructure Functioning
This thing that works in Miracles manner
They're working themselves to death
And often litereally the gratitude for that,is sorely lacking sp[ecialy among the people who should be ost gratefull
The social Justice bentwho are among the most protected and the privileged people the world has ever produced
They take everything they have for granted
Failing to understand that,there's always massive infrastructure of unbelievable hard working
Solidly laboring working class men
Breaking Themselves in half on a regular basis,Making sure that everything that always breaks Works

Your browser is not able to display this video.
 
Kuna jamaa yangu namheshimu sana, na ni mfano wa kuigwa.

Tulikutana wakati tunasubiria matokeo ya form four. Tukawa marafiki anakuja nilipokua naishi na ndugu yangu maisha yakaendelea. Majibu yametokea nikapangiwa kidato Cha Tano, yeye hakubahatika awamu ya kwanza, nipo shule akaambiwa amepata second selection, wakati huo Hana ada Wala nauli, yule ndugu yangu niliyekua naishi nae akampatia nauli na pesa ya kujikimu akaenda shule.

Tuliendelea kuwasiliana na likizo tunakutana Dar. Baada ya kumaliza kidato Cha sita, sikukaa sana mtaani, nikajisemea mambo ya IT, Kuna mmama akanipa sehem nimfanyie kazi yake ndio ikawa mwanzo wa kuanza ukurasa mpya wa maisha yangu. Turudi kwenye hoja ya Rafiki yangu...

Alikuja nayeye akawa pale nilipokua ila akawa eneo lingine, alikua mtu wa hasira alileta varangati akamtwanga ngumi mtoto wa boss, nimeitwa kutoa ushahidi ilikua siku ngumu sana kwangu, nikisema ukweli, jamaa kazi Hana, nikiongopa, tunaweza kupoteza wote kazi na kuvunjia uaminifu wote nilionijengea. Nilikua mkweli jamaa kazi ikapotea lakini tuliendelea kuishi wote.

Baada ya muda akapata kazi laundry Moja wanafua nguo za mahospitalini, alifanya Kwa muda akapata kazi hoteli flani mambo yakawa mazuri sana.

Wakati huo mie niliondoka pale nikapata eneo lingine zuri zaidi, napiga dai na kukwea daladala za Posta. Nikaona maisha si ndio haya?

Jamaa yangu akavuruga Tena huko hotelini, akawa anapiga zege site mie sikuwa na taarifa, nilikua nashangaa alirudi jioni kachoka hatari anajirusha sakafuni usingizi mzito. Tulikua hatupiki ila ntanunua chochote kuleta geto, alikuja kunihafithia baadae machozi yalinitoka.

Baada ya hapo akapata zile kazi za parking Posta, unajua aliweka aibu pembeni, Posta inakutana na watu umesoma nao wengine wamekufaham ukiwa na kazi nzuri, jamaa hakuangalia hayo yote aliifanyia kazi yake Kwa moyo mkunjufu na zile sare zao.

Alikuja kupata Tena kazi clearing and forwarding ndio ikawa ticket yake ya kutoka, tunavyoongea ameshahamia makampuni matatu, amepata degree yake, amepata nyumba yake Madae, Kapiga hatua sana. Ujasiri wa kuweka pembeni aibu ndio hua namsifia huyo jamaa. Uzuri tumeendelea kuwa marafiki tumekua kama ndugu Sasa.
 
Mi hiii ningemaliza, 150k ya bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…