Mtu ambaye anaweza kuwa na uwezo wa kukusanya taarifa na kuwapelekea wahusika na hao wahusika wakaamua kuzifanyia Kazi kwa usahihi pasipo kulenga kumuumiza mnunuaji au muuzaji kisha wewe ukafaidika na ile asilimia chache hapo unakuwa umefanya Kazi vizuri.
Ila watu wanaojiita madalali kwa bongo wengi hawajui Namna ya kuifanya hii Kazi zaidi ya upigaji .
Wachache Kama Silent ocean , Hassanary sound , Dalali Mwanamke wanapata Sana pesa kwakuwa hii kwao ni Kazi Ambayo wanafanya kwa kufata utaratibu maalumu.
Mimi ninao wakubali ni wale ambao hufanya Kazi ya kuuza bidhaa ya mtu na wao kulipwa aslimia kadhaa na sio kitu kinauzwa mil 4 wewe unauza mil 5 yaani. Unapata faida kumzidi mwenye Mali na hapa ndo utapeli uzaliwa.