Kazini kwangu ninaowasimamia hawanisikilizi, naomba ushauri

Ukanda huo wapo hivyo, wanapenda Sana kujinyanyua na kujionesha kwamba wamakua Ila Ni waoga Sana.

Ulitaka watambuemakosa yao, hebu Kama Ni usafi fanya mwenyewe Tena mbele yao bila kuwaambia kitu.
 
Katafute dawa ya heshima yaani ukichanjwa hiyo ukifika kazini unakuwa unaogopwa kama simba
Hata awe boss anaufyata

Vingibevyo wewe ndio utafukuzwa kazi, hao wafanyakazi wananamachimbo yao kuna sejemu huwa wanaenda ndio maana wanakiburi
 
Mungu akusaidie, kama umepewa uongozi, na watu wanakudharau na haujui cha kufanya, mwombe Mungu akupe kazi nyingine, wee sio kiongozi. ungekuwa kiongozi usingehitaji hata kuuliza hapa.
 
Akileta mambo ya kwenye makaratasi kwa wamakonde niamini mimi atafukuzwa kazi ndani ya wiki moja

Hana confidence inabidi akajipange kiroho ndio awavae hao watu vinginevyo atakuwa jobless muda sio mrefu
 
Ongoza kwa mfano

Msimamizi: fagia
Mfanyakazi: sitaki
Msimamizi: chukua ufagio ufagie
 
Dah! Aisee mbona mambo ni magumu kumbe unakuwa unatengeneza vita Tena juu
 
Don't show them who is in charge! Yasome mazingira, waelewe wao wanataka nini then itakuwa rahisi kwako kuwaongoza.

Mpaka uongozi haupo tayari kuachana nao maana yake wao wanaweza kuwa mhimu zaidi yako wewe ama wamekuwa sehemu ya taasisi au biashara husika kwao hivyo ni watu mhimu.

Leadership is not about holding power or position, it's all about inspiring your people.
 
Kuna kitu hakipo sawa na ukilazimisha mambo yasiyowezekana shauri yako kikwete alisema la kuambiwa changanya na za kwako.
 
Hao nenda nao kimkakati, kwa sababu ninachoona wanataka kukuonesha kuwa wao ni wakubwa kuliko wewe. GIVE THEM WHAT THEY WANT.

Cheza na akili zao, wape fursa ya kujiona wakubwa, wape fursa wajione wao ndio waamuzi na wako juu yako.

Let them feel superior while you stay very low and submissive but watchful.

Wakishajaa kwenye mfumo utaona wanaanza kufanya kazi kama MANYUMBU tena kwa hamasa huku wakiamini wao ndio viongozi.

Au pita katikati yao UWAGAWANYE.... teua mmojawao awe kiranja wao, au teua watano wawe viongozi wa wenzao.... kisha hao watano uwape motisha kubwa ili WAWASIGINE WENZAO. KWISHA KABISA.

Tumia kila mbinu na kila mwanya unaopatikana kuhakikisha hawana umoja, tumia rushwa, upendeleo, fanya uonevu kwa baadhi yao, toa zawadi kwa baadhi huku wengine ukiwanyima, wape uongozi baadhi yao, tumia mgawanyo wa jinsia, mtengeneze adui miongoni mwao ili wang'atane wao kwa wao,... hakikisha unawavuruga huku wewe ukiendelea kujenga mamlaka yako na hakikisha wanakuona kama MKOMBOZI na MTETEZI.

Cc: Lamomy mshamba_hachekwi Nguva Jike Mia ya noti Mr Devil heartbeats min -me nipo online Ngurukia Evelyn Salt Gidamnyoda Alubati kwa-muda wakunyonya Yoda olegunasoljer ScaniaR Mkanganyiko kukanganya sysafiri zerominus10 safuher DR HAYA LAND Dr am 4 real PhD Norshad Lycaon pictus Kama ipo ipo Kimwakaleli Equation x Uhakika Bro MKILINDI Yofav @
 
ila bachelor ya business management hukuipata bure
 
Msimamishe kazi mmoja wao hasa anaye jiona kiongozi wao kwa mda
 
Acha ujuaji ni either uingie kweny system au ufunge domo deal na yako😅
 
Kama mabosi wanasema uende nao hivyo hivyo. Hefu fanya kitu kimoja, kesho wachangamkie halafu nenda ofisini tulia tulii usimwambie mtu kuhusu majukumu yake hata kama utaona kuna sehemu hawajafanya usafi.

Kuna watu wanapenda ligi. Jinsi wewe unavyoumia kuwaelekeza ndiyo furaha yao huku wewe unaweza kupata hata presha.
 
Kwani mkataba wao wa kazi unawapa majukumu gani na je wasipoyatimiza wanachukuliwa hatua gani?
Ila yote ya yote Acha unoko kazini busara itumike zaidi.
 
Fanya hivi nyamaza usiwaulize chochote hata wafanye vile wanavyotaka wao au kaa nao mjadili kuwa nini kinawapa ugumu katika kazi zao kirafiki tu.
 
Dah! Aisee mbona mambo ni magumu kumbe unakuwa unatengeneza vita Tena juu
Yah hamna maisha mepesi, kadiri unavyopanda madaraja unakaribisha maadui wapya
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…