Kelele za Tundu Lissu akiwa Ubelgiji ni sawa na fimbo ya mbali isiyoweza kuua nyoka. Arudi bongoland kuweka mbinyo wa kisiasa

Nilikuwa namkubali kwa kujenga sana hoja ndani ya bungeee

changamoto kila zama na mambo yakeee / siasa ni zaidi ya nijuavyo

angepunguza jazba na hasira vingemsaidia sanaa
 
..sio jambo la ajabu kwa WANAHARAKATI kulazimika kuhama nchi zao kwa muda.

..Tunao viongozi wengi wa Afrika ambao wamepata kuishi uhamishoni, kwa mfano Thabo Mbeki, Jacob Zuma, Robert Mugabe, Sam Nujoma, Emerson Mnangagwa, na wengine.
Lisu mbaya wake alishakufa! Sasa kinachomkalisha ubelgiji ni nin?
 
Wapo wengi walioyaweka Maisha yake rehani,waliombambikia vyesi vyesi vya uchochezi, na wale waogopao mwangwi wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, na wale wasio heshimu haki za msingi za raia pamoja na uzingativu wa sheria na katiba yetu. Hao wote wanamwogopa kama moto.
 
Fimbo ya mbali haiwezi kuua nyoka hata kidogo. Lazima iwe karibu na kumfikia nyoka na kisha kumuua.

Lissu yupo Brussel anakula bata kwa mrija, lakini ana malalamiko mengi juu ya mambo yanayotamaraki hapa Tanzania.

Analalamika juu ya kutokuwa na katiba inayokidhi mahitaji ya watanzania. Hivyo anataka Tanzania wapate katiba mpya. Sasa akilalama akiwa Brusels ndio ujumbe utafika vizuri? No anatakiwa aje hapa bongo.

Analalamika juu ya utawala usiofuata sheria na kubambikia watu kesi. Mfano anadai kuwa Mbowe amebambikiwa tuhuma za ugaidi. Lissu aje Tanzania na awasaidie watu kama Mbowe ambao wanaoenewa. Maana msaada wake ni mahakamani.

Kwa ujumla Lissu ana malalamiko mengi ambayo kimsingi hawezi kuyafikisha akiwa Brusele anakula kuku kwa mrija huku anasikiliza rhumba la Kikongo.

N.B . Idugunde ni member wa Jf anayeishi Igunga akifanya kilimo cha Mpunga. Sio mwananchama wa chama chochote kile.
Ajabu fimbo hiyo imekubutua hadi umekuja kuanzisha uzi baada ya kusikia maumivu yake, isingekuwa na maumivu sidhani kama ungeanzisha uzi
 
Wapo wengi walioyaweka Maisha yake rehani,waliombambikia vyesi vyesi vya uchochezi, na wale waogopao mwangwi wa katiba mpya na tume huru ya uchaguzi, na wale wasio heshimu haki za msingi za raia pamoja na uzingativu wa sheria na katiba yetu. Hao wote wanamwogopa kama moto.
Lisu ni mwansheria nguri na msomi kweri kweri?

Sasa anaogopaje vikesi kesi?
 
Harakati huzaa matunda ikiwa tu zinafanyikia home ground. Ndio maana hata Anc walikuwa wanarudi kufanya mashambulizi nyumbani.

..baadhi wanatakiwa wawe ndani, na wengine nje.

..jambo lingine serikali iongeze uhuru wa watu kufanya siasa.

..nadhani kukiwa na uhuru wanaharakati hawatahitajika. Hutasikia Mtz anapiga makelele akiwa nje ya nchi.
 
Fimbo ya mbali haiwezi kuua nyoka hata kidogo. Lazima iwe karibu na kumfikia nyoka na kisha kumuua.

Lissu yupo Brussel anakula bata kwa mrija, lakini ana malalamiko mengi juu ya mambo yanayotamaraki hapa Tanzania.

Analalamika juu ya kutokuwa na katiba inayokidhi mahitaji ya watanzania. Hivyo anataka Tanzania wapate katiba mpya. Sasa akilalama akiwa Brusels ndio ujumbe utafika vizuri? No anatakiwa aje hapa bongo.

Analalamika juu ya utawala usiofuata sheria na kubambikia watu kesi. Mfano anadai kuwa Mbowe amebambikiwa tuhuma za ugaidi. Lissu aje Tanzania na awasaidie watu kama Mbowe ambao wanaoenewa. Maana msaada wake ni mahakamani.

Kwa ujumla Lissu ana malalamiko mengi ambayo kimsingi hawezi kuyafikisha akiwa Brusele anakula kuku kwa mrija huku anasikiliza rhumba la Kikongo.

N.B . Idugunde ni member wa Jf anayeishi Igunga akifanya kilimo cha Mpunga. Sio mwananchama wa chama chochote kile.
Atakuja uchaguzi ukikaribia maana ni nyoka msakatonge.
 
Kwa hiyo atafia ughaibuni?

..haya mambo ya vifo watu wanaya kompliket sana.

..wewe unauliza kama atafia ughaibuni badala ya kwao Tanzania.

..usishangae kuna mwingine anauliza kama atafia mjini / Dsm badala ya kwao Ikungi.

..kila mtu atakufa mahali na kwa namna atakayopangiwa.
 
Fimbo ya mbali haiwezi kuua nyoka hata kidogo. Lazima iwe karibu na kumfikia nyoka na kisha kumuua.

Lissu yupo Brussel anakula bata kwa mrija, lakini ana malalamiko mengi juu ya mambo yanayotamaraki hapa Tanzania.

Analalamika juu ya kutokuwa na katiba inayokidhi mahitaji ya watanzania. Hivyo anataka Tanzania wapate katiba mpya. Sasa akilalama akiwa Brusels ndio ujumbe utafika vizuri? No anatakiwa aje hapa bongo.

Analalamika juu ya utawala usiofuata sheria na kubambikia watu kesi. Mfano anadai kuwa Mbowe amebambikiwa tuhuma za ugaidi. Lissu aje Tanzania na awasaidie watu kama Mbowe ambao wanaoenewa. Maana msaada wake ni mahakamani.

Kwa ujumla Lissu ana malalamiko mengi ambayo kimsingi hawezi kuyafikisha akiwa Brusele anakula kuku kwa mrija huku anasikiliza rhumba la Kikongo.

N.B . Idugunde ni member wa Jf anayeishi Igunga akifanya kilimo cha Mpunga. Sio mwananchama wa chama chochote kile.
Wewe ni CCM lialia, tunaweza kuweka hapa post zako zaidi ya laki. Au unataka tuanze kuzibandika?
 
Back
Top Bottom