Kenani Kihongosi awa Katibu Mkuu UVCCM
Sijaelewa, yani Mkuu wa Wilaya ameteuliwa kwenda kurithi nafasi iliyoachwa wazi na alieenda kuwa Mkuu wa Wilaya, kweli CCM imeishiwa viongozi.
 
Mmmhh hivi hizi kunguni wanaosaga CDM na genge lake siku hizi mbona kama hazina madhara?
Mbona kama chura kapigwa teke kwenda mbele?

Bado tunaitaka katiba ya wananchi KWA maslahi ya wananchi,Tumechoka ngonjera za CCM na CHADEMA utafikiri mtu na mke mwenza!
 
Sifa ya kuchagua katibu mkuu wa jumuiya kama UVCCM ni ipi?
Mhamasishaji wa mpiga siasa za propaganda mzuri au vip, hii inajumuisha na vyama vingine vya siasa Tanzaniania.

Nadhani, taasisi ya UVCCM mtendaji wao mkuu (Katibu) anatakiwa awe ni mtu mwenye akili sio tu ya propaganda, ila awe na creative na innovative brain ili kushirikiana na serikali kutengeneza fursa hasa ajira kwa vijana wakiwamo kutoka CCM.

Tanzania imezungukwa na nchi 8 (Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Congo, Zambia, Malawi na Mozambique); Barahi ya hindi kuna visiwa kama Seychelles, Madagascar, Comoro na Mauritius.

Kwa competitive advantage ya Tanzania inaweza kuuza ni kwenye soko la hizi nchi ambacho kikizalishwa Tanzania kinalifikia soko na tunavutia forex kuja Tz wakati huo vijana wanalio kwenye mchakato wa hilo suluhisho wakiwa na ajira.

Israel is a tiny country, wao competitive advantage yao imekuwa kuuza solutions za diverse sector ikiwamo kilimo, cyber; Sasa Tanzania hata korosho tunayozalisha, UVCCM katibu alitakuwa kuwa creative dept, sio vibaya vijana waka-own industries, hata za kuzalisha mafuta ya kula kwa kutumia corn harvest na kuuza GCC soko ambalo lina fedha na purchasing power ya kununua top quality products ikiwamo corn cooking oil.

UVCCM enzi za Mwl. Nyerere iliwekeza kwenye real estate, ndio maana wana majengo na wamepangisha.

CCM ya leo Mkiti akiwa Mhe. Samia ambae kajinasibu kufungua nchi, wao wanawaza nini kwenye kutengeneza solutions za ndani na nje ya Tanzania ili kutengeneza "mchuzi"?

Nadhani yule kijana alieteuliwa kushughulikia uchumi kwa kuwa ana jina kubwa, sio right choice kwao; ana fedha na amepata tenda kubwa kuuza jezi za simba, ila kwa UVCCM, wanatakiwa kuwa na brains to solve a lot of problems around and increase value of diverse goods and services which will inturn create wealth. Ila najua kwa kuwa tunapenda sana hiena hiena na propaganda imeonekana ndio mpango mzima, huyu nae anaweza akawa hana tofauti na yule alietoka.

Kila la heri UVCCM na katibu mpya wa sasa.

Amani iwe kwenu.
F
 
Ni Wazi sasa hawa Vijana wamechoka. Kenani Kihongosi DC wa Iramba ateuliwa kuwa Katibu Mkuu UVCCM. Yule Msanii aliyekua Arusha wananchi wakamlalamikia

====

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Kenani Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) akichukua nafasi ya Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro
View attachment 1826673
Ndio tayari kishafichwa , mara zote UVCCM anayesikika ni Mwenyekiti tu
 
Jamani huyu sindo yule alikuwa wa Arusha kumbe Jana alikuwa Singida anaapa kuwa atawatumikiwa watu wa Iramba Leo Tena inabidi akiache kiapo Cha Jana aende Dodoma tena aanze kazi mpya aisee hii nchi tamu sana.
 
Kwaiyo uko UVCCM vijana wakushika hiyo nafasi wameisha mpaka wampe kihongosi tena hiyo nafasi wakati tayali ni DC
 
Ni Wazi sasa hawa Vijana wamechoka. Kenani Kihongosi DC wa Iramba ateuliwa kuwa Katibu Mkuu UVCCM. Yule Msanii aliyekua Arusha wananchi wakamlalamikia.

====

Chama cha Mapinduzi (CCM) kimemteua Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Kenani Kihongosi kuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) akichukua nafasi ya Raymond Mwangwala ambaye ameteuliwa kuwa Mkuu wa wilaya ya Ngorongoro.

Isimamie vyema ccm Kenani, achana na lopo lopo wachadema, maana kwasasa jambo wanalo weza ni kubweka kama Mbwa
 
Kwaiyo uko UVCCM vijana wakushika hiyo nafasi wameisha mpaka wampe kihongosi tena hiyo nafasi wakati tayali ni DC
Ajabu iko wapi Mbona ata Mbowe alipokuwa Mbunge bado alibaki kuwa mwenyekiti wa chadema, halafu akaongezewa cheo kingine kiongozi mkuu wa kambi rasmi ya upinzani, kwahiyo ebu tulia
 
Back
Top Bottom