Kenani Kihongosi awa Katibu Mkuu UVCCM
Huyu aliwacharaza viboko......wafanyabiashara Arusha
 
Habari wanabodi,
Kutoka hapa dodoma kunakoendelea na Mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Mhe SAMIA HASSAN SULUHU na kamati kuu tayari wameshatoa jina la katibu huyu wa UVCCM.

Kwa wasiomjua Mhe Kenan huu ni wasifu wake mfupi

1.Amekua mkuu wa wilaya ya Iramba .
2 mkimbiza Mwenge wa kitaifa mwaka 2019.
3.Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa mwaka 2017.
4.Katibu wa TAHLISO mwaka 2014/15.


Please Mods msifute huu uzi.
20210622_175019.jpg
View attachment 1826750
 
Shaka na Kihongosi ni vijana wa CCM ambao kwa kiasi fulani wana historia za kusikitisha kwenye maisha yao ya siasa.

Ndg. Shaka kipindi akiwa Kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM, ni moja ya waliosimamishwa kazi baada ya kamati ya kuchunguza ubadhirifu wa mali za chama iliyoongozwa na Ndg. Dkt Bashiru kumtaja na bahati ikaangukia kwake akapewa Ukatibu wa CCM Mkoa wa Morogoro. Huko nako tuliona kwenye ziara ya Hayati Rais John Magufuli Alhamis Februari 11,2021akizindua soko kuu la Morogoro akimsimamisha kazi kwa tuhuma za Rushwa, nikinukuu maneno ya Hayati Rais Magufuli “Hukutakiwa kuwa meya aliyetakiwa sikumrudisha kuwa meya na bahati mbaya hata utafutaji wa meya hapa ulikuwa umejaa rushwa na ndio maana Katibu wa CCM wa hapa tumemsimamisha kazi atajadiliwa kwa sababu alikula rushwa kwa madiwani,”.

Kila sehemu kijana huyu anapokuwepo rushwa inanuka iwe kwa kashfa au kiukweli. sidhani Rais wa nchi anaweza kumshambulia mwananci wake hadharani kwa shutuma kama hizo.

Kihongosi ambaye leo amependekezwa kuwa katibu mkuu wa UVCCM ni moja ya watu wenye skendo kibao ambazo zinaumiza na kuhuzunisha. Ni moja ya watu waliosema waziwazi juu kifo cha binadamu mwenzake kisa tofauti zao kisiasa na kimtazamo, kitendo hicho ni kinyume kabisa na azimio ya umoja la mataifa la haki za kuishi na kulindwa.

Nikinukuu moja ya kauli zake aliwahi kusema "wapinzani wanaoichafua Serikali wanapaswa kukosolewa au Kuuawa kabisa", ni maneno aliyosema akiwa Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Iringa.

Kauli na matendo hayo yanahimiza chuki na ina dalili zote za kukosa busara. Je, tunapompa vijana madaraka makubwa, si tutatengeneza uongozi usiowajibika?

UVCCM ni idara inayoelea, zalisha na kuinua vijana kwenye ndoto zao za kuwa viongozi wakubwa, hivyo haina budi kuongozwa na watu wenye hekima, uwezo mkubwa wa kufikiri na busara ya kunena na kutenda. Vijana wenye sifa hizo wapo wengi
 
Habari wanabodi,
Kutoka hapa dodoma kunakoendelea na Mkutano mkuu wa Halmashauri kuu ya CCM.
Mwenyekiti wa CCM na Rais wa JMT Mhe SAMIA HASSAN SULUHU na kamati kuu tayari wameshatoa jina la katibu huyu wa UVCCM.

Kwa wasiomjua Mhe Kenan huu ni wasifu wake mfupi

1.Amekua mkuu wa wilaya ya Iramba .
2 mkimbiza Mwenge wa kitaifa mwaka 2019.
3.Mwenyekiti wa UVCCM mkoa wa Iringa mwaka 2017.
4.Katibu wa TAHLISO mwaka 2014/15.


Please Mods msifute huu uzi.View attachment 1826751View attachment 1826750
Wakuu naomba kuuliza, Ina maana ile nafasi ya uDC anakuwa ameacha so ndio?
 
Na huyu KHERI SINDANO THUMU si DC ubungo
 
Kuna mradi hapa wa thamani ya tril 69.5

Kuna project ya ujenzi wa SRG fela-Isaka thamani ya mradi ni USD 1.2bn (2.7 Tril)

Hapo namna gani kunakuwa na local content; kuna uwezekano vijana wakawa hawana fedha mkononi au dhamani za kuwafanya wakopesheke; ni namna gani UVCCM au wizara ya kazi na vijana waka-develop financial instruments ili vijana wakopesheke say equipment ili kwenye mnyororo wa thamani kuwa na kampuni owned na vijana kuuza
kokoto
maji
moram
kukodisha magari
catering services
housing services ile mradi unaisha, kupitia financial instrument zilizowekwa na kwa kuwa soko lipo kununua bidhaa au huduma za ujenzi, mikopo inalipika na kwa fedha nyingi kubaki ndani tax base inapanuka pia.
Mambo kama haya nilitegemea hata waziri wa fedha ambae katoke UVCCM na kawahi kuwa mweka hazina wa CCM, yeye anawezaje kuifanya hazina ika-offer financial instruments ili Watanzania wawe sehemu ya USD 1.2bn project ambayo isha-take off?

Tanzania kuna namna akili zetu sijui tumepeleka wapi kwenye kujenga projects/investments financial leverage ili kupanua tax base na kuhakikisha fedha nyingi ya miradi hususan ujenzi inabaki ndani kadri iwezekanavyo.
 
Muulize katiba ni nini? Akikujibu bila kùuliza itakuwa miujiza
 
Hapo sijaipata. Mkuu wa Mkoa wa Arusha ni nani kwani? Aliyekuwa anawapiga bakora wafanya biashara walioiba viti vya shule?
Kwa màana hiyohuyu kwanza alikuwa Arusha,ambako alichapa watu viboko kikatili,Good God,na sasa amekuwa Katibu Mkúu wa UVCCM?
Aisee! I have no comment.!
 
Back
Top Bottom