Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

Mohamed Said

JF-Expert Member
Joined
Nov 2, 2008
Posts
21,967
Reaction score
32,074
KENYA ABDALLAH HASSAN KATIBU MKUU WA KWANZA MUISLAM WIZARA YA ELIMU AMEFARIKI

Kenya Abdallah Hassan nimemfahamu toka utoto wangu Moshi katika miaka ya 1960.

Siku hizo mimi nikiwa shule ya msingi madarasa ya chini sana yeye alikuwa Mawenzi Secondary School.

Kenya alikwenda Makerere, Uganda nilikuja kujua baadae.

Kenya angefariki na mimi wala nisingenyanyua kalamu yangu kuandika chochote kuhusu yeye kama isingetokea mwaka wa 1987 jambo lililogusa Waislam wengi Tanzania.

Mwaka huo Prof. Kighoma Malima alichaguliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Elimu.

Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Ilikuwa kama vile Rais Mwinyi amevunja mwiko alioweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka uhuru mwaka wa 1961kuwa nafasi hiyo haishikwi na Muislam.

Baada ya kuwa Waziri wa Elimu Prof. Malima Rais Mwinyi akamchagua Kenya Abdallah Hassan kuwa Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

Rais alikuwa kapiga msumari wa moto juu ya kidonda.

Wizara ilichafuka na wahariri wa magazeti wakawa wanachonga penseli zao ziandike vizuri.

Kuna watendaji ndani ya wizara waliona kama vile sasa bwawa limeingia luba itakuwa tabu kuogelea kwa raha na salama.

Yaliyotokea sasa ni historia.

Prof. Malima aliondolewa kwenye Wizara ya Elimu baada ya kujadiliwa Dodoma.

Hayo ndiyo yaliyofanya mimi hii leo nimkumbuke kaka yangu Kenya Hassan.

Mola amghufirie dhambi zake na amlipe Pepo ya Firdaus.

Amin.

Screenshot_20210326-180739_Facebook.jpg
 
Asee nakukubali sana mzee wangu unaupeo mkubwa sana ila bahati mbaya umeamua kutumia upeo wako mkubwa kusambaza propaganda za kuwagawa binadamu kwa misingi ya udini.
 
Ujoka,

Katika Wakurugenzi watano Wizara ya Elimu wote watano walikuwa Wakristo.

Una fikra gani katika mgawanyo huu?
Halafu mkuu wakati huo kwani Karibu Mkuu wa wizara alikua anateuliwa na Waziri sio Rais mwenyewe?

Nadhani hiyo ilikua ni Presidential appointment kwa wote wawili (Malima & Kenya)

Nyakati ukuta kwakweli
 
Daah, ila wewe mkuu!
Lupweko,
Hii hapo chini kanitumia msomaji mmoja:

"Nakumbuka Prof. Ndalichako alipokuwa Mkurugenzi wa Elimu kuna skuli moja ya Kiislamu walifelishwa skuli nzima.

Baada ya Waislam kufuatilia ndio Wizara ikaomba radhi na kusema kuna makosa ya bahati mbaya.

Sitasahau kadhia hiyo na zawadi ya Prof. ikawa ni kuwa, "Promoted to a full ministerial post. Minister of education to date."
 
Lupweko,
Hii hapo chini kanitumia msomaji mmoja:

"Nakumbuka Prof. Ndalichako alipokuwa Mkurugenzi wa Elimu kuna skuli moja ya Kiislamu walifelishwa skuli nzima.
Baada ya Waislam kufuatilia ndio Wizara ikaomba radhi na kusema kuna makosa ya bahati mbaya.
Sitasahau kadhia hiyo na zawadi ya Prof. ikawa ni kuwa, "Promoted to a full ministerial post. Minister of education to date."
Labda ngoja nifanye kushare experience yangu ya makosa kama hayo. Kuna mwaka fulani darasa letu watu wote wenye majina yaliyoanzia herufi M hadi Z katika somo moja tuliwekewa alama 'F', yaani zilifuatana kama zote kiasi kwamba hata ile pattern kwa macho tu mtu akiiona anaingia wasiwasi, maana lilikuwa somo rahisi ambalo waliokuwa na majina ya herufi A hadi L walikuwa wanapata alama 'A' na 'B'.

Shule iliripoti tatizo NECTA, na ndani ya mwezi tukapewa matokeo halisi. Ni tatizo la teknolojia ndogo wakati huo walikuwa wanatumia Excel (ambayo kwangu mimi najua inahitaji umakini sana), kwa hiyo aliyekuwa anaingiza marks huenda alidrag marks au formula ya ajabu ikaapply kote. Hiyo shule ilikuwa ni ya serikali, wala sio ya private wala ya kidini.

Kwa hiyo hata hilo la waisilamu, naamini haikuwa hujuma, ni makosa ya kuingiza data/formula au kutumia applications zisizo powerful au ambazo zipo delicate kama excel
 
Lupwelo,
Hilo kweli linawezekana wala hakuna wasiwasi.

Naingia Maktaba nikuwekee jambo lingine.

''Lakini tuende kielimu. Ninayo ripoti ya mwaka huu. Waliofanya mtihani wa darasa la saba kuingia darasa la tisa, asilimia 71 Waislamu. Asilimia 29 ni wengine.

Walioshinda katika wale asilimia 71 ni asilimia 21. Katika wale 29 walioshinda tena sema mwenyewe.

Katika asilimia 29 waliokwenda shuleni ni asilimia 79.
asilimia 71 waliokwenda darasa la tisa ni asilimia 21.

Sasa kuna moja, ama Waislamu wajinga ama akili yao haifanyi kazi, ama mtu ukiwa Muislamu wewe huna kitu, ama kuna kitu.

Sasa namwomba Waziri anayehusika, anaposema aseme ya kwamba kwa hali ilivyo Waislamu wameumbwa wajinga.

Au kwa hali ilivyo kuna sababu kadha, kadha.

Mwalimu Nyerere alisema zamani ifanywe bidii ya kuwanyanyua waliokuwa chini.

Sasa bidii hii siyo ya kuwanyanyua waliokuwa chini. Bidii hii ni ya kuwakandamiza waliokuwa chini.''

(Mh. Kitwana Kondo Bungeni, Dodoma1999)
 
Ulipoingiza udini katika uzi wako ukaharibu kila kitu.
Sam,
Udini ni kule kueleza kuwa walikuwapo watu katika watendaji wa Wizara ambao hawakupendezewa na kuwa na Waziri na Katibu Mkuu Waislam?

Tafadhali nifahamishe.
 
Halafu mkuu wakati huo kwani Karibu Mkuu wa wizara alikua anateuliwa na Waziri sio Rais mwenyewe??

Nadhani hiyo ilikua ni Presidential appointment kwa wote wawili (Malima & Kenya)

Nyakati ukuta kwakweli
Geo...
Ahsante sana.
 
Apumzike kwa Amani. Aliwahi pia kuwako Wizara ya Mambo ya Nje? Siku zimepita nyingi.
 
Lupweko,
Hii hapo chini kanitumia msomaji mmoja:

"Nakumbuka Prof. Ndalichako alipokuwa Mkurugenzi wa Elimu kuna skuli moja ya Kiislamu walifelishwa skuli nzima.

Baada ya Waislam kufuatilia ndio Wizara ikaomba radhi na kusema kuna makosa ya bahati mbaya.

Sitasahau kadhia hiyo na zawadi ya Prof. ikawa ni kuwa, "Promoted to a full ministerial post. Minister of education to date."
Mzee una nadharia zisizo na msingi. why unapenda kuhusisha dini katika kila masuala. Yani inaonekana ulimchukia sana Mzee Nyerere maana huishi shutuma kwake dhidi ya udini. Hivi mzee angekuwa kama unavoshutumu hapo nchi ingekuwa hivi hii kweli? waislam na wakristo wanaishi kwa amani kabisa pamoja, regardles ya dini.
 
Back
Top Bottom