Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

Kenya Abdallah Hassan, Katibu Mkuu wa kwanza Muislam Wizara ya Elimu, amefariki

KENYA ABDALLAH HASSAN KATIBU MKUU WA KWANZA MUISLAM WIZARA YA ELIMU AMEFARIKI

Kenya Abdallah Hassan nimemfahamu toka utoto wangu Moshi katika miaka ya 1960.

Siku hizo mimi nikiwa shule ya msingi madarasa ya chini sana yeye alikuwa Mawenzi Secondary School.

Kenya alikwenda Makerere, Uganda nilikuja kujua baadae.

Kenya angefariki na mimi wala nisingenyanyua kalamu yangu kuandika chochote kuhusu yeye kama isingetokea mwaka wa 1987 jambo lililogusa Waislam wengi Tanzania.

Mwaka huo Prof. Kighoma Malima alichaguliwa na Rais Ali Hassan Mwinyi kuwa Waziri wa Elimu.

Hili lilikuwa halijapata kutokea.

Ilikuwa kama vile Rais Mwinyi amevunja mwiko alioweka Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere toka uhuru mwaka wa 1961kuwa nafasi hiyo haishikwi na Muislam.

Baada ya kuwa Waziri wa Elimu Prof. Malima Rais Mwinyi akamchagua Kenya Abdallah Hassan kuwa Katibu Mkuu katika Wizara hiyo.

Rais alikuwa kapiga msumari wa moto juu ya kidonda.

Wizara ilichafuka na wahariri wa magazeti wakawa wanachonga penseli zao ziandike vizuri.

Kuna watendaji ndani ya wizara waliona kama vile sasa bwawa limeingia luba itakuwa tabu kuogelea kwa raha na salama.

Yaliyotokea sasa ni historia.

Prof. Malima aliondolewa kwenye Wizara ya Elimu baada ya kujadiliwa Dodoma.

Hayo ndiyo yaliyofanya mimi hii leo nimkumbuke kaka yangu Kenya Hassan.

Mola amghufirie dhambi zake na amlipe Pepo ya Firdaus.

Amin.

View attachment 1735030
Hakika umejaa Historia!.
Kongole kwako ndugu!
 
wewe ni nyoka mwenye sumu mbaya ya udini
TT,
Ungejibu inakuwaje Wizara ya Elimu yote imeshikwa na waumini wa dini moja ungekuwa umefanya jambo zuri.

Tuliza ubongo wako na uwaze ingekuwaje Wizara ya Elimu iwe chini ya watendaji Waislam watupu na vijana wa Kikristo wanazuiliwa kupata elimu ya juu?

Kutoa matusi maana yake ni kuwa umeelemewa na huu ukweli ninaouweka hapa.

Nadhani umeshatambua kuwa ukumbi umetulia mimi ndiye sasa nimeshika kitabu nasomesha na mnanisikiliza.

Hamjapata kabla kusikia haya.
Kuna mtu kaniambia mimi mchochezi.

Nikamwekea historia ya Ally Sykes alivyokuwa akisakwa na Special Branch kwa uchochezi.

Ally Sykes ni kati ya waasisi 17 wa TANU na mmoja wa wafadhili wa chama na kadi yake ya TANU ni no. 2 na yeye ndiye aliyempa Nyerere kadi no.1 na kaka yake Abdulwahid kadi no. 3.

Kubwa yeye ndiye aliyesanifu hizo kadi na akanunua kadi 1000 za kwanza kutoka mfukoni kwake.

Mchochezi inategemea umesima upande upi.
Upande wa haki au upande wa dhulma.

Yuko aliyesema mimi siandiki taazia ila aliyefariki awe Muislam.
Nimeweka taazia ya Jim Mdoe na ya Arthur Mambeta.

Yuko aliyeniingiza kwa magaidi nimeweka muhadhara niliotoa University of Ibadan kuhusu ugaidi.

Hawa wote hawajakuwa hata na uungwana wa kurejea hapa na kunishukuru.
Sisemi wanitake radhi waseme kuwa wamenizulia uongo.

Wewe umenitukana.
Mimi sirejeshi matusi ukinitukana unakuwa umenidhihirishia kuwa nimeshinda.

Mwalimu wangu aliyenisomesha elimu ya mnakasha yaani majadiliano marehemu Sheikh Haruna amenifunza kutokughadhibika na kutoogopa kusema kweli.
 
Hakika umejaa Historia!.
Kongole kwako ndugu!
Ngoni...
Ahsante sana ndugu yangu.

Mimi nimeyajua haya kwa kuwa walioasisi harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika na kuunda TANU ni babu zangu na kijiti kikapokelewa na baba na shangazi zangu.

Elimu hii sikupata ati kwa kusoma.
 
Ngoni...
Mimi nimeyajua haya kwa kuwa walioasisi harakati za kupigania uhuru wa Tanganyika ni babu zangu na kijiti kikapokelewa na baba na shangazi zangu.

Elimu hii sikupata ati kwa kusoma.
Shukran!.
 
Philipo mpango, makamu wa raisi mkuu
BlackPanther,
Mwenyezi Mungu amuongoze afanye kazi yake kwa uadilifu nchi ineemeka kutokana na elimu na ujuzi wake.

Black Panther hili jina umenikumbusha maisha yangu ya udogoni niko St. Joseph's Convent School hapa Dar es Salaam.

Miaka ile tukiwausudu sana Wamarekani na ilikuwa sisi ni watu wa kusoma magazeti ya Kimarekani Time na Newsweek, Ebony nk.

Wamarekani ni hodari sana kwa propaganda na wanajua kukamata bongo za vijana.

Sisi ilikuwa watu wa kusikiliza Soul Music - Wilson Picket, James Brown, Areth Franklin kwa kuwataja wachache.

Zile zilikuwa nyakati za wazimu khasa.

Tukiwausudu sana akina Huey Newton na Stokley Carmichael.
Na mengine mengi.

Umenigusa kidogo nilipoona umetumia hili jina.
 
Allah amrehemu mzee we2, na waislamu wote kwa ujumla.



Sheikh Mohamed Said shukran jaziilan, Allah akujaalie umri mrefu wenye kheri na wewe.
Dalmine,
Amin kwa sote na Allah ajaalie viongozi wetu wajue kuwa tunajemga fitna kubwa kwa hii hali ambayo siku moja tutakuja kujuta.

Allah awajaalie viongozi na wauone huu ukweli na wafanye marekebisho kwani dhulma inaangamiza.
 
Dalmine,
Amin kwa sote na Allah ajaalie viongozi wetu wajue kuwa tunajemga fitna kubwa kwa hii hali ambayo siku moja tutakuja kujuta.

Allah awajaalie viongozi na wauone huu ukweli na wafanye marekebisho kwani dhulma inaangamiza.

Ameen yaarabbil'alamiin sheikh wangu
 
Back
Top Bottom