Kenya wakimaliza kuvurumishana, wataikuta Tanzania imerusha satellite yake anga za juu

Kenya wakimaliza kuvurumishana, wataikuta Tanzania imerusha satellite yake anga za juu

Unapigana na Rais wako aliyerudisha wilaya ya ngorongoro na viji vyake?
Subiri uchaguzi upite, utaona kama unachosema kina maana yoyote. Ardhi ya Kenya imeuzwa yote kwa wageni na watu binafsi, hivyo Ngorongoro imejaa watu kutoka Kenya wanaowinda na kuchungia pale. Mbuga ya Ngorongoro inakufa na kupoteza maana yake kwakuwa binadamu wameongezeka idadi na wamasai wa sasa hivi sio kama wale waliohamishiwa pale kutoka Serengeti. Wamasai wa sasa wanavaa nguo, wanajenga nyumba za matofali na bati juu, wanakula ugali na ubwabwa, wananunua pikipiki na magari na wanaua wanyamapori kupata mbembe na ngozi, wanakwenda shule, wanahitaji zahanati, nk. Lazima wahame kutoka pale kupisha wanyama na utalii..
 
Wakenya hawajamjua mchawi wao, wacha watifuane kwa kisingizio cha demokrasia. Wana Katiba ambayo kila mtu anagoma aongezwe mshahara, watu 100 wanaweza kushikilia 80% ya ardhi yote yenye rutuba, watu 50 wanaweza kumiliki 70% ya rasilimali zote za nchi. Not yet Uhuru. Marekani imemwamuru Ruto apeleke askari polisi Haiti hata kama hapendi kufanya hivyo, hata kama katiba ya Kenya inakataza kufanya hivyo; NOT YET UHURU.
Huwezi kuilinganisha Kenya huku kamjambeni kila mtu chawa
 
Demokrasia itawachelewesha sana Kenya, hawana uchumi unaohimili demokrasia ya mangaribi. Wanataka kumuondoa MAKAMU wao wa RAIS kihuni TU.

Kuna wezi wengi sana Kenya wanakula mali ya umma bila kuchukuliwa hatua kali kama hizi, why Gashagua?

Watutukuta tz tuko siti za mbele sana kimaendeleo.

Soma Pia: Yanayojiri Bungeni Kenya: Wabunge 281 wapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua
Nchi ya kenya ni ya kuigwa kwa mambo mengi ya kisiasa.
Lazima kuwepo mahali pa kuanzia katika dhana nzima ya kuwajibishana.
Tunachotakiwa kujadili ni je,anayotuhumiwa kayafanya au ni uongo?
Kama ni uongo,Mungu atamfanikisha kwa kufanya shughuli nyingine nje ya siasa.
kama kayafanya lazima awajibishwe bila kujali huko nyuma walifanya nini na wako wapi.

Kuanzia kwake kila mtu atakuwa makini,akilitafuta atalipata.
Nawapongeza wakenya kwa hatua kubwa ya demokrasia.
 
Hapa naungana na wewe 100%. Afrika haihitaji demokrasia ya Magharibi bali inahitaji njia ya kuwaondoa na kuwaadhibu mara moja hadharani kila mtu na watu wote wanaokula mali ya umma na kuwateka na kuwaadhibu hapohapo hadharani watu wote wanaoungana na wageni kuziibia nchi zao. China kwamfano, hawana demokrasia ya magharibi lakini wanao mfumo unaowakamata na kuwaadhibu vikali watu wote wanaokula keki ya umma au wanaoungana na wageni kuihujumu China.
 
Ikitokea hivyo wenyewe watazirai kwa mshangao.
Magufuli alikuwa anaelekea huko, lakini hata mama Samia hayuko mbali na direction hiyo. Nimefika Dar es Salaam mwezi August nikakuta mji mzima vumbi linatimka kwa ujenzi wa barabara za kisasa kabisa. Nikakuta siku hizi kutoka DSM-Dodoma ni masaa 3 tu. Kilimo kimewekewa mkakati unaoeleweka na kuelezeka, nishati ya kupikia imewekewa msukumo wa maana, usambazaji wa maji unarindima kila kona ya tz. Satellite ya kwanza tz haiko mbali. Rais mwanamke pekee Afrika hawezi kufanya upuuzi utakaowakatisha tamaa wanawake wenzake Afrika. Nimekaa paleee. Mabeberu kupitia akina Lissu walijaribu kutaka kuingiza mkono wao mchafu kwenye plan zake kupitia kutekwa kwa mzee Kibao (RIP), akawapa kalipio kali sana la kikakamavu haraka sana mbele ya camera.

Speed yetu inawaogopesha, Mama ana uwezo, fedha na jeuri ya kutoa ndege kwa timu ya taifa kupeleka wachezaji kucheza mechi zao kokote wanakokwenda. Unataka nini wewe?
 
Speed yetu inawaogopesha, Mama ana uwezo, fedha na jeuri ya kutoa ndege kwa timu ya taifa kupeleka wachezaji kucheza mechi zao kokote wanakokwenda. Unataka nini wewe?
Yote hayo ni sawa,lakini bila katiba mpya hata vumbi lingetimka mpaka chumbani tunakolala,
akija mtu ataviuza vilivyojengwa na hutakuwa na la kumfanya,maana atatumia mamlaka yake kikatiba.
 
Yote hayo ni sawa,lakini bila katiba mpya hata vumbi lingetimka mpaka chumbani tunakolala,
akija mtu ataviuza vilivyojengwa na hutakuwa na la kumfanya,maana atatumia mamlaka yake kikatiba.
Bro mnaweza kuwa na katiba nzuri matata sana lakini kama mkipata kiongozi wa hovyo ni bure kabisa. Katiba yetu ni hii ni nzuri sana kama tukipata kiongozi mzuri saaaana mpenda maendeleo na watu wake lakini ni mbaya saaaana kama tutapata kiongozi wa hovyo lakini anaependwa au aliyewekwa na nchi za Magharibi. Kwahiyo Katiba nzuri au mbaya huwa hazifanyikazi Afrika katika kuwaletea maendeleo wananchi. Kwa kutumia katiba hiihii kuna viongozi walituibia sana na kuna viongozi walifanya kazi nzuri.
 
Bro mnaweza kuwa na katiba nzuri matata sana lakini kama mkipata kiongozi wa hovyo ni bure kabisa. Katiba yetu ni hii ni nzuri sana kama tukipata kiongozi mzuri saaaana mpenda maendeleo na watu wake lakini ni mbaya saaaana kama tutapata kiongozi wa hovyo lakini anaependwa au aliyewekwa na nchi za Magharibi. Kwahiyo Katiba nzuri au mbaya huwa hazifanyikazi Afrika katika kuwaletea maendeleo wananchi.
Unataka kuniambia toka tupate uhuru hatujawahi kupata kiongozi bora?
kama tumewahi kupata mbona hadi sasa watu nanachangia madimbwi na mifugo kupata maji ya kunywa
wakati nchi ina umri sawa na mstaafu.
 
kupata kiongozi bora bila mwongozo wa kumwongoza ili afikie malengo ni sawa na kutokuwa na kiongozi,
maana atawaongoza kufuatana na uelewa wake.
 
Kama tuna reli ya umeme na barabara za mabasi ya haraka kama nchi za magharibi tutashindwa nn kuwa na satellite yetu? Kenya wanavyo?
Ahsante sana mzalendo wa kweli! Wale wenye hadithi eti miaka 63 ya uhuru Tanzania hakuna maendeleo yoyote tuendelee kuwapuuza!
 
Mkuu no 4 s pw SIJUI LINI TUTA ANDAMANA NCHI NZIMA mbowe alijikuta yupo peke na wale waandish wa habari sasa et mwenyekit vp mbona upo peke ako ha ha ha ha a
Vitu vilivyojaa kwenye vichwa vya wa Tz
1. Diamond ana mahusiano na mwanamke gani
2. Kucomment umbea kwenye page za mange kimambi hadi mtoto wakiume aandika "Da mange"
3. Kumuita Maulidi kitenge ni usalama wa Taifa kisa anaweka Airpods maskioni.
4. Kuhamasishana maandamano kila mtu anasema yuko tayari kufa ila siku ya maandamano hatokei hata mmoja.
5. Kuwaza ngono 2MMkuu
 
Kupata kichekesho kingine kama hchi nibonyeze ngapi ?
 
Unataka kuniambia toka tupate uhuru hatujawahi kupata kiongozi bora?
kama tumewahi kupata mbona hadi sasa watu nanachangia madimbwi na mifugo kupata maji ya kunywa
wakati nchi ina umri sawa na mstaafu.
Hiyo hali iko karibu nchi zote za Afrika kusini mwa jangwa la sahara. Hii ina maana kuwa tatizo haliko ndani ya Afrika na waafrika wenyewe, bali kuna factor/mfumo ambayo imetengenezwa kuzifanya nchi zote za Afrika zifanane kimaendeleo. Huwezi kusema viongozi wa Afrika woooooote ni wapumbavu hawapendi maendeleo ya nchi na watu wao. Wakoloni wanatudhoofisha kwa njia mbalimbali zinazohakikisha kuwa rasilimali zetu hazitunufaishi. Wanafanya hivyo kwa kuhodhi masoko ya bidhaa, technologia, mitaji na kutuchagulia viongozi wetu wenye kuwahakikishia maslahi yao (vibaraka/mapandikizi). Wanahikisha kuwa viongozi wenye maono na akili sana kama mimi hawapati nafasi na wakipata nafasi watapinduliwa au kuuawa.
 
Mkuu no 4 s pw SIJUI LINI TUTA ANDAMANA NCHI NZIMA mbowe alijikuta yupo peke na wale waandish wa habari sasa et mwenyekit vp mbona upo peke ako ha ha ha ha a
Vyama vya upinzani na wananchi ni kama maji na mafuta kama wakiwekwa sehemu moja. Wapinzani hawana hoja mbadala zinazowakuna wananchi, na hata pale wanapopata nafasi kama ubunge au udiwani wanajikumbuka wao wenyewe na familia zao, maisha yao yanabadilika ghafla badala ya kutumia kila senti wanayoipata kuimarisha vyama na kutatua kero za wananchi wao japo kwa uchache. Utawakuta na wao wanasomesha watoto na wajukuu wao international schools, wanasomesha watoto wao nje ya nchi, wanajenga majumba makubwa na mahoteli, wanatembelea magari makubwa, nk. Na wengine wanarudi CCM tena kwenda kuunga juhudi. Hawana sera vutivu, wanadandia matukio tu kama fisi anaevizia binadamu auangushe mkono wake auokote.
 
mh! kenya wamesharusha mbona!
Kama Gashagua anaondoka basi wa kwanza kuondoka anapaswa kuwa Ruto aliyepiga U turn kutoka mkate mzima kwenda nusu mkate bila kushirikisha wapiga kura wake. Alijitafutia comfort zone kwa kuungana na Raila kuunda serikali.
 
Demokrasia itawachelewesha sana Kenya, hawana uchumi unaohimili demokrasia ya mangaribi. Wanataka kumuondoa MAKAMU wao wa RAIS kihuni TU.

Kuna wezi wengi sana Kenya wanakula mali ya umma bila kuchukuliwa hatua kali kama hizi, why Gashagua?

Rais Ruto aliwaahidi wapiga kura wake kuwa hakutakuwa na serikali ya "nusu mkate" lakini sasa wana serikali ya "robo mkate" (Ruto, Gashagua, Raila, na nchi za magaribi). Aliwashirikisha wapiga kura wake?

Watutukuta tz tuko siti za mbele sana kimaendeleo.

Soma Pia: Yanayojiri Bungeni Kenya: Wabunge 281 wapiga kura ya kumuondoa madarakani Gachagua
Una uhakika na unaloongea?
 
Vitu vilivyojaa kwenye vichwa vya wa Tz
1. Diamond ana mahusiano na mwanamke gani
2. Kucomment umbea kwenye page za mange kimambi hadi mtoto wakiume aandika "Da mange"
3. Kumuita Maulidi kitenge ni usalama wa Taifa kisa anaweka Airpods maskioni.
4. Kuhamasishana maandamano kila mtu anasema yuko tayari kufa ila siku ya maandamano hatokei hata mmoja.
5. Kuwaza ngono 24/7
Ongezea simba na yanga
 
Back
Top Bottom