Zawadi Ngoda
JF-Expert Member
- Aug 13, 2009
- 4,175
- 2,294
Acheni fitina na uoga. Si siri vision ya TZ ni kuita wawekezaji nchini toka nchi za Afrika na nje ya Afrika ili kuongeza mzunguko wa pesa. Kila muwekezaji ni fursa kwa Tanzania na wananchi wake. Iwe kutoka S. Afrika au Moroko au Kenya ni sawa tu.TANZANIA YAJISALIMISHA TENA MIKONONI MWA KENYA
Kwa miaka takribani mitano Tanzania imekuwa "mwana mpotevu" baada ya Hayati Rais Magufuli kustukia "faulo" za kibiashara yaani biashara zisizokuwa na mizania sawa baina ya majirani hawa wawili. Ikumbukwe kuwa Kenya ndilo taifa la kiafrika linaloongoza kwa uwekezaji nchini Tanzania. Kwa lugha nyingine, Tanzania imekuwa "koloni mamboleo" la Kenya kwa miongo kadhaa.
Hayati Rais Magufuli hakutaka Tanzania iendelee na utumwa, akaratibu mipango ya kuinasua Tanzania kutoka kwa "mkoloni mweusi". Hatua hii ya Magufuli iliikera sana Kenya na tangu hapo uhusiano wa kibiashara ukayumba.
Ikumbukwe pia kuwa Kenya ni kitovu kikubwa cha mabeberu katika ukanda wa Afrika Mashariki. Makampuni mengi ya Kenya ambayo yamewekeza hapa nchini hayamilikiwi na wakenya ama yanamilikiwa na wakenya wenye asili ya kizungu (walowezi).
Kenya ambayo ilishirikiana na mabeberu wa Israel kufanikisha "Operesheni Entebbe" mwaka 1976 haiwezi kuwa mshirika wa kuaminiwa na mwenye uchungu na mtu mweusi.
Tutarajie
👉 Kenya kuongoza tena katika mauzo ya madini ya Tanzanite.
👉 Watalii kurejea Kenya
👉 Mlima Kilimanjaro sasa kuwa rasmi mlima wa Kenya
👉 Hujuma katika Shirika letu la Ndege (ATCL) ili kuikuza tena Kenya Airways
👉 Hujuma katika mashirika yetu ya simu ili kuikuza Safaricom
👉 na kadhalika.
Suala muhimu siyo "KAZI IENDELEE" bali "KAZI GANI IENDELEE"!
Vijana wako mitaani, acha wawekezaji waje Madegree yanayosaga lami yapate ajira. Leo hii uwekezaji wa Kenya umewapatia ajira watanzania zaidi ya 50 elfu. Hivi hamlioni hilo!