Hahaa nimesoma hapo miaka mitano uchumi na takwimu ila huwa nawashangaa sana wanaoenda kuongeza elimu pale wahadhiri wengi ni washamba sana.
Ph.D ya miaka 3/4 watu wanasoma mpaka miaka 7/10. Pale shule kuanzia ngazi za juu ni kama wanakomoana hapafai hawezi kuvumilia ujinga.
Hii ni mentality fulani ya Kibongo, si UDSM tu.
UDSM inaweza kuwa kinara kwa sababu kuna ile hadhi ya chuo cha kwanza, watu wana Status Anxiety vibaya sana.
Mimi huwa naiita "Kafkaesque Kerfuffle". Kufuatia hadithi za Franz Kafka. Ukienda kwenye maofisi ni hivyo hivyo, yani unaweza kukutana na kajamaa kamlinzi tu ka mlangoni, lakini kanataka kukutesa bila sababu ya maana utambue kuwa upo eneo lake la kujidai.
Nilivyokuwa nasoma undergraduate (NYC, US) kuna profesa mmoja wa falsafa nilikuwa nabishana naye sana darasani. Philosophy elective. Kila kipindi ile back and forth ya kubishana ilikuwa kubwa sana darasani. Kubwa mpaka nikawa najiona kama nina dominate lile darasa. Mpaka siku moja dada mmoja akaniuliza, hivi unavyombishia yule Profesa, huwa unaamini kweli zile hoja, au unamfanyia show ya makusudi tu? Nikamwambia naamini kabisa.
Sasa, siku ya mtihani wa mwisho wa term, niko library nasoma ile ya mwishomwisho kabla ya mtihani, Profesa akanitumia email, anasema usije kwenye mtihani.
Nikasema mama yangu, Profesa ndiyo ananikata nisifanye mtihani kwa sababu ya ubishi wangu darasani? Ntakoma leo. Nikamuuliza kwanini?
Profesa akasema mabishano yako ya darasani yamekupasisha mtihani huu, yale mabishano si ya darasa hili la undergraduate, yale ni mabishano ya masters degree.
Nikamuuliza, sasa utanipa alama gani kwenye mtihani huu?
Akasema hakuna alama nyingine. Nitakupa A+ kwenye somo hili.
Huyo Profesa ni kila kitu tofauti na mimi. He was white, I am black, he was conservative, I was liberal, he was an old American judge, I was a young African immigrant.
Lakini, aliamini sana katika dhana ya Profesa na wanafunzi kubishana kifalsafa darasani. Yani pale nilipoona kama naharibu kubishana sana na Profesa, yeye, bila ya kunionesha wazi, alikuwa anafurahia sana kuona ana mwanafunzi anayejiamini, anayejibizana, anayeweza kuonesha kasoma mambo mengi na anaweza kuyatetea.
Hata baada ya kumaliza somo lile, alinitaka niwe naenda kwenye picnics zao anipe introductions kwenye networks zao, ila mimi nikawa nina mambo mengi tu.
Profesa yule alinifikirisha sana. Nikajiuliza, hivi hapa ningekuwa UDSM ningeweza kubishana na Profesa hivi, halafu anipe A+ kutokana na mabishano yangu ya darasani?
Thubuuutuuu.
Sasa hapo ndipo wanafunzi wanashindwa kujenga confidence, creativity, critical thinking skills.
Wanakwenda kikondoo kondoo wakiogopa ma Profesa tu.
Wanaogopa wakimbishia Profesa, atawashika shati awapige disco.
Wanasoma ili wapate cheti tu, si kuelewa mambo.