Kero ya kukuta mtu kakaa kwenye siti yako ya dirishani kwenye Bus.

Anza kwa kumuuliza "samahani seat yako ni namba ngapi?"

Akisema, mwambie yangu ni hii, hivyo umekaa kwenye seat yangu... Au hio sio namba ya seat yako, seat yako ni hii Akibisha muite konda wa gari.

Mbona issue zingine simple tu mzee..
 
Unamuita TU konda wa gari unamuomba akuoneshe siti Yako kama ilivyokwenye tiketi. Kondakta atakuja kumuelewesha kuwa hiyo sio sehemu yake . Kisha atamuonesha anapotakiwa kuketi. Haina haja ya kugombana na jirani Yako ktk safari na mtakua hapo pamoja Kwa muda mrefu,. Muachie hiyo kazi konda
 
Unamwambia tu mkuu.. au siku nyingine ukishaona.. kakaa unamuita konda akuonyeshe siti yako. Hapo unaepusha kelele.
 
namwambia tu Oya mwamba hiyo siti ni yangu, anabishaje sasa, akibisha aonyeshe tiketi yake mbona jambo jepesi sana, sema labda wanawake unawavungia hasa ukiona hana mtoto
 
Kama kumwambia mtu akupishe seat unashindwa, sasa utaweza kusimama na kutoa maelekezo siku ukiwa na familia kweli mkuu...☹️
 
Ya kwangu utanipisha, akili yangu naijua mwenyewe.
Nitakupa neno moja unaweza kushuka hata kwenye gari...ni kipawa tu😂
 
Mtu aliyekaa kwenye seat ambayo sio yake anakua amefanya makusudi,na hii ni kukosa ustaarabu na kukosa heshima kwa mwenye seat yake,

So,mtu wa hivyo usimuonee aibu hata siku moja,ukimuignore ndio itakua tabia yake,mchane wazi kabisa kua hiyo seat sio yake na anatakiwa akupishe,kisha acha stori nae mpaka mwisho wa safari coz huyo ni mpumbavu huna cha kuongea nae cha maana.
 
Huwezi amini mimi zamani nilikuaga kama wewe ila skuizi walaa tena napataga ya dirishani ila mtu akija namwambia kaa dirishani🤣 sijui nmekua! Yani miaka hata 6 /7 nmekua hivyo
 

Anza kwa kumuuliza "samahani seat yako ni namba ngapi?"

Akisema, mwambie yangu ni hii, hivyo umekaa kwenye seat yangu... Au hio sio namba ya seat yako, seat yako ni hii Akibisha muite konda wa gari.

Mbona issue zingine simple tu mzee..
Siti ya dirishani sikai hofu kupigwa pasi
 
M Me huwa namtoa tu mkuu hiyo sio siti yako simama kakae kwako.
 
Kuna siku nilikaa siti ya dirishani mwenye siti akaja akaogopa kunisemesha akaenda kumfata konda, konda akaja kunitoa...

Sasa katikati ya safari kumbe lile dirisha la upande wake alifungi vizuri, alipigwa na upepo karibia afeee nailikua usiku...

Ikabidi aniombe niamie pale apate unafuu, mimi nikaamia iyo siti ya dirishani pale panapotoa upepo nikachomeka masai shuka upepo ukakata...
Cha kushangaza akawa ameona wivu tena ila ninacho shukuru alikuja akawa pisi yangu kama miezi miwili
 
Tabia hiyo wanayo sana wanawake.Na bado kama ana mtoto anakuajiri kwa muda uwe yaya wake.
Aseee nilishawahi kupewa majukumu ya kulea kwa masaa mengi sana ya ile safari
Mbaya zaidi watoto wanakula kila muda huku mimi nikiwa kinyume chao....sipendi kabisa kula safarini na huwa naomba nisikae na mtu anayekula kula hovyo

Yule mama alikata siti moja wakati ana watoto wadogo wawili...wabongo safari ya kustaarabika bado ni ndefu sana!!!!

Komenti yako imeibua hasira upya ya ile safari
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…