Kero ya kukuta mtu kakaa kwenye siti yako ya dirishani kwenye Bus.

Kero ya kukuta mtu kakaa kwenye siti yako ya dirishani kwenye Bus.

Aseee nilishawahi kupewa majukumu ya kulea kwa masaa mengi sana ya ile safari
Mbaya zaidi watoto wanakula kila muda huku mimi nikiwa kinyume chao....sipendi kabisa kula safarini na huwa naomba nisikae na mtu anayekula kula hovyo

Yule mama alikata siti moja wakati ana watoto wadogo wawili...wabongo safari ya kustaarabika bado ni ndefu sana!!!!

Komenti yako imeibua hasira upya ya ile safari
Joanah the baby-sitter.😂
 
jf kuna watu mnapanda bus si mlisema mnatumia ndege
Hata kwenye ndege kiongozi hao watu wapo, unamkuta kakaa kimya, ukimwambia anaanza sababu.

Binafsi iwe bus iwe ndege lazima nimueleze mtu kistaarabu tu, siti ya dirishani si ya kumuachia mtu isipokuwa kwa dharura ya kueleweka sana.
 
Mie huwa nawachomoa faster tu,sionei haya mtu.
Labda aniombe,na awe na sababu ya msingi.
 
Kama gari halitumii AC nitamsihi tu asifunge dirisha. Kuna wengine wanang'ang'ania kukaa upande wa dirisha na wanaogopa upepo. Akikubali masharti haina shida. Akikataa nitaomba tu anipishe.
Kuna zee moja lilikatalia dirishan na siti ni yangu kwa kumheshimu nikamuacha , sasa Wakat wa safari nikamuomba afungue dirisha akakataa et upepo mkali. Mbona nilimtoa nikakaa mie maana karibu basi Zima walikuwa wamefunga madirisha hewa ikawa nzitoo .
 
Mna deal vipi na hawa watu maana kusafiri ni starehe pia.

Yaani una chagua siti yako ya dirishani una lipia ili kesho usafiri kwa raha uki enjoy mazingira afu una kuta mtu kakaa kwenye iyo siti na wala hajiongezi kabsa ana jikausha kimya as if hamna kilicho tokea .

Binafsi hili jambo lina nikera sanaa na ubaya huwa siwezi kumwambia mtu atoke kwenye siti yangu kuepusha maneno.

Ila watanzania mjaribu kuwa wastaarabu kama una jijua umechelewa kukata ticket na uja kata ya dirishani ni kheri uombe au ukae siti yako sio una jiwahisha mapema afu una jiona mjanjaa kumbe jinga tu.
Hakuna siti ninazo chukia kukaa kama siti za dirishani ambazo hakuna kufungua dirisha, bora mara kumi elfu nikae siti ya koridoni ndiyo najiachia vizuri zaidi!!
 
Kumuacha mtu akae kwenye seat ambayo imesajiriwa kwa majina yako katika trip hiyo ni kosa kubwa...

Kwahiyo kama unakua mzito before haujakaa yafaa umuulize like eti seat yako ni namba ngapi, akisema seat number unamwambia asogee kwenye seat yake, hakuna abiria wa safari ndefu unaemwambia akupishe seat yako akaanza kuleta maneno maneno, labda awe hana akili timamu... mimi ni introvert ila sijawahi kushindwa kumwambia mtu anipishe kwa seat coz kuna njia nyingi za kumwambia apishe bila kumwambia apishe.
 
Ila ukikuta pisi kali unatulia 😂😂

Kuna siku nilipanda bus nikakaa siti ya dirishani sio yangu ila jamaa akawa humble na vocha nilinunuliwa acha chakula cha njiani nilifaidi 🤣🤣🤣
Aliomba namba nikamwambia anipe zake tulivyoshuka nikafuta 😹
 
Nitamwambia Straight, kwamba amekaa kwenye Siti yangu, akihama sawa, akiwa Mbishi Wala sijibizani nae, naenda Kwa Kondakta, Kondakta atakuja kunipa Siti yangu.
 
Back
Top Bottom