Kero ya kukuta mtu kakaa kwenye siti yako ya dirishani kwenye Bus.

Mi namwambia Mara ya kwanza atoke kwenye siti yangu kistaarabu kabisa,after that asiponisikiliza nitatupwa dirishani🤨
 
5 na 33 hakuna maridhiano hapo kila mtu akae kwake kwa amani tu,bora ingekua siti za next door to door!!
 
Kwa sasa ticket zinauzwa online na ukiingia kwenye hizo site za mabasi unaona siti zilizobakia,changamoto inatokea kwa wale wanaokata tiketi kwa vishoka hawa ndio hua wanaleta hizo shida kwakua wanauziwa ticket ambazo hazipo,nilikwisha kuta huo ugomvi kwenye mabasi na haswa kutokea mikoani kuja mijini at least toka mijini kwenda mikoani haipo sana
 
Kwanini mkuu?
Sipendi tu na nadhani mazoea yameshaniharibu tayari. Huwa sipendi kubanwa banwa. So nikikaa dirishani let say upande wa dereva ina maana kulia dirisha na kushoto kuna mtu whili nisipokaa dirishani, kulia kuna mtu na kushoto kuna space ya kutembea watu. Halafu pia mi napenda ile hanger ya mkono inayokua kwenye siti.
 
Mi naonaga ni ushamba tu, huko dirishani kuna kipi cha maana?
 
Sasa ukute gari ya Mbeya Dar. Mmama wa kinyakyusa wa Kyela wale kichwa ngumu mwenye mtako mkubwa amewahi siti yako, ushirikiano Hana kibaya zaidi mtako wake umekuja mpaka hii siti uliyokalia. Kibaya zaidi muda wote anatafuna Kama sio kipaja Cha kuku basi Ni mahindi ya kuchemsha, kinachoumiza zaidi akiacha kutafuna anaongea na simu kwa kinyakyusa, kibaya Sana Sana mkishavuka Morogoro anaanza kusinzia na kuachia valvu zote.
Siku hizi ufaidi hela yako panda Basi la 1x3. Hugusani na raia yoyote.
 
Ustaarabu hamna kabisa, vitu vidogo sana sijui ni kutokujitambua au kutokujua. Nilishakuta ugomvi wa siti, Hadi aibu kabisa, vitu vidogo mnoooo hivi.

Binafsi Wala sifagilii hayo mambo, kama unalitaka dirisha basi nakuachia nafasi kiroho safi.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…