Ninawasilisha kero kuhusu watu wanaotoa mahubiri au kutangaza bidhaa zao ndani ya mabasi ya mikoani. Kwa kweli, jambo hili limekuwa kero kwa abiria wengi wanaohitaji kusafiri kwa utulivu.
Safari ni muda wa abiria kupumzika, lakini si kila mtu anayekuwa safarini yuko katika hali ya kusikiliza mahubiri au matangazo. Wengine wanakuwa wamefiwa na wanaelekea kwenye mazishi, huku wengine wakisafiri kwenda kuwaona wagonjwa hospitalini au kwa sababu nyingine zinazohitaji utulivu.
Naiomba mamlaka husika ilifuatilie suala hili na kuweka utaratibu utakaolinda haki ya abiria kusafiri kwa amani na utulivu bila kulazimika kusikiliza mahubiri au matangazo yasiyo ya hiari yao.