JUAN MANUEL
JF-Expert Member
- Nov 26, 2010
- 7,808
- 16,972
Huwezi kutatua shida kwa njia ya maonyesho kama wanavyofanya!Nimekuwa nikifuatilia wananchi wa Mkoa wa Arusha wakitoa kero zao mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Arusha Ndugu Makonda. Kwa asilimia kubwa lazima sheria zifuatwe na Mkuu wa Mkoa hayuko juu ya sheria. Inawezekana kero nyingi zilizotolewa tayari aidha ziko Mahakamani au uamuzi wa kisheria ulikwishapitiwa.
Mimi naona wananchi wengi wanapoteza muda wao na hawatasaidiwa chochote na Mkuu wa Mkoa ni vema wakafuata taratibu za kisheria. Hata yule Mwanasheria wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha alioagiza ahamishwe, mimi naona siyo utawala bora kusema mbele ya watu kuwa ahamishwe.
Usitafute popularity ambayo haisaidii. Najua wananchi wana kero nyingi na wanaonewa lakini ni budi sheria zifuatwe kutatua kero hizo.
Kuna taasisi ilibidi ziwe zinashughulikia haya Mambo, Polisi, takukuru, mahakama,
Kama kila mkuu wa mkoa akiitisha mkutano kusikiliza kero za watu, tuna wakuu wa mikoa 26! Wananchi wapo milioni 60! Utaweza vipi kusikiliza kero zao? Ofisi zenu zina kazi gani?