Kesho Mwanza CHADEMA itaifunika CCM sherehe za uhuru. Wakuu wa chama kuhudhuria

Hao ni wasanio tu wasikupe tabu.Mbowe akienda Kia anapanda ATC

..hizo ni ndege za magufuli siyo za waTz.

..zingekuwa za waTz zisingeandikwa campaign slogan za magufuli.
 
Aende wapi! Kashindwa kwenda hapo Kurasini Askari wake Tisa (9) walio uawa Mkiru yeye anaenda kufungua zile expansion joints pale UDSM?
Hakika ingekuwa JK au watangulizi wengine kama CiC hata kama wangekuwa wagonjwa wangeahirisha zoezi lile.

Sio lazima kila msiba aende rais. Kama mnampenda sana JK mkaribisheni mkanywe naye chai.
 
Lini rais aliongea kikabila ambacho Watanzania walengwa hawakuelewa? Akiongea Kiingereza ni sawa au sivyo?

..kuna wakati huyu mzee anajiona ni raisi wa kule, na wakati mwingine raisi wa waTz wote.

..mbona nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete, hawakuwahi kuongea lugha za makabila yao?
 
..hizo ni ndege za magufuli siyo za waTz.

..zingekuwa za waTz zisingeandikwa campaign slogan za magufuli.

Kama unapenda iwe hivyo sio mbaya. Nasikia wana copy right ya hayo maneno.
 
Hata wakizikashifu haiondoi maana kuwa hata wao ni zao. Fedha zilizonunulia hata kama kwa utaratibu mbaya bado zao, gharama za uendeshaji bado zao nk.
Kwanza wanachama na wapenzi wa Chadema ndio wachangiaji wakubwa wa kodi maana ndio wasomi wengine wenye kazi nzuri, biashara nzuri na kubwakubwa tofauti na CCM ambayo wapenzi wake na wanachama wengi hawana elimu, masikini na wazee.
(Hiyo sisemi Mimi lakini ni tafiti ya Twaweza)
 
..hizo ni ndege za magufuli siyo za waTz.

..zingekuwa za waTz zisingeandikwa campaign slogan za magufuli.
Wakija chadema watakewa kata funua na operation sangara,usiwe na hofu
Yaani neno hapa kazi tu linakuumiza,hutaki tufanye kazi?
 
..kuna wakati huyu mzee anajiona ni raisi wa kule, na wakati mwingine raisi wa waTz wote.

..mbona nyerere, mwinyi, mkapa, kikwete, hawakuwahi kuongea lugha za makabila yao?

Nyerere yupi? Mbona alikuwa anaongea kizanaki tu, hata kigogo alikuwa anakimanya wacha uongo. Laba useme hao wezi waliofilisi nchi hii kina Mkapa na JK waliouza mashirika ya umma wakati wao.
 
Sio lazima kila msiba aende rais. Kama mnampenda sana JK mkaribisheni mkanywe naye chai.

..haiyumkiniki askari wapoteze maisha namna ile halafu Raisi asiende kutoa heshima na kuwafariji wanafamilia na askari wenzao.

..wakati mwingine watu kama nyinyi mnampotosha raisi kwa kushindwa kusimamia ukweli.
 
Lini rais aliongea kikabila ambacho Watanzania walengwa hawakuelewa? Akiongea Kiingereza ni sawa au sivyo?
We ile lugha ya kuchungia ng'ombe anayochanganya Mara nyingi unadhani kila mtu anamuelewa?
We wengine wanakula nyama kila siku lakini hawajawahi kumuona huyo ng'ombe
 
Hapo ndipo unapoonesha umbumbu wako, kwani hao twaweza walitoa hizo takwimu kufuata uchama? Ati wasomi wengi na sisi ambao ni wasomi tuseme nini au kwa sababu sio wana Chadema? Hii ni mpya yaani biashara zote kubwa zinamilikiwa na Chadema? Haya endelea kuwasingizia twaweza.
 
Nyerere yupi? Mbona alikuwa anaongea kizanaki tu, hata kigogo alikuwa anakimanya wacha uongo. Laba useme hao wezi waliofilisi nchi hii kina Mkapa na JK waliouza mashirika ya umma wakati wao.

..hapana.

..Nyerere alikuwa haongei Kizanaki kwa namna hii ambayo Magufuli anahutubia Kisukuma.

..Nyerere alikuwa akitoa "stori" au akitumia misemo ya Kizanaki alikuwa akitoa tafsiri ya Kiswahili hapo hapo.

..Magufuli anaongea Kisukuma na kuwatenga waTz wengine wasijue Raisi wao ameongea nini. That never happened wakati wa Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere.
 
We ile lugha ya kuchungia ng'ombe anayochanganya Mara nyingi unadhani kila mtu anamuelewa?
We wengine wanakula nyama kila siku lakini hawajawahi kumuona huyo ng'ombe

This is below the belt.
 
At least unakubali alikuwa anaonga Kizanaki lakini sasa ndio unatolea ufafanuzi ...... ....... .... BTW wakati ule mwalimu alikuwa ana-deal na watu wengi ambao sio wasomi leo hii baada ya miaka 60 kwa nini JPM asiongee lugha anazozifahamu alikuwa anaongea kigogo few weeks ago, alipokuwa Mtwara aliongea kimakonde what the hell do you people want a president to do. Tanzanians wanamuelewa wewe na chama chako mnampinga ati kisa kisukuma hamkimanyi jifunzeni. BTW hakuna Mtanzania anayebaguliwa ubaguzi upo kwenye chama cha Chadema.
 
Ni vigumu sana kumsusia au kumnunia aliyenacho.

Waache watakufa siku si zao JPM anafanya kazi ambayo inailetea heshima Tanzania kila mahali ulimwenguni.
 
..huko kwa makabila mengine huwa anasalimia tu.

..lakini akifika Usukumani inakuwa habari nyingine.

..tuwe wakweli kwamba kila kiongozi akiamua kuiga mfano huu wa Magufuli bado tutakuwa na nchi, au tutagawika vipande vipande.

..Pamoja na tatizo la ukabila, kuna tatizo la matamko ya kidini-dini ktk shughuli za kiserikali.

..TUJISAHIHISHE.
 
Nyerere alikuwa haongei Kizanaki kwa namna hii ambayo Magufuli anahutubia Kisukuma.
Mkuu huyu Jamaa wa Pale Magogoni (JPM) hajui lugha nyingine yeyote ya kitaifa na kimataifa zaidi ya vilugha (vernacular) hasa kisukuma. Sasa unategemea nn? Hana option nyingine ya kujimwambafai zaidi ya kisukuma.

Ndiyo maana ziara zake 90% ni huko huko kanda ya ziwa.
 
JPM anafanya kazi ambayo inailetea heshima Tanzania kila mahali ulimwenguni.
Ulomwengu upi mkuu? Labda kama kuna ulimwengu wa chuki, visasi, utekaji na mauaji
 
Wacha uongo wewe, ziara za JPM zinajulikana weka fact hapa kama unataka. Amekwenda huko Moshi na Arusha mara ngapi? Tanga nk. Kabla ya hii ziara alikuwa wapi? Mtwara, Mbeya, Dodoma nk. Wacha kuhesabu likizo yake wakati alitembelewa na Kenyata ulitaka ahamie Moshi? Wacha wivu wa kike.

Mkuki kwa nguruwe eeeh? Umesahau wakati wa Msuya na Mramba ambao walikuwa mawaziri tu?

BTW JPM anaweza kuongea lugha nyingi wewe Je? Ana shahada zinazotambulika ulimwenguni wewe Je?
 
Ulomwengu upi mkuu? Labda kama kuna ulimwengu wa chuki, visasi, utekaji na mauaji

The universe has several planets, one of them is called earth.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…