Missile of the Nation
JF-Expert Member
- May 24, 2018
- 17,047
- 63,206
Kesi dhidi ya Lissu imejikita kwenye dhana kuwa ametoa kauli ya
1. Kuhamasisha uasi
2. Kuzuia uchaguzi
3. Kukinukisha.
Makosa yote hayo ni abstract, hayana legal stand na ni vigumu kwa Jamhuri kutengeneza kesi ya maana. Sanasana inaenda kumdhalilisha SSH, Polisi, Mwendesha Mashitaka na dola kiujumla nitaeleza.
1. Neno uasi, kisheria limekaaje?
Hakuna sheria hata moja nchini inayojikita kwenye neno "UASI". Bali kuna sheria mama ndani ya katiba inayozungumza UHAINI. Na katiba ikaeleza kwa kirefu uhaini ni nini na ni wakati gani mtu anaweza kuwa ametenda kosa la UHAINI. Hivyo Basi UASI WENYE KUPELEKEA UHAINI HILO NI KOSA KISHERIA ila UASI KWA MAANA YA KUPINGA UVUNJIFU WA SHERIA KAMA VILE KUNYIMA WANANCHI HAKI YAO YA KUCHAGUA VIONGOZI HALALI, KURA FEKI, HUO SIYO UHAINI BALI NI WAJIBU WA MSINGI WA MWANANCHI.
Pili kilugha neno Uasi linaweza kubeba maana nyingi kwa mfano, linaweza kumaanisha
1. Rebellion
2. Disobedience
3. Revolt
Disobedience kwa maana ya Civil Disobedience haiwezi kumaanisha Uhaini. Na Lissu hakuzungmzia mahali popote armed Struggle. Kwa hiyo itakuwa ni jukumu zito kwa Jamhuri kuthibitisha mahakamani ni Uasi gani huo Lissu kausema ambao ni.kinyume cha sheria zetu.
2. Kuhamasisha kuzuia uchaguzi.
Hapa wala hakuna mashiko yoyote ya kumtia ndani Lissu. Zipo njia za kisheria za kuzuia uchaguzi. Mahakama inaweza kuzuia uchaguzi ikithibitika kuwa zipo sababu za msingi za kisheria kuuzuia uchaguzi. Sasa Jamhuri ikathibitishe mahakamani kuwa Lissu aliposema watazuia uchaguzi hakumaanisha kuwa Watakwenda kuuzuia mahakamani!. Au hawatawaburuza mahakamani wote watakaofanya vitendo haramu vya kuendesha uchaguzi kinyume cha haki.
3. Kwamba Lissu atawashawishi watu kukinukisha.
Ndiyo, tutakinukisha kwelikweli Facebook, Instagram, hapa JF. Yaani tutapiga kelele kwelikweli jinsi uchaguzi ulivyombovu, tutataka watakaoendesha uchaguzi mbovu wawajibike. Yaani tutatiknukisha kwa maandamano halali ya amani, tutakinukisha kwa kupetition jumuia za kimataifa.
Hahahaha
Jamhuri inaweza kumfunga Lissu kiubabe tu, kimagumashi tu lakini Hakuna kesi hapo zaidi ya kwenda kujiaibisha mahakamani!.