GE2025 Kesi iliyotoa zuio la CHADEMA kutofanya siasa yahairishwa hadi Julai 14

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Joined
Apr 18, 2017
Posts
5,352
Reaction score
15,876
Kesi Namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha CHADEMA kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, inatarajiwa kuendelea Julai 10, 2025 mbele ya Mh. Jaji Hamidu Mwanga katika Mahakama Kuu-Dar es salaam.

June 24, 2025 ilikuwa imepangwa kusikilizwa, lakini ikaelezwa Mh. Jaji Hamidu ambaye anasikiliza kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine Mkoani Mtwara.

Ikumbukwe kesi hiyo ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Ambapo iliwasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi ya msingi waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama

1752130825193.png

KESI YAHAIRISHWA HADI JULAI 14

Kesi namba 8323/2025 ya mgawanyo wa rasilimali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyokuwa inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 14, Julai 2025 saa nne asubuhi.

Ahirisho hili limekuja baada ya mawakili wa upande wa waleta maombi kuiomba mahakama kupata muda wa kwenda kuisoma na kutafakari barua iliyopelekwa mahakamani hapo na upande wa wajibu maombi (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu).

Wakili wa wajibu maombi Mpale Mpoki aliieleza Mahakama kuwa wateja wake waliandika barua kwenda kwa Naibu Msajili wa Mahakama kuomba na kutaka Jaji Hamidu Mwanga ajitoe kusikiliza kesi namba 8323/2025.

Wakili Mpoki ameileza mahakama kuwa walichelewa kuupatia upande wa waleta maombi nakala ya barua kutokana na kwamba barua hiyo ilikuwa ni ya mahakama tu hivyo hawakufahamu kama upande wa waleta maombi wanapaswa kuapatiwa nakala ngumu.

Hata hivyo kuahirishwa kwa shauri hilo kunaathiri maombi yaliyowasilishwa mahakamani na upande wa CHADEMA ya kuiomba mahakama kufuta uamuzi alioutoa Jaji Mwanga Juni 10, juu ya kusimamishwa kwa shughuli za CHADEMA.

Hivyo Jaji Mwanga amesema maombi hayo madogo yatafanyiwa kazi baada ya uamuzi kutoka wa yeye kuendelea na kesi hiyo au lah.

1752143492498.png

1752130825193.png
 
Kesi Namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha CHADEMA kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, inatarajiwa kuendelea Julai 10, 2025 mbele ya Mh. Jaji Hamidu Mwanga katika Mahakama Kuu-Dar es salaam.

June 24, 2025 ilikuwa imepangwa kusikilizwa, lakini ikaelezwa Mh. Jaji Hamidu ambaye anasikiliza kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine Mkoani Mtwara.

Ikumbukwe kesi hiyo ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Ambapo iliwasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi ya msingi waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama.
Sema MBOWHE anahangaika sana. Naona bado ana maumivu makubwa sana moyoni mwake, hakujiandaa wala kutegemea kwamba kuna siku KISU alichojua butu kitakuja kumkata.. Kweli alikua mfanyabiashara wa SIHASA.
 
Yote haya kayataka Mbowe. Hivi angestaafu kwa heshima na kukabidhi chama kwa Lissu au Heche shida ingetokea wapi?. Leo chama kingekuwa kimoja na kingeingia kwenye uchaguzi na nguvu mpya. Yeye akalazimisha mwishowe kapigwa ngwara. Sasa yeye na kundi lake wanataka kukiangamaiza chama. Mtu ni mwanavhama wa CHADEMA unataka chama kisifanye siasa then what?. Lengo lako ni Nini?. Watu walikuwa CHADEMA kimaslahi.
 
Kesi Namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha CHADEMA kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, inatarajiwa kuendelea Julai 10, 2025 mbele ya Mh. Jaji Hamidu Mwanga katika Mahakama Kuu-Dar es salaam.

June 24, 2025 ilikuwa imepangwa kusikilizwa, lakini ikaelezwa Mh. Jaji Hamidu ambaye anasikiliza kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine Mkoani Mtwara.

Ikumbukwe kesi hiyo ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Ambapo iliwasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi ya msingi waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama

Wastage of funds, time and resources
 
Yote haya kayataka Mbowe. Hivi angestaafu kwa heshima na kukabidhi chama kwa Lissu au Heche shida ingetokea wapi?. Leo chama kingekuwa kimoja na kingeingia kwenye uchaguzi na nguvu mpya. Yeye akalazimisha mwishowe kapigwa ngwara. Sasa yeye na kundi lake wanataka kukiangamaiza chama. Mtu ni mwanavhama wa CHADEMA unataka chama kisifanye siasa then what?. Lengo lako ni Nini?. Watu walikuwa CHADEMA kimaslahi.
Upo sahihi kabisa expert wangu,mwamba bado alikuwa na nia ya kuendelea kukalia kiti

Naamini mwamba angeacha mwenyewe kwa hiari yake angekuwa tayar kushirikiana na wenzake
 
Yote haya kayataka Mbowe. Hivi angestaafu kwa heshima na kukabidhi chama kwa Lissu au Heche shida ingetokea wapi?. Leo chama kingekuwa kimoja na kingeingia kwenye uchaguzi na nguvu mpya. Yeye akalazimisha mwishowe kapigwa ngwara. Sasa yeye na kundi lake wanataka kukiangamaiza chama. Mtu ni mwanavhama wa CHADEMA unataka chama kisifanye siasa then what?. Lengo lako ni Nini?. Watu walikuwa CHADEMA kimaslahi.
Inashangaza sana..
 
Back
Top Bottom