GE2025 Kesi iliyotoa zuio la CHADEMA kutofanya siasa yahairishwa hadi Julai 14

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kesi hii ni njama ya timu Mbowe baada ya kushindwa uchaguzi ukiokuwa HURU na HAKI walijaribu kuushinikiza uongozi mpya kwamba na timu yao iwe ndani ya mfumo.
Sasa baada ya kuona wengi wao hasa wale wa makao makuu wamebwagwa - ndiyo hii mizongi zongi ikaanza pamoja na hili la kutaka kujaribu kukifuta chama kupitia kesi ambayo ina baraka zote na msajili wa vyama, Kama muemdelezo wa mashambulizi wakafungua chama kipya iwe mnadala wa CDM baada ya kumvamia mzee wa ubwabwa.

Hata hili nalo si muda mrefu kitafeli vibaya sana sababu Shetani ( Roho chafu) huwa hafurukuti kwenye Haki.
Kesi imalizike mwezi November mwanzoni kabisa
 
Mbona mnakwepa kuwajibika? Mbowe angestaafu vipi kwa heshima wakati mlimwandama kwa kejeli na matusi? Angestaafu si ndio mngezidi kumbeza kuwa amewaogopa? Pamoja na matusi na mbinu chafu Mbowe aliwezesha uchaguzi ufanyike kwa uwazi na weledi mkubwa. Aliposhindwa akaaga akaenda zake na Mwenyekiti Mpya akamwambia apumzike na achukue likizo.

Uongozi mpya ndio walikuwa na uwezo wa kuunganisha chama sio Mbowe. Lakini badala ya kufanya hivyo wakaendekeza siasa ya visasi na kuwatenga wale ambao waliamini wako bado upande wa Mbowe. Ulikuwa ndio wakati wa kutamba warriors wa social media ambao furaha yao ilikuwa kwenye mzodoa na kumbeza Mbowe na wale ambao waliamini kuwa ni timu yake. Uongozi wa Chadema haukuwakemea, ukaweka pamba masikioni. Walikaa kimya hata pale kiongozi mmoja alipopigwa na walikataa hata kwenda kumuona. Matokeo ya yote hayo ni wakina Mrema kuamua hamna sababu ya kung'ang'ania chama ambachl hakiwataki. Uongozi wa sasa wakasema good riddance na mpaka leo wanaendelea kuwasema kwenye majukwaa yao. Sasa hivi adui mkubwa wa Chadema amekuwa ni Chaumma, sio CCM.

Yanayoendelea Chadema ni matokeo ya uongozi mpya na sio mtu mwingine. Pambanieni hali yenu, muacheni Mbowe aendelee kupumzika.

Amandla...

..kesi ilioko mahakamani haitokani ni matendo au maamuzi ya uongozi mpya wa Chadema.

..hii ni kesi ya hila tu dhidi ya uongozi mpya. Wadai walioko mahakamani kiuhalisia wanalalamika kwamba uongozi wa Mbowe uliwabagua na kuwapunja rasilimali za chama. Lakini kwasababu Chadema ni chama cha siasa, hivyo makosa yaliyofanyika huko nyuma, yanaweza kuadhibu hata uongozi mpya.
 
Kumtetea Mbowe na genge lake hili linalokishitaki chama ni kazi sana.
Umejipa kazi ngumu ambayo hutaiweza.
 
..kesi ilioko mahakamani haitokani ni matendo au maamuzi ya uongozi mpya wa Chadema.

..hii ni kesi ya hila tu dhidi ya uongozi mpya. Wadai walioko mahakamani kiuhalisia wanalalamika kwamba uongozi wa Mbowe uliwabagua na kuwapunja rasilimali za chama. Lakini kwasababu Chadema ni chama cha siasa, hivyo makosa yaliyofanyika huko nyuma, yanaweza kuadhibu hata uongozi mpya.
Mimi nilikuwa najibu bandiko lililokuwa linamlaumu Mbowe na kusema kuwa yuko nyuma ya kesi nzima bila ushahidi wowote.

Inawezekana kabisa kuwa walioshitaki wamefanya hivi ili kuukomoa uongozi mpya. Uongozi mpya hauwezi kukwepa lawama kwa jinsi ambavyo wali wa handle wale walioonekana kuwa wa upande wa pili. Ungewekeza nguvu za ziada katika kuponya majeraha yaliyotokana na uchaguzi pengine haya yasingetokea. Matendo ya uongozi na wafuasi wao yamechangia sana kujenga chuki ambayo ndio inatumika kujaribu kuivuruga Chadema. Jeuri na kibri ndio zimewafikisha hapa. Kiongozi makini angehakikisha chama chake hakifikishwi hapa kilipofika. Kumsingizia Mbowe hakusaidii kitu.

Waliitwa kwenye retreat wakakataa kwenda sasa ulitaka wafuatwe majumbani kwao? Haya yote kayataka Mbowe, kama angeheshimu ahadi yake aliyotoa 2019 kuwa hatagombea tena angeacha kwa heshima kubwa lakini kakubali kushikiwa akili na Mzanzibari akaamuabkuondoka kwa fedheha.
 
Kesi imalizike mwezi November mwanzoni kabisa
Samia anamuogopa sana Lissu kwenye sanduku la kura ndiyo maana ametumia nguvu kubwa sana ya vyombo vya dola kumdhibiti, kwenye uwanja sawa wa uchaguzi Samia saa nne tu chali.
 
Kesi Namba 8323/2025 ambayo imetoa zuio la muda kwa Chama cha CHADEMA kufanya shughuli zozote zile kiutendaji na oparesheni mpaka pale kesi ya msingi iliyofunguliwa itakapoanza kusikilizwa, inatarajiwa kuendelea Julai 10, 2025 mbele ya Mh. Jaji Hamidu Mwanga katika Mahakama Kuu-Dar es salaam.

June 24, 2025 ilikuwa imepangwa kusikilizwa, lakini ikaelezwa Mh. Jaji Hamidu ambaye anasikiliza kesi hiyo alikuwa na majukumu mengine Mkoani Mtwara.

Ikumbukwe kesi hiyo ilifunguliwa na aliyewahi kuwa Makamu Mwenyekiti wa chama hicho Zanzibar, Saidi Issa Mohamed na wenzake wawili (2) dhidi ya Baraza la Wadhamini na Katibu Mkuu wa CHADEMA.

Ambapo iliwasilishwa Mahakamani hapo na Mawakili wa waleta maombi wakiongozwa na Wakili Gido Thomas Simfukwe ambao waliiomba Mahakama kuweka zuio hilo hadi kesi ya msingi itakapoanza kusikilizwa.

Katika kesi ya msingi waleta maombi waliwasilisha madai kuwa CHADEMA imekuwa ikiitenga Zanzibar katika masuala mbalimbali ikiwemo mgawanyo wa raslimali za Chama

KESI YAHAIRISHWA HADI JULAI 14

Kesi namba 8323/2025 ya mgawanyo wa rasilimali za Chama cha Demokrasia na Maendeleo iliyokuwa inaendelea katika Mahakama Kuu ya Tanzania Masjala Ndogo ya Dar Es Salaam, imeahirishwa mpaka Jumatatu ya tarehe 14, Julai 2025 saa nne asubuhi.

Ahirisho hili limekuja baada ya mawakili wa upande wa waleta maombi kuiomba mahakama kupata muda wa kwenda kuisoma na kutafakari barua iliyopelekwa mahakamani hapo na upande wa wajibu maombi (Wajumbe wa Bodi ya Wadhamini wa CHADEMA na Katibu Mkuu).

Wakili wa wajibu maombi Mpale Mpoki aliieleza Mahakama kuwa wateja wake waliandika barua kwenda kwa Naibu Msajili wa Mahakama kuomba na kutaka Jaji Hamidu Mwanga ajitoe kusikiliza kesi namba 8323/2025.

Wakili Mpoki ameileza mahakama kuwa walichelewa kuupatia upande wa waleta maombi nakala ya barua kutokana na kwamba barua hiyo ilikuwa ni ya mahakama tu hivyo hawakufahamu kama upande wa waleta maombi wanapaswa kuapatiwa nakala ngumu.

Hata hivyo kuahirishwa kwa shauri hilo kunaathiri maombi yaliyowasilishwa mahakamani na upande wa CHADEMA ya kuiomba mahakama kufuta uamuzi alioutoa Jaji Mwanga Juni 10, juu ya kusimamishwa kwa shughuli za CHADEMA.

Hivyo Jaji Mwanga amesema maombi hayo madogo yatafanyiwa kazi baada ya uamuzi kutoka wa yeye kuendelea na kesi hiyo au lah.

View attachment 3400212
View attachment 3400022
Mbowe na wtu eake walikihujumu chama muda mrefu sana na bado wsnaendelea.
 
Inashangaza sana..
Ililazimu iwe hivi ili chama imara kijitokeze mbele.

Mbowe na kundi lake wangenyamaza, huku wakiwa na uchungu moyoni, chama kingeendelea kuwa na matatizo makubwa sana.

Ngoja haya ya ite ili CHADEMA imara izaliwe.
 
Waliitwa kwenye retreat wakakataa kwenda sasa ulitaka wafuatwe majumbani kwao? Haya yote kayataka Mbowe, kama angeheshimu ahadi yake aliyotoa 2019 kuwa hatagombea tena angeacha kwa heshima kubwa lakini kakubali kushikiwa akili na Mzanzibari akaamuabkuondoka kwa fedheha.
Mtu ambae yuko committed kuponya majeraha angeongeza jitihada, hata kama ni kuwafuata nyumbani.
Mbowe alitangaza kugombea baada ya nyie kumkebehi, kumwambia amelamba asali, kuwa yeye ni msaliti na ampishe mtu wenu. Mngefanya kampeni ya kistaarabu angeweza kuachia ngazi. Lakini bila shaka baada ya kuona aina ya watu wanaomtaka afanye hivyo akaamua sio tu kugombea bali kulipia sehemu kubwa za gharama za uchaguzi. Mlitaka aondoke kama mbwa koko lakini ameondoka kwa term zake. Hata mumtukane vipi ataendelea kuheshimiwadla kwa uungwana aliouonyesha.

Badala ya kumuandama mtu ambae mlisema hamumtaki, kipiganieni chama chenu kwa vitendo ama sivyo kweli kitapotea kama vingine vilivyokitangulia.

Kuhusu kampeni chafu pande zote mbili zilishambuliana na lugha za kuudhi zilitumika kumbuka kauli za Ntobi na Yericko Nyerere dhidi ya Lissu, wewe umeamua kuchukua upande ndiyo maana unafumbia macho mapungufu yaliyokuwa kambi ya Mbowe.
 
Yericko na Ntobi walikuwa wanajibu mashambulizi yenu. Na kuna tofauti kubwa kati ya kumuita mtu mropokaji na kumuita mwingine msaliti. Msaliti huku yake ni kifo wakati mropokaji ana dharauliwa tu.

Lakini pamoja na yote hayo Mbowe aliwakemea mapema wakina Ntobi na wakaacha. Lissu hajawahi kukemea lugha za matusi na kejeli za watu wake. Na mpaka sasa hivi si yeye au Heche aliyewahi kuzikemea. Hiyo ndio tofauti yao.

Pambaneni na mambo yenu. Pamoja na kujibhalaghua kwenu hizo threat zinaweza kuathiri vibaya chama chenu. Zipeni umuhimu zinazostahili. Achaneni na Chaumma.

Amandla...
 
Back
Top Bottom