GE2025 Kesi iliyotoa zuio la CHADEMA kutofanya siasa yahairishwa hadi Julai 14

Matukio, Taarifa, Habari na Mijadala ya Wananchi WAKATI wa Mchakato wa Uchaguzi Mkuu 2025
Kesi hii ni njama ya timu Mbowe baada ya kushindwa uchaguzi ukiokuwa HURU na HAKI walijaribu kuushinikiza uongozi mpya kwamba na timu yao iwe ndani ya mfumo.
Sasa baada ya kuona wengi wao hasa wale wa makao makuu wamebwagwa - ndiyo hii mizongi zongi ikaanza pamoja na hili la kutaka kujaribu kukifuta chama kupitia kesi ambayo ina baraka zote na msajili wa vyama, Kama muemdelezo wa mashambulizi wakafungua chama kipya iwe mnadala wa CDM baada ya kumvamia mzee wa ubwabwa.
1. Chama kina kesi na hakiruhusiwi kufanya siasa.
2. Chama kimenyimwa Ruzuku
3. Mwenyekiti ana kesi ya uhaini
4. Baadhi ya viongozi hawatambuki na msajili wa vyama

Haya yote Hata muda si mrefu yatafeli vibaya sana sababu Shetani Roho chafu) huwa haifurukuti kwenye Haki.
 
..hii ya kumkataa Jaji nadhani inawapotezea muda Chadema na kuwazuia wasiendelee na shughuli za chama.

..walichopaswa kufanya ni kupinga tu uamuzi wa Jaji kuwazuia kufanya siasa, pamoja na kuwazuia kutumia mali za chama.

..Chadema wafanye maamuzi kama wanasiasa, sio kama wanasheria.

..Wanasheria wanapenda sana mivutano ya TECHNICALITIES / MAPINGAMIZI na hawaoni shida kupoteza muda mahakamani.

Cc Nguruvi3
 
Mahakama za chama
 
CHADEMA WANAKUWA KAMA HAWANA AKILI SASA HAO JUMATATU WATAAMBIWA SAWA JAJI AMEJITOA WASUBIRI WAONE JAJI GANI ATAKUWA AVAILABLE ITAAHIRISHWA MWEZI WAKIJA WANAEWA JAJI MWINGINE NAYE ANAAHIRISHA ILI ASOME MWENENDO WA KESI HAO CHADEMA NI CCM B WAMENUNULIWA WANAKULA MUDA TU SIKU ZIENDE
 
Mbona mnakwepa kuwajibika? Mbowe angestaafu vipi kwa heshima wakati mlimwandama kwa kejeli na matusi? Angestaafu si ndio mngezidi kumbeza kuwa amewaogopa? Pamoja na matusi na mbinu chafu Mbowe aliwezesha uchaguzi ufanyike kwa uwazi na weledi mkubwa. Aliposhindwa akaaga akaenda zake na Mwenyekiti Mpya akamwambia apumzike na achukue likizo.

Uongozi mpya ndio walikuwa na uwezo wa kuunganisha chama sio Mbowe. Lakini badala ya kufanya hivyo wakaendekeza siasa ya visasi na kuwatenga wale ambao waliamini wako bado upande wa Mbowe. Ulikuwa ndio wakati wa kutamba warriors wa social media ambao furaha yao ilikuwa kwenye mzodoa na kumbeza Mbowe na wale ambao waliamini kuwa ni timu yake. Uongozi wa Chadema haukuwakemea, ukaweka pamba masikioni. Walikaa kimya hata pale kiongozi mmoja alipopigwa na walikataa hata kwenda kumuona. Matokeo ya yote hayo ni wakina Mrema kuamua hamna sababu ya kung'ang'ania chama ambachl hakiwataki. Uongozi wa sasa wakasema good riddance na mpaka leo wanaendelea kuwasema kwenye majukwaa yao. Sasa hivi adui mkubwa wa Chadema amekuwa ni Chaumma, sio CCM.

Yanayoendelea Chadema ni matokeo ya uongozi mpya na sio mtu mwingine. Pambanieni hali yenu, muacheni Mbowe aendelee kupumzika.

Amandla...
 

Sisi waTanganyika tunayajua haya
 

Attachments

  • downloadfile-114.png
    742.9 KB · Views: 20
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…