Kesi ya Lissu Septemba 10, 2026: IGP Wambura, DCI Kingai na CDF Mkunda waitwa kutoa ushahidi

Kaka usijali uyo uwakika anajiweza
 

..sio rahisi.

..wakili wa serikali atakuwa anapotoka akijaribu kutengeneza mazingira kwamba TL alitaka kufanya uhaini kwa kushirikiana na wazee wastaafu, viongozi wa Dini, jukwaa la wahariri, na taasisi za kutetea haki za binadamu.

..hoja ya Upande wa mashtaka itakuwa ni kwamba TL ni mtu ambaye amepitia changamoto fulani na serikali, ana chuki nayo, hivyo alitaka kuipindua.
 
Yeye kazi yake kuleta yanayoendelea Mahakamani, Mimi kazi yangu kuleta Tathimini, wewe kazi yako kunitukana.
Kila mtu na kazi yake, Happy now?
Umeshatuambia kwamba ananyongwa hiyo ndo tathmini yako basi tumekubaliana na wewe. Basi tuache tuendelee kufuatilia kesi. Kila wakati unapost kanyongwa kanyongwa. Basi tumeshakusikia. Kaa pembeni
 
Now we are talking sensible things
 
Umeshatuambia kwamba ananyongwa hiyo ndo tathmini yako basi tumekubaliana na wewe. Basi tuache tuendelee kufuatilia kesi. Kila wakati unapost kanyongwa kanyongwa. Basi tumeshakusikia. Kaa pembeni
Nikuache kwani nimekuoa?
 
Eti nyie ndio chama cha Demokrasia. Hali hii mko nje je mkipata madaraka!
Umeshatuambia kwamba ananyongwa hiyo ndo tathmini yako basi tumekubaliana na wewe. Basi tuache tuendelee kufuatilia kesi. Kila wakati unapost kanyongwa kanyongwa. Basi tumeshakusikia. Kaa pembeni
Mkuu,

Nyie ndio mnawapa airtime!!!

Kaeni kimya msiwajibu piga ignore.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 14.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo uliwaeleza Wadau kuhusu kuhamasisha kuupinga Uchaguzi ujao.

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti aliwaeleza Wadau wote kwamba kila mtu kwa nafasi yake.

Lissu: Umesikia swali langu?

Nimesema mazungumzo yangu (mimi) juu ya kuhamasisha watu kupinga huo Uchaguzi ikiwa unakuja 2025.

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Lissu aliwaeleza Wadau kuwa tutaendelea kupinga Uchaguzi ujao kwa njia ya mikutano ya hadhara.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu kuhamasisha uasi wa Watanzania dhidi ya mfumo wetu huu wa Uchaguzi.

Heche: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu vizuri katika hilo jambo.

Labda arudie.

Heche: Hakuna exactly sehemu aliyosema kuhusu uasi, neno uasi kama uasi hakulitumia neno hilo.

Lakini mwisho wa siku alimaanisha kupinga mfumo huu.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu kuzungumzia neno “nitahamasisha umma kuzuia Uchaguzi.”

Heche: Ndiyo Waheshimiwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako na kumbukumbu zako, ukulinisikia nikisema “tutahakikisha Uchaguzi haufanyiki” kwa Wadau hao.

Na maneno hayo nimeshitakiwa nayo.

Heche: Ndiyo Waheshimiwa Majaji.

Alisema Uchaguzi huu unastahili kuvurugwa kwa sababu siyo huru na haki.

Lissu: Siyo unastahili kuvurugwa, bali tutauvuruga.

Heche: Ndiyo Waheshimiwa Majaji, alisema tutauvuruga.

Nassoro Katuga: Ile tafsiri yake kwamba Leading Question ni lile linalo-suggest jibu la “NDIYO.”

Sasa aseme yeye kama jibu hilo linahitaji kuwa sehemu ya ushahidi.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, swali langu siyo Leading Question, ila jibu “ndiyo” lina tatizo.

Epuka majibu ya “ndiyo”, na mimi sijakuuliza useme ndiyo au hapana.

Jaji Ndunguru: Shahidi, umesikia?

Heche: Ndiyo, nimesikia.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, ni lini tulitumia neno “tutakinukisha?”

Heche: Sijawahi kusikia sehemu ukisema “tutakinukisha.”

Lissu: Katika kikao cha Wadau, waeleze Waheshimiwa Majaji kuhusu ugawaji wa majimbo bila kuzingatia idadi ya watu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, ni kweli alieleza kuhusu ugawaji wa majimbo bila uwiano.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nini kuhusu kuzungumzia uteuzi na engua-engua ya wapinzani.

Job Mrema: Naona Mshtakiwa Tundu Lissu, kama amechoka, ndiyo maana tatizo la maswali limekuwa linajirudia-rudia.

Jaji Ndunguru: Umesikia hoja ya upande wa mashitaka?

Lissu: Sijachoka, wacha nirudie swali.

Anachosema Wakili wa Mashitaka ni kwamba nimuache shahidi ajisemee bila kumuongoza.

Wajibu wangu ni kuhakikisha shahidi haendi nje.

Nimemueleza Shahidi kuna mambo yamezungumziwa hapa Mahakamani.

Kwa utaratibu huo, Waheshimiwa Majaji, hakuna Leading Question hapo, Waheshimiwa Majaji.

Na siyo kwa sababu nimechoka. Nikichoka nitakuwa wa kwanza kueleza.

Ni hayo, Waheshimiwa Majaji.

Jaji Ndunguru: Naomba urudie hilo swali.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo nilizungumzia kuhusu engua-engua ya Wagombea wetu.

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alieleza Wadau namna ambavyo Wagombea wetu walienguliwa kwa wingi, akitolea mfano Uchaguzi wa 2020 ambao ulivunja rekodi ya Wagombea wa Udiwani na Ubunge walivyoenguliwa.

Alitolea mfano Jimbo la Mlimba, alipokuwa anagombea Suzan Kiwanga.

Alizungumzia pia Uchaguzi wa Serikali za Mitaa ambapo Wagombea wa CHADEMA asilimia 80 ya Wagombea walienguliwa.

Waheshimiwa, ninaposema Serikali za Mitaa, ni Mitaa mijini na Vijiji na Vitongoji kwa Vijijini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nilizungumzia nini kuhusu Uchaguzi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza namna kampeni za Wagombea zinavyozuiliwa.

Wagombea wa CHADEMA kuzuiliwa kufanya kampeni, kusimamishwa kufanya kampeni.

Ratiba za Wagombea zinavyoingiliwa.

Vyombo vya habari kutokutoa nafasi sawa.

Vyombo vya umma na binafsi kufanya upendeleo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo nilizungumzia kuhusu Kamati za Maadili.

Heche: Waheshimiwa Majaji, alizungumzia kuhusu Kamati za Maadili zinavyozuia CHADEMA kufanya kampeni zao vizuri na kwa uhuru.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN HECHE MAHAKAMANI

SEHEMU YA 15.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji kwenye mikutano hiyo na Wadau nilisema nini kuhusu Mawakala wa Wagombea na Mawakala wao.

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alieleza jinsi ambavyo Mawakala wa Wagombea wanavyozuiliwa nje katika zoezi la upigaji kura huku mchakato wa Uchaguzi unaendelea.

Alisema utaratibu wa Mawakala ni mbovu, unalenga kuzuia CHADEMA kuwa na Mawakala.

Lissu: Nilisema nini juu ya jinsi inavyofanyika siku ya kupiga kura?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza kwa undani namna ambavyo zoezi la kupiga kura linavyovurugwa na Wasimamizi kuharibu Uchaguzi, kura feki kuingizwa kwenye vituo vya kupiga kura, Wagombea ambao siyo halali kutangazwa wameshinda na hawakushinda.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini kwa Wadau kuhusu utaratibu wa kupinga matokeo Mahakamani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza namna ambavyo ni vigumu kupinga matokeo Mahakamani.

Kwanza, kama umeenguliwa huwezi kwenda Mahakamani kama wamekuengua.

Unatakiwa urudi kwa hiyo hiyo Tume ya Uchaguzi, na wakitoa maamuzi yao hayapingwi.

Kwa hiyo, kama umeenguliwa hata kimakosa, unakuwa umepoteza haki yako, huwezi kuidai.

Vilevile, kama ulikuwa Mgombea unahitaji kukata rufaa, huruhusiwi kwenda Mahakamani.

Lakini pia, kama huna kiasi cha fedha kama bond, huruhusiwi kufungua kesi bila kiasi hicho cha fedha.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini juu ya kupinga matokeo ya Urais Mahakamani?

Heche: Waheshimiwa Majaji, Mheshimiwa Tundu Lissu alieleza kwamba huwezi kupinga matokeo ya Urais, hata kama hajachaguliwa.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji nilisema nini juu ya Wananchi ambao siyo wanachama wa Vyama kugombea uongozi?

Heche: Waheshimiwa Majaji, alieleza kuwa mtu au Mgombea huru hana nafasi ya kugombea.

Kama unataka uongozi, lazima upitie kwenye chama cha siasa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
nitahamasisha umma kuzuia Uchaguzi "tutauvuruga."


Hapa Heche Jamhuri ya Muungano inafurahi sana, kwa kuisaidia kutenda haki
 
Chain yako imeruka baadhi ya process, kumbuka mnyika alieleza mbele ya mahakama kwamba walipeleka mapendekezo yao ya mabadiriko ya sheria ya uchaguzi mbelw ya kamati ya kudumu ya bunge ya utawala, katiba na sheria.

Then wakafungua kesi mwisho mahakama ikasema maswala ya kisiasa yaamuliwe kwa njia za demokrasia ya kisiasa.

Chadema ikatangaza "No Reform, No Election", ikiwa ndio miongoni mwa njia za kidemokrasia ya kisiasa, Then hapo sasa ndipo Chain of Prosecution inaweza kuendelea kinyume na hapo.

Tathmini yako ni yenye kuegemea upande mmoja kiasi kuathili ukweli wa mambo.
 
Ndio maana nasema tusubiri majibu ya Heche kama atabanwa Hilo swali
 
 

Attachments

  • Yeriko.png
    1.8 MB · Views: 12
  • Screenshot_20250903-155409.jpg
    115.5 KB · Views: 11
  • 6185098-34c7b9f4eee53e3e336141c880c2b9c1.mp4
    7.3 MB
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…