Sisi ndiyo wanaume wa kweli hatuishi kwa kukariri kama nyie. Tunaita koleo kwa jina lake na hatuiiti Kijiko kikubwa. Unataka niwe na msimamo wa kumtetea Mbowe na UJINGA wake.? Na hapo ndipo mnapokosea wana CHADEMA kwa kuwa kiuhalisia Chama chenu ni mali ya Mbowe na mkwewe Edwin Mtei, hakuna mwenye ujasiri wa kumshauri wala kumuonya.
Laiti mngenguwa na UHURU wa kumkosoa na kumshauri ilikuwa mumwambie aachane na PAPARA za kiuanaharakati, asome mchezo kwanza wa awamu ya 6, ndipo mjue mnakabiliana vipi na Serikali ya haiba ya Rais Samia
Nakuletea hapa uzi wangu niliandika kumtahadharisha kabla hajakamatwa.
Kwako Freeman Mbowe, Mwenyekiti wa CHADEMA Ni wazi CDM mnapoteza focus maana Kama alivyosema E Lowassa mwaka 2015 kuwa Chama chenu ni wana harakati zaidi kuliko wanasiasa. Wanaharakati huenda na matukio wakati wanasiasa huenda na mikakati. Kuna mabadiliko makubwa ya kisiasa, kijamii na...