Kesi ya Mbowe na Wenzake: Polisi Wazuia watu kuingia kufuatilia, Mawakili wa Utetezi watoka nje. Kesi yarejea na kuahirishwa mpaka 17 Sept
CHADEMA Tanzania (@ChademaTz) Tweeted:
Wananchi wakiwa nje ya Mahakama Kuu Division ya Uhujumu Uchumi na Rushwa baada ya kuzuiwa kuingia ndani ya Mahakama na Jeshi la Polisi, ambapo leo Sept. 16, 2021 shahidi wa kwanza Kamanda wa Polisi Mkoa wa Kipolisi wa KinondonI ACP Ramadhani Kingai ataendelea kutoa ushahidi wake. https://t.co/B0ORcpvcfi
 
Freeman Mbowe na wenzake wameletwa tayari. Lakini ulinzi mkali umeimarishwa. Askari wengi. Pia kuna zuio la watu kuingia ndani ya mahakama. Wanasema ni mawakili 20 tu, wanahabari 10 (leo wameruhusiwa), ndugu 5, Viongozi 5, lakini simu marufuku.

Askari magereza wanalalamika kwamba jana tumefanya ujinga sana. Ujinga gani, tunawaukliza, wanasema tulikuwa tunatuma habari nje. Wanamueleza Benson Kigaila, NKM CHADEMA. Tumewaeleza kwamba, anayetakiwa kulalamika ni Jaji sio wao. Mahakama siyo gereza. Wajishikilie vizuri.

Mahakama imechelewa kwa dakika 40, yote hii ni kutokana na Jamhuri kutaka kuhodhi mamlaka ya mahakama, bila kujua kwamba wote hapa tuna interest na kesi hii, wao ni walalamikaji, sisi ni watuhumiwa. Kwanini watuzuie kuingia mahakamani na simu?

Watoto wote wa Freeman Mbowe, (Nicole na Dudley) pia wapo nje ya mahakama, pamoja na ndugu zao wengine.

Kama kawaida yao, makarao waliovalia kiraia, wamekaa kwenye siti karibu zote za mahakama, wamechukua nafasi kama kesi ni yao pekee yao.

Mambo ya ajabu yanafanyika

Lakini kitu cha muhimu hadi sasa ndugu zangu ni kwamba, kwa umoja wetu wote tupo nje ya mahakama kuu Divisheni ya makosa ya uhujumu uchumi na Rushwa, Ubungo-Mawasiliano, tumeshawaelekeza MAWAKILI wetu wasomi kwamba "No ENTRANCE NO CASE"... And it's done, hii ni open court!

Updates
Jana Jaji Mustapha Siyani alisema watuhumiwa waletwe mapema, saa 3 asubuhi kesi ianze, lakini mpaka saa 5 na Dakika 24 sasa kesi haijaanza kwa sababu ya polisi kuzuia watu. Mawakili wetu walikwenda kumuona Jaji, wanatupa taarifa kwamba Jaji amekana kuzia Jambo hilo mahakamani.

C&P Martin

Mbowe Ni Raisi 2025
 
Braza una mjibu mtu ambaye hata kuandika kwa usahihi hajui?
Huyo uzi mmoja anaweza comment mara 10 hata kama hakuna aliye mu quote
tulieni dawa iwaingie mashoga wa jf nyie waacheni wanaume waongee
 
Hamna kazi za kufanya kazi yenu ni kukaa mahakamani siku nzima kufuatilia kesi ya Mbowe????

Anyway, kuna kitu watu wengi hawajui. Gaidi siyo lazima awe anamiliki AK47 au M16 Rifle au mabomu.
Gaidi anaweza akawa na kisu tu na akafanya ugaidi. Gaidi anaweza akawa na "ideology" tu kichwani na akafanya ugaidi.

By the way sisemi Mbowe ni gaidi, hapana. Kwa sasa hivi Mbowe is innocent until proven guilty.

Time will tell.
Hamza mli prove wapi Ni gaidi?
 
Baada ya Jana jamii kupata habari ya kila kilichotokea Mahakamani kwa ufasaha bila kupindisha Leo jeshi la Polisi limedhibiti uingiaji Mahakamani pamoja na kuzuia matumizi ya simu. Sababu zakufanya hivyo hazijawekwa wazi. Ikumbukwe ACP Ramadhani Kingai ambaye ni mkuu wa Polisi Kinondoni leo anaendelea kuhojiwa katika kesi ndogo iliyoibuka kutoka kesi ya msingi.

Wakati jana anahojiwa kuhusu uwepo wake Mahakamani hapo Mara kwa mara kesi hii inapokuwa inasikilizwa alikiri kuwa anafika Mahakamani hapo na kwa mazingira haya yeye akiwa ni shahidi pia yeye ndiyo kiongozi wa Askari kwa eneo hili la mahakama na hivyo yawezekana baada ya Jana kuona Hali ya utata na maswali yaliyoibuka Mahakamani Leo hii amejiwekea ulinzi kuepusha taarifa za ushahidi wake kutokufika kwa jamii.

Hali hii imelalamikiwa muda mrefu na tatizo halijawekwa wazi kwamba serikali ndiyo inafanya haya au mahakama yenyewe ndiyo imeamua kutokuonekana matendo yake kwa wananchi. Katika ulimwengu wa Sasa nchi nyingi Duniani zimeruhusu live cavarage Mahakamani tofauti na Tanzania ambapo hata waandishi wa habari wanaoruhusiwa kuingia mahakamani ni wale tu ambao Jamhuri inaamini wataripoti kile ambacho wao wanataka.

Mfano mzuri ni tukio la Jana ambalo hakuna chombo Cha habari kilichokuwa mahakamani kiliweza kuweka updates ya kinachoendelea mahakamani. Vyombo vyote vilikaa kimya isipokuwa JF na Kurasa za tweeter.

Mahakama kwa mwendo huu inaonyesha wazi kwamba siyo chombo huru, vinginevyo itoe tamko kwa dola kuruhusu watu kuingia kulingana na ukubwa wa ukumbi wa mahakama na ikumbukwe hakuna sheria inayokataza kesi kuripotiwa moja kwa moja kwa wananchi.
I hope Mkuu Mwala atakuwepotema kutuletea dondoo za mwenendonwa kesi kama ilivyokuwa jana
 
Hii kesi kama ikiachwa iendelee inakwenda kumwaibisha mtu.. hii kesi ni ya kuachana nayo haraka ili tusonge mbele kama taifa. Tunatakiwa kuanza mapema kumalizia mchakato wa katiba mpya ili kabla ya 2023 iwe tayari na tuanze kujiandaa kwa 2025.
 
Nimeshtushwa sana na hawa polisi wetu ambao wanalalamikiwa kila kona ya nchi kwa kupora haki za watu, sasa wanazuia watu kuingia mahakamani na simu zao ni utaratibu wapi huu na umeanza lini? Mnataka kuficha kitu gani? Kwani hii ni mahakama ya kijeshi?

Kuweni current acheni mambo ya Kizamani, ICC yenyewe inahoji mashahidi mahakaman wazi wazi mpaka inafanya maamuzi. Kwanini mnaficha? Mkiambiwa mnatumoka kisiasa mnasema jamii haiwapemdi
 
Back
Top Bottom