Leo shahidi wa sita naye kapita na mazaga zaga yake kama yale yale, ya wale wa awali.
Shahidi huyu anadai alipata barua ikimtaka kukagua silaha kama ilikuwa imesajiliwa nchini 25/11/2020. Akaijibu barua hiyo 15/3/2021, miezi 5 baadaye.
Maajabu yapate vipi kukoma?
Tumeona hukumu zikitolewa katika hatua mbali mbali za shauri hili.
Tumeona Hati ya Mashtaka ikibadilishwa ndani ya shauri. Tumeona na mengi mengine.
Siyo siri kuwa pana ukakasi wa kutosha unaoligubika shauri hili.
View attachment 1998796
Ukweli ni pumzi ya wapenda haki.
Maisha ya wenye haki yako mashakani kutokana na idadi ya waongo kuongezeka kila kukicha.
Hata hivyo yote kheri kwani ukweli utaendelea kuwa ukweli.