Kesi ya Mbowe Novemba 4, 2021: Mrakibu Mwandamizi wa Jeshi la Polisi, Sebastian Madembwe atoa ushahidi. Kesi yaahirishwa hadi Novemba 5, 2021

Mie natoa maoni yangu huenda yakafika mbali.
kwanza hii kuulizwa kabila ifutwe na badala yake aulizwe kalazaliwa wapi. na ni raia wawapi. Au kapataje uraia wake.
pili anataka kula kiapo kwa kutumia kitabu kipi.
 
Point 3 muhimu.
 
Hawa jamaa sijui waliandikaje hii script... miezi yote hiyo wamekaa nayo ila details zinagoma... gaps kibao.

Sasa hata kama mnataka Mbowe afungwe jamani, Mahakama haiwezi mfunga mtu Mifungo cha Maisha kwa ushahidi kama huu ni ngumu mno, mno.
 
Najaribu ku track mwenendo wa huyu Jaji sijapenda. Anaanza kunipaashaka Sana. Huyu si mwema hata kidogo. Ana lake Jambo naliona
Huyu anaweza kuwa mzuri kuliko Mustapha Siyani...

Maana yule Siyani, alisifiwa kuwa ni mzuri na anajali haki za binadamu kwa kuwa tu alikuwa anahimiza washitakiwa kupewa maji ya kunywa mara kwa mara...

Lakini mwisho wa siku, kila mtu aliona kumbe yule ni kicheche ambaye hupanua kinyeo chake, na kuku hudanganyika kudhani ni mnofu wa nyama...

La haula, wakilogwa apeleke kichwa chake kudonoa nyama hiyo, masikini, inakuwa ndiyo mwisho wake...

Nisemacho ni hiki; HERI MWANZO MBAYA LAKINI UKAMALIZA NA MWISHO MWEMA...

Let's continue giving him the benefit of doubt kwamba tutakuwa na mwisho mwema..
 
Hii kesi kwa kusoma ni sawa na kusoma lyrics za nyimbo ukijua kwamba unasikiliza muziki...

Kuna vingi tunavikosa, maandishi hayawezi tuonyesha body language za wahusika , kutetemeka, vigugumizi n.k

Inasikitisha sana...

Kinachokusikitisha ni nini ndugu yangu?

Hilo liko wazi kabisa kuwa ukiwa physically palepale mahakamani au kuangalia kwenye TV unaona vyote...

Lakini reporting ya kutumia kalamu haiwezi kuchukua mengine...

Lakini tuwape pongezi waliojitolea kutupa yajiriyo huko mahakamani ktk kesi hi kwa njia ya kalamu na kusaidiwa kusambazwa na social medias. Pongezi kwa JF, Twitter na Instagram maana ndizo hasa zinazosambaza taarifa kwa haraka na wepesi....

Tunakosa mengine, lakini the basic infos tunazipata. Maana hata mimi wa Shinyanga naelewa nini kumeendelea DSM...!

Mimi nadhani ushukuru kwa hili ingalau badala ya kusikitika...!!

NB: Niwahakikishie watu kuwa, kesi hii inafuatiliwa na watu wengi sana hadi vijijini ili mradi mtu ana simu...
 
Wamfunge tu mbona ushahidi wa jamhuru umeenyooka hivyo. Kuliko hata ule wa Sabaya wa kuunga unga naa gundi. Kama hii kesi ni ya uwongo niamini kesi ya namna gani. Technologia aidanganyi bhana.

Mnasumbua tu mahakana.
Ufungwe wewe na mamako
 
====================

Jaji ameingia..

Kesi namba 16 ya Mwaka 2021 Khalfani Bwire na Wenzie imetajwa

Jaji: Wakili wa Mshtakiwa wa kwanza

Mtobesya: Shahidi Unakumbuka Ushawahi Kuandika Maelezo Polisi

Shahidi: Nakumbuka


Mtobesya: Unakumbuka Uliyasoma Maelezo Yako na Ukahakikisha Kwamba ni sahihi

Mtobesya: Unakumbuka Uliandika Siku gani ya Tarehe Ngapi Mwezi na Mwaka

Shahidi: 20 Mwezi 03 Mwaka 2021

Mtobesya: Kuanzia wakati huo Mpaka Sasa ni Muda gani umepita?

Shahidi: Miezi Saba


Mtobesya: Nitakuwa sahihi nikisema wakati Unaandika Memory Yako ilikuwa sahihi wakati unaandika Maelezo yako ulikuwa Umesha andika Barua Iliyopokelewa Kama Kielelezo Namba 10?

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Uliongelea pia Kuhusu hiyo Barua

Shahidi: Rudia Swali tafadhali


Mtobesya: Kwenye Maelezo Yako Unakumbuka Uliongelea Barua Uliyoitoa, Lakini hukukumbuka Wakati Ule kama Ulikosea Jalada Namba Umekuja Kukumbuka Leo?

Shahidi: Kwenye Maelezo Yangu nilikuwa nimesimamia kazi ya kile nilichokifanya Kuhusu Uchunguzi Enheeeeeeee..


Mtobesya: Malizie hiyo Enheeeeeee

Shahidi: Sikuiangalia

Mtobesya: Barua yenye Matatizo ya Kiuandishi ndiyo hiyo hiyo ulikuwa unaielezea

Shahidi: Tatizo la Kiuandishi lilikuwa Kwenye Jalada


Mtobesya: Ndiyo nakuuliza sasa Barua yenye Matatizo ya Kiuandishi Ndiyo hiyo uliyoifanyia Uchunguzi

Shahidi: Sahihi

Mtobesya: Ulitaja Mapungufu ya Barua yako

Shahidi: Sikumbuki Kama nilitaja

Mtobesya: Mheshimiwa Naomba Original Statement ya Shahidi aweze Ku' refresh Memory


Mawakili wa Serikali Wanaitafuta Bado

Mtobesya: anampatia Shahidi

Mtobesya: angalia Kama haya Ndiyo Maelezo ya Kwako Uliyoyaandika Polisi Kama ni ya Kwako kwa Mujibu wa Kesi hii

Shahidi: Ndiyo yenyewe


Mtobesya: Soma yote kwa Sauti ilituone Kama Kuna sehemu Uliomba Kurekebisha

Jaji: Sorry Kwani alisema yeye aliandika?

Mtobesya: alisema Hakumbuki

Nimemwambia asome tusikie Kama alisema. Unless kama Mahakama ina maoni tofauti aseme Hakuna tuishie hapo


Jaji: anaposema hakumbuki, naona ungem' lead labda, Kusema asome statement Yote naona Mhhhh Sijui lakini

Shahidi: Kwenye Maelezo CD IR 2097 2020

Mtobesya: Unasoma Wapi

Shahidi: Juu kabisa

Mtobesya: Tupo Chini hapo Ndiyo kwenye Content yako

Shahidi: Hakuna Sehemu niliyoandika


Mtobesya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Kwamba Katika Maelezo Yako hiyo Kumbukumbu namba

Shahidi: Nakumbuka ilikuwa 15 March 2021 Baadae nikaja Kuandika Maelezo, kwa hiyo Makosa ya Kibinadamu tu

Mtobesya: Kwa hiyo Kipengele hicho kwenye Maelezo yako kipo au Hakipo

Shahidi: Hakipo


Mtobesya: Umesema Ulifanya kazi Kwa Kutumia Mfumo, Je uliweza Ku' Demonstrate namna huo Mfumo unafanya Kazi

Shahidi: Issue ya Kuwaita watu ili waweze Kushuhudia ninachokifanya ni suala lingine

Mtobesya: Je Uliwahi Kufanya?

Shahidi: Ndiyo Mara yangu ya kwanza


Jaji: Kuna sehemu hamuelewani naona

Mtobesya: labda Nirudie Swali

Ulionyesha Wakati Unaelekezwa na Wakili wa Serikali namna Mfumo unavyofanya kazi

Shahidi: Sikuonyesha


Ni mallya anasimama


Mtobesya amemaliza, anaketi, anasimama John Mallya

Mallya: Dhumuni la Usajili wa Silaha ni Kudhibiti Silaha isifanye Uhalifu

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo wewe Ulipewa silaha Kuchunguza ni Rahisi Kujua Kama ilifanya Uhalifu

Shahidi: Mie naletewa Kuchunguza Silaha ni ya nani

Mallya: Sasa ulisema Hapa Mahakamani Leo kuwa Results ni No Records?

Shahidi anatoa Macho tu hajibu swali, anashangaa

Mallya: Mheshimiwa Jaji nasubiri Jibu

Shahidi: nilicho present Leo ndiyo kilichokuwepo

Mallya: Kwa hiyo umeleta au hujakileta

Shahidi: Hakipo


Mallya: Umeingia Polisi Ukiwa na Miaka 24

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo unauzoefu Wa Miaka zaidi ya 20

Shahidi: Ndiyo

Mallya: hiko Kitengo Unamuda nacho gani

Shahidi: Miaka 20

Mallya: Ulipata Kujua hiyo silaha imepatikana wapi

Shahidi: hiyo siyo Kazi yangu


Mallya: Kwa hiyo wewe unatolea Majibu ya Uchunguzi Silaha iliyosajiwa tu?

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Ulizungumzia Ufanisi wa huo Mfumo wakati unaongozwa

Shahidi: Data base Ipo Vizuri na ina Speed

Mallya: Ulizungumzia hilo suala

Shahidi: Sikuzungumzia


Mallya: Nilikusikia Kwamba Ukibonyeza Save, huwezi Kufuta bila Ruhusa ya Admin

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Je Kama hukueleza Admin Ndiyo Mwenye Mandate Vipi Kama Admin Alibadilisha umiliki wa Silaha Ya Kingai aweze Kumbambikia Mtu

Shahidi: Adimn hana Mandate ya Moja Kwa Moja


Mallya: Sasa Unabadili Ushahidi Wako?

Shahidi: Hapana Kuna mambo Sikuulizwa

Mallya: Je ulielezea namna Admin anavyotoa ruhusa

Shahidi: Sikueleza

Mallya: Ulisema Pia Kuna Taarifa Unazitumia katikati, Je ulipata Mazingira ya Serial Namba Kufuta na wahalifu

Shahidi: Ni sahihi


Mallya: Mwambie Mheshimiwa Jaji Sasa Namna kama hiyo inaweza kujitokeza

Shahidi: Endapo Parameters Zimefutwa tunashirikiana na watu wa Ballistic

Mallya: Kwa hiyo tunakubaliana Parameters Zako siyo Kitu Pekee cha kutambua Silaha

Shahidi: Ndiyo


Mallya: Kwa hiyo Ulielezea wakati Unaulizwa

Shahidi: Hapana Sikueleza

Mallya: umewahi Kupata Mazingira ambapo namba imefojiwa kutoka namba 04 kwenda namba 07

Shahidi: Unajua kwa Mazingira yangu

Mallya: Jibu swali Shahidi

Shahidi: Issue za Ku temper hatujazishuhudia

Mallya: Ulieleza Kwamba Uliletewa Barua tu siyo Bastola

Shahidi: Ndiyo

Mallya: Kwa hiyo Ujajisumbua Kama namba ulizo letewa zilikuwa tempered

Shahidi: Siyo Jukumu langu

Mallya: Unafanya Kazi Siku Ngapi katika wiki

Shahidi: Maasa 24 kwa Siku Saba


Fedrick Kihwelo sasa


Fredrick Kihwelo: Ni kweli tarehe 25 ulipokea Barua Kutoka kwa ASP Msangi

Shahidi: Ndiyo nilipokea

Fredrick: Mpo wangapi Kwenye hicho Kitengo

Shahidi: Tupo 20

Fredrick: Barua ya ASP Msangi Ilikuwa inakutaka Ufanye nini

Shahidi: Kutoa Majibu ya Umiliki


Fredrick: Wewe Ulitoa Taarifa ya Umiliki au Uchunguzi

Shahidi: Nilifanya Uchunguzi nikatoa Taarifa ya Umiliki

Fredrick: Barua Yako ya majibu ni ya Uchunguzi au Umiliki

Shahidi: Umiliki

Fredrick: Ni sahihi Mnafanyia Uchunguzi Siku hiyo hiyo Mnapopokea Barua

Shahidi: Ndiyo


Fredrick: Wewe Ulipokea Barua Siku gani 25 /11/2020, ukatoa majibu lini?

Shahidi: 15 March 2021

Fredrick: Ni Muda gani umepita

Shahidi: Miezi 05

Fredrick: Je Katika Majukumu yako ulitaja Jukumu lako la Kutaja Umiliki

Shahidi: Hapana


Fredrick: Ni kweli Kuna Njia 2 za Kumiliki Silaha?

Shahidi: swali sijaelewa

Fredrick: Katika Maelezo Yako ulisema Mtu anaweza Kumiliki Silaha Kwa Njia ya Kuingiza ndani ya Nchi, Kununua Ndani ya Nchi na Kama amerithi, Sasa Nakuuliza Je kuna namna Mbili tu za Kumiliki Silaha


Shahidi: Si kweli

Fredrick Kihwelo anaketi na anasimama Peter Kibatala


Kibatala: Kielelezo Cha Mashtaka namba 10 umetaja Barua ya Tarehe 25 Nov Mwaka 2020 aje ni sahihi Kwamba Barua hii Ndiyo Chanzo Chote cha wewe Kuandika Barua

Shahidi: Sahihi

Kibatala: Ni sahihi Kwamba bila Barua hiyo wewe Usingeandika hiyo Barua

Shahidi: Ndiyo sahihi Kabisa

Kibatala: Siyo Kawaida yako kuandika tu barua

Shahidi: itakuwa Kinyume na kazi.

Kibatala: Je hiyo Barua iliyokufanya Uandike Barua Umekuja nayo?

Shahidi: Si kuja nayo Lazima aionyeshe mahakama msingi wa yeye kuandika hiyo barua si vinginevyo maana yake atakuwa ameitunga tu

Kibatala: kwa Ufahamu wako wewe ni Muhimu au Siyo Muhimu

Shahidi: kwa Upande wangu sikuona Umuhimu wa Kuja nayo

Kibatala: na Kwa hiyo Barua ndimo ambapo tungepata Details za Hiyo Bunduki ambayo wewe Ulipswa Uifanyie Uchunguzi

Shahidi: Sahihi Kabisa


Kibatala: na Ndiyo humo tungeona Namba CZ 100,Callibre 9mm hatuwezi Kuona Popote zaidi ya hiyo Barua

Shahidi: Sahihi kabisa

Kibatala: hujazungumza kabisa Kuhusu CZ 100 9MM za Ulikuwa unachunguza kwenye hiyo Barua Uliyoandikiwa

Shahidi: Sahihi Kabisa


Kibatala: sahihi Kabisa hujazungumza Kuhusu CZ 100, Callibre 09mm

Shahidi: Sahihi sikuzungumzia

Kibatala: Kuhusu Electronic Data Base Ulizungumza Kuhusu Mmiliki wa Risasi

Shahidi: Kwenye electronic Data Base inaonyesha kuwa Idadi ya Risasi za kutumia wakati wa Uhai wa Leseni


Kibatala: Je Katika huo Mfumo Usajili wa Bunduki na Risasi ni Kitu kimoja au tofauti

Shahidi: Ni Kitu Kimoja

Kibatala: Kwa hiyo Ni kisha Sajiliwa Bunduki naona na Risasi zilizopo..?

Mfano TRA Umiliki wa Gari Unaonyesha na Kiasi cha Mafuta Kilichomo

Shahidi: Hapana


Kibatala: Kwa hiyo Mfano niondoe

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je Risasi zinasajiliwa..?

Shahidi: Hazisajiliwi

Kibatala: Na hujazungumza kuhusu Risasi

Shahidi: Sijazungumza

Kibatala: na wala Kwenye Barua p10 hujazungumza kuhusu Risasi

Shahidi: Ni sahihi Kabisa


Kibatala: Kuna swali umeulizwa kuhusu Umiliki Possession, Je Mtu aki import Bunduki inakwenda Wapi

Shahidi: Lisenced Warehouse

Kibatala: Wewe Katika System Yako Muda huo Inasomeka nini

Shahidi: Muda huo inakuwa haijaingizwa Kwenye Mfumo


Kibatala: Ulisema Chochote a kuwa Inawe zekana Bastola Ile Inaweza Kuwa Imetoka Lisenced Warehouse

Shahidi: Sikusema Chochote

Kibatala: Ulisema hiyo Possibility kwenye hiyo Barua yako

Shahidi: Sikusema


Kibatala: Ulitaka Jaji akusamehe Kwa Makosa ya Kumbukumbu namba, Je ni sahihi Kwamba ili tukusamehe ni lazima marekebisho yako tuangalie Kwenye Barua (mama) ambayo yenyewe ndiyo ina mwaka sahihi

Shahidi: Sahihi Kabisa

Kibatala: Barua hujaitoa Mahakamani

Shahidi: sahihi Kabisa


Kibatala: Kwa hiyo sasa Msamaha wako Unaelea kwa sababu hatuna Control

Shahidi: Ni sahihi kabisa

Kibatala: hii Barua Yako inaonekana Ulikuwa unaipeleka ASP H. MSANGI, Je Kuna Mtu anaitwa Inspector Swila, Je Ulimtaja

Shahidi: Sikumtaja


Kibatala: Kwa hiyo akisema Inspector Swila Kuwa yeye Ndiyo aliyeandika hiyo Barua atakuwa anasema ni Uongo

Shahidi: Mimi nilipewa na ASP H. MSANGI

Kibatala: ASP H. MSANGI Hukum' Adress kwa Bahati Mbaya, Ni Kwa sababu Yeye ndiye alikuandikia Barua Mama, akija Inspector Swila kasema Ulimpelekea Majibu ya Uchunguzi atakuwa Muongo

Shahidi: Mimi Najua ASP H. Msangi

Kibatala: Wakati Unaandika Barua Ofisi yako ilikuwa Chini ya Mkurugenzi ya Makosa ya Jinai

Shahidi: Ndiyo


Kibatala: Ni sahihi wewe na Msangi Mlikuwa Mpo wote Chini ya Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Kama Serial Namba ikichezewa Ikafutwa Je hilo ni Jukumu la nani

Shahidi: Jukumu la Ballistic


Kibatala: Umesema ulipokea Barua Ukagonga Barua na Utaratibu Wa Kupokea Barua lazima Pawe na Kitabu Kama Ili Sajiliwa Kuingia Ofiini kwenu

Shahidi: Ikihitajia nitaileta

Kibatala: Lakini Hapa hujaitoa

Shahidi: Hapa Sijaitoa


Unaileta wapi bwana hatutaki kitu kipya sisi


Kibatala: Ulitoa Maelezo Kwa Jaji kwanini Hiyo Register hukuleta Kama Sababu ni Nzito au Kubwa

Shahidi: Sababu Sikutoa

Kibatala: ulisema kwamba Result ni Negative

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Je ulifafanua Kwa Jaji Kwanini Hukuleta hiyo Negative Results

Shahidi: Sikufafanua


Kesi za kijinga kijinga kabisa si wafute tu


Kibatala: Unafahamu Kwamba Ushahidi Wako Lazima Upitie Sehemu kadhaa, Mahakama lazima Ipime Ushahidi wako

Shahidi: Hiyo nafahamu

Kibatala: Mwambie Sasa Mheshimiwa Jaji Kama Ulifafanua kwanini ulishindwa a kuleta Extract ya Negative Result

Shahidi: Sikufafanua


Kibatala: Nilisikia Kwamba Kuna Typing Error Kwenye P10

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sasa Mahakama Itajuaje Kama Hakuna tena Makosa ya Kibinadamu humu?

Shahidi: Ni Jukumu la Mahakama Sasa Kupima


Kibatala: Kuna Sheria Yoyote au Kanuni yoyote ambayo inasema usilete Barua Mama, Report iwe Inajitegemea

Shahidi: Hakuna

Kibatala Ni wewe tu Uliamua

Shahidi: Kimyaaaaaaaaa

Kibatala: Swali langu la Mwisho


Kibatala: Unakubaliana na Mimi Kuwa hakuna Kosa Linajitegemea Kumiliki Silaha Bila Kibali

Shahidi: Ndiyo

Kibatala: Sheria Inaitwaje

Shahidi: Inaitwa Sheria ya Umiliki na Udhibiti wa silaha Kifungu cha 20

Kibatala: Mheshimiwa Jaji sina Mengine


WS: Shahidi Umeulizwa Maswali Mengi kuhusiana na Barua Mama, Uliposema Hukuona Umuhimu ulimaanisha nini

Shahidi: Ile ilikuwa Inaonyesha Guidance Ya Uchunguzi Ninaopaswa Kufanya

Baada ya Kukamilisha Kwangu Sikuona kama Kuna Ulazima wa Kuleta Ile Barua


WS: Uliona Umuhimu kitu gani

Shahidi: Taarifa ya Uchunguzi

WS: Ieleze Mahakama Ulifanya Kazi Jambo gani

Shahidi: Particulars nilizozitumia Kutoka Kwenye Barua Mama, Ndiyo Key Issues Katika Uchunguzi wa Umiliki wa Silaha


WS: Elezea Kuhusu Tukio la Uhalifu

Kibatala: OBJECTION hayo ni Mambo Mapya

Shahidi: Tunapopokea Taarifa hizo Majibu Kwamba Ni Chanya, Data Base Inaonyesha Silaha Inamilikiwa na Mtu fulani tuna Command Button, Kisha Report Inatoka

Mallya: OBJECTION hiyo ni fact Mpya tunapinga


WS: Mheshimiwa Jaji sijui lakini ni Maoni yetu Kwamba Cross examination ndiyo imeibua Extract Kuhusu Negative Results

Ameulizwa hiyo, Shahidi aachwe aeleze

Kama Wakili angeona siyo Issues Sana alipaswa asiibue

Ni hayo tu, Tunaomba Shahidi ajibu


Kibatala Wakili hakatai Those are Neww matters anajaribu Ku Exclude New Matters

Mtobesya: Mheshimiwa Jaji Sahamani, halafu Hakuongelea Printabiliy ya Negative Results

Jaji: Hoja Mmelewa ya Upande wa Utetezi?

Hapa anakuja na Ufafanuzi Kwamba Siku weza Ku' command



Ila Print na Mimi nakubaliana nao Kwamba hilo ni Jambo Jipya ambalo hakuzungumza na Sasa anataka Kuzungumza

Wakili wa Serikali: Shahidi Nitakuuliza suala hilo hiyo kama Majibu yakiwa Negative guwezi Kuprint, Kwanini sasa!?



Wakili wa Serikali: Shahidi Nitakuuliza suala hilo hilo kama Majibu yakiwa Negative huwezi Kuprint, Kwanini sasa?

Shahidi: Ukikomand ina Print........

Mallya OBJECTION

Kibatala OBJECTION

Mtobesya OBJECTION


Jaji: nafikiri unaweza Kwenda Kwa njia Nyingine

WS: Nilisikia Umeulizwa kuhusu Inspector Swila kwamba Ile Barua Mama Kaandika Nani

Shahidi: ASP H. MSANGI

WS: Kwamba Ile Barua Mliandikiana Wenyewe, Hebu fafanua


Shahidi Ni sahihi Kabisa Kwamba Vitengo Vyote Vipo kwa DCI, Yeye kazi yake ni Kuhakikisha Je tuna Mfumo, linapokuja suala la Kiuchunguzi yeye hausiki tena

Ofisi yangu ya Mrajisi Kama Mtaalamu wa Kufanya Uchunguzi ni Kufanya Uchunguzi Bila Kuingiliwa na Maamuzi au Msukuko wowote wa Mkurugenzi wa Makosa Ya Jinai

WS: Uliulizwa kuhusu forgery, ELEZEA Mahakama Ulichunguza nini

Shahidi: Mimi Sikuletewa Silaha nilichunguza Barua na Particulars Zilizokwepo kwenye Zile Barua zilikuwa ni Key Parameters zilizoniwezesha Mimi Kufanya Uchunguzi



Sasa kama wewe hukuletewa SILAHA na uliletewa BARUA uichunguze kwanini hiyo BARUA uliyoichunguza hukuionyesha mbele ya mahakama ???



WS: Uliulizwa pia kuhusiana na Silaha inayoingizwa Nchini kutoka nje, wewe Maelezo yako hayajaondoa possibility

Shahidi: Mfumo wetu wa Silaha na Usajili, Mfumo wetu Unamuingiza Mwishoni kabisa baada ya silaha Imeshaingia Nchini au Kukamilisha Utaratibu wa malipo



WS: Mheshimiwa Jaji Mimi naishi hapo Kama Kuna Wenzangu waendeleeeee

WS: Wenzangu na wao hawana kitu

Jaji: Shahidi tunakushukuru, unaweza Kuendelea

WS: Ndiye Shahidi Tuliyekuwa naye Leo, Tunaomba Hairisho Hadi Kesho Tuweze Kuendelea na Shahidi Mwingine

Jaji: Upande wa Utetezi


Kibatala: hatuna Pingamizi

Jaji anaandika, Mahakama ipo kimya

Jaji: Maombi yaliyoletwa na mashtaka mahakama inakubali mpaka kesho Saa 3 asubuhi

Upande wa Mashtaka mnaelekezwa kuleta mashahidi. washtakiwa wataendelea kuwa chini ya magereza mpaka kesho
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…