Tuliobahati kufika mahakamani kwa siku chache wakati wa kesi hii tulicheka sana na kujifunza. Picha linaanza anaombwa cheti cha ndoa katoa kumbe ni batili baada ya mahakama kujiridhisha. Ilikua hivi, jina la kanisa feki, pastor feki basi mahakamani ikaomba mshenga, msimamizi wa harusi jibu la Vick eti wooote kwa sasa ni marehemu.
Kwa jitihada za watoto halali wa Mzee wakafanya safari mpaka Sengerema kufika kwenye kanisa husika, kanisa lilkakata kutambua cheti hicho. Pia akafikiwa anaesemekana ndio kafungisha ndoa alirubuniwa majina yake kutumika kama pastor lakini yeye hana taaluma hiyo kabisa.
Ila anamtambua Vick kama jirani na class mate wake tu. Basi mahakama pia ikaomba picha ya harusi yao Vicky anasema zimepotea. Sema wazee marafiku wa Dkt. Likwelile wanasema tangu enzi za uhai wa marehemu alikua anasema Vick kwangu kafata mali na si vinginevyo.
Hivyo aliwachia OG mirathi ambayo imekuja kuwasaidia watoto leo. Dkt. aligawa fei too much sema mdangaji hakuridhika kabisa. Kila MTU alipata chake kabisa. Napenda kuwapongeza wazee wamjini kusaidia watoto wa marehemu hata pale mlipohitajika mliacha safari zenu na kuja mahakamani. Mungu awasimamie na awape maisha marefu mnoo.
Naomba nikutambue Mzee wa msafara, mkuu wa ruti, Mzee wa mjini na marafiki wooote wa marehemu na familia kwa ujumla. Sema Vick anapenda ulozi jamani mpaka nikimuangaliaga nabakia kusema hii ni Hatare na nusu. Full waganga kutoka kwao kanda ya ziwa ogopa mganga hajui kiswahili ni kilugha tu. Lakini leo mahakama imewashinda. Sema watoto wa marehemu acheni uzungu sana.