Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

🔴 Overall: Mnyika ameisaidia Serikali takriban 6/10

Mnyika ameisaidia Serikali kuthibitisha mazingira ya tukio, uwepo wa mkutano, uwepo wa Lissu, baadhi ya maneno, msimamo wa No Reforms No Election, na uwepo wa waandishi.
Sawa Katuga wewe wasema.
 
Ndio, wako mahakamani, hilo nalijua.

Ninaposema ameisaidia Serikali namaanisha ushahidi wake umeipa prosecution baadhi ya vitu vya kuthibitisha: uwepo wa mkutano, Lissu kuwepo na kuzungumza, baadhi ya kauli, msimamo wa No Reforms, No Election na uwepo wa waandishi.

Hiyo haimaanishi Mnyika yuko upande wa Serikali.
Kwa mtazamo wangu, ushahidi huo unaongeza uwezekano wa Lissu kutiwa hatiani, ingawa bado si ushahidi wa kuthibitisha kila kipengele cha shtaka.

Ndiyo maana nikasema 6/10.
Inaonekana hukuwepo tangia hii kesi inaanza. Mbona hayo yote hayabishaniwi. Kinachobishaniwa je Kuna njama za uhaini?
 
Haikuwa hoja kwamba uwepo wa mkutano na Lissu kuwepo haukujulikana.

Hoja yangu ni kwamba Mnyika ame confirm hayo akiwa shahidi wa upande wa utetezi, na pia amethibitisha mambo mengine yanayohusiana na mazingira ya shtaka, ikiwemo baadhi ya kauli na kwamba kulikuwa na nia ya ujumbe kufika kwa umma.

Hivyo nilisema ushahidi wake una baadhi ya vipengele vinavyoweza kutumiwa na prosecution, si kwamba ndiye aliyefanya Serikali ijue Lissu alikuwepo.
Kuna mtu anabisha kwamba mkutano haukuwepo? Wao wanadai Lissu ndio alichapisha maneno, ila kwenye ushahidi jambo ndio waliochapisha na mchapishaji hakualikwa na Lissu alialikwa na Mkutigenzi wa Jambo na mkutano hakuandaliwa na Lissu Bali Katibu Mkuu. Sasa hapo Lissu anaingiaje kama mshatkiwa. Kumbuka kauli ya Ni reform no election haikultwa na Lissu. Fualtilia kesi kwanzia mwanzo
 
Hapo kuna point moja umeisahau, Mnyika mwenyewe amesema wazi kuwa Mkutano wa tarehe 3 Aprili ulikuwa “mkutano wa ndani.” Hivyo si sahihi kuuchukulia kama mkutano wa hadhara wa kuwaelimisha wananchi.

Ndiyo maana suala la waandishi, walialikwaje, walikaa muda gani, nini waliruhusiwa kusikia na kama kulikuwa na nia ya taarifa kufika kwa umma linakuwa relevant kwenye mazingira ya shtaka.

Na nakubaliana na wewe kwamba Mnyika ameimsaidia Lissu kwenye baadhi ya maeneo muhimu hasa aliposema hakusikia neno “Serikali”, hakusikia yote yaliyo kwenye hati ya mashtaka, na kwamba No Reform, No Election yenyewe haina maneno “uasi”, “tutakinukisha” au “kuvuruga uchaguzi”.

Lakini kusema “hajaiachia prosecution chochote” si sahihi. Ame confirm uwepo wa Lissu, kwamba alizungumza, amekiri kusikia baadhi ya kauli zinazotegemewa na prosecution, na amekiri kwamba kulikuwa na nia ya ujumbe wa No Reform, No Election kuwafikia umma.

Kwa hiyo mimi bado nasema ushahidi wake una pande mbili: baadhi unamsaidia Lissu, baadhi unaweza kutumiwa na prosecution.

Ndiyo maana niliweka 6/10, si 10/10.
Hivi ingekuwaje kama angeongea yake maneno bila waandishi wa habari na mtu akamrekodi kwa simu? Si kesi ingekuwa mbaya. Ila aliongea wazi kwenye mkutano bila kificho.
 
Hapo ndipo tunatofautiana. Mimi sijadai Mnyika amethibitisha uhaini. Nimesema ushahidi wake una vipengele vinavyoweza kutumiwa na prosecution.

Ni kweli No Reforms, No Election haikuwa kauli ya Lissu, na Mnyika amesema mkutano uliandaliwa na Sekretarieti.

Lakini pia Mnyika amethibitisha Lissu alikuwepo, alizungumza, alisikia baadhi ya kauli, na kulikuwa na waandishi pamoja na nia ya ujumbe kufika kwa umma. Hivyo swali la mwisho ni prosecution itaweza kuunganisha facts hizo na vipengele vya uhaini? Hapo ndipo kesi inapozunguka.

Ndiyo maana nasema Lissu bado ana hatari ya kutiwa hatiani, si kwamba tayari amethibitishwa na Mnyika.
 
Kwa hivyo issue sio uhaini Tena? Mnahamia kwenye uchochezi. Chagueni kosa kwanza ni uhaini au uchochezi.
 
Hivi ingekuwaje kama angeongea yake maneno bila waandishi wa habari na mtu akamrekodi kwa simu? Si kesi ingekuwa mbaya. Ila aliongea wazi kwenye mkutano bila kificho.
Kuwa alisema wazi mbele ya waandishi hakumaanishi moja kwa moja kwamba ametenda kosa la uhaini. Hapo tunatakiwa kutenganisha mambo mawili; 1 maneno yalisemwa na yalifikishwa kwa umma
2 maneno hayo yanatimiza vipengele vya kisheria vya uhaini.

Point yangu ni kwamba uwepo wa waandishi na nia ya ujumbe kufika kwa umma ni mazingira ambayo prosecution inaweza kuyatumia. Lakini kama maneno yenyewe hayathibitishi vipengele vya uhaini, hapo ndipo prosecution ina kazi kubwa ya kufanya.

Ndiyo maana nasema Mnyika ameisaidia pande zote mbili kwa sehemu.
 
Kwa hivyo issue sio uhaini Tena? Mnahamia kwenye uchochezi. Chagueni kosa kwanza ni uhaini au uchochezi.
Uhaini ndiyo issue, siyo uchochezi. Nimetumia maneno kuunganisha facts na vipengele vya uhaini kwa sababu ndiyo kazi ya prosecution kuthibitisha shtaka lililopo.

Uchochezi sijauingiza kama kosa jipya.

Usichanganye maudhui ya kauli na jina la kosa linaloshtakiwa.
 
Challenging the status quo means questioning existing ways of doing things and actively seeking better approaches for growth and improvement

Sasa Chadema Wanachallenge kweli kweli
 
Hapo kuna point moja umeisahau, Mnyika mwenyewe amesema wazi kuwa Mkutano wa tarehe 3 Aprili ulikuwa “mkutano wa ndani.” Hivyo si sahihi kuuchukulia kama mkutano wa hadhara wa kuwaelimisha wananchi.

Ndiyo maana suala la waandishi, walialikwaje, walikaa muda gani, nini waliruhusiwa kusikia na kama kulikuwa na nia ya taarifa kufika kwa umma linakuwa relevant kwenye mazingira ya shtaka.

Na nakubaliana na wewe kwamba Mnyika ameimsaidia Lissu kwenye baadhi ya maeneo muhimu hasa aliposema hakusikia neno “Serikali”, hakusikia yote yaliyo kwenye hati ya mashtaka, na kwamba No Reform, No Election yenyewe haina maneno “uasi”, “tutakinukisha” au “kuvuruga uchaguzi”.

Lakini kusema “hajaiachia prosecution chochote” si sahihi. Ame confirm uwepo wa Lissu, kwamba alizungumza, amekiri kusikia baadhi ya kauli zinazotegemewa na prosecution, na amekiri kwamba kulikuwa na nia ya ujumbe wa No Reform, No Election kuwafikia umma.

Kwa hiyo mimi bado nasema ushahidi wake una pande mbili: baadhi unamsaidia Lissu, baadhi unaweza kutumiwa na prosecution.

Ndiyo maana niliweka 6/10, si 10/10.
Kwani mkutano wa ndani hauruhusiwi vyombo vya habari?
Mbona ccm huwa wanafanya mikutano yao ya ndani ya halmashauri ya chama na waandishi wanakuwepo..
 
Ubongo wako mdogo kama wa kuku. Mjadala huu upo juu ya uwezo wako
 
Utetezi wa Chadema ni kuwa kilichofanyika ni makubaliano ya vikao halali vya chama na sio maamuzi yake binafsi.

Je chadema wapo tayari kubeba mzigo wa Lisu.

Msajili akifuta kwa matendo yake watamlaumu nani?

..Msajili alishasema no reforms no election haina matatizo yoyote.
 
Sasa wewe unataka u own JF iwe yako. 🤣 🤣 🤣 🤣 Jinga kabisa. Unataka watu wawaze kama wewe. Ni idiot pekee mwenye mawazo kama yako
Umeyasoma wapi hayo, au huo u-president ndio unaokuwezesha kuweka maneno ambayo hukuambiwa mwenyewe?

Hayo ya u-'idiot' nauona mwingi sana ukikuzunguka.
 
Back
Top Bottom