Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Hapo ndipo tunatofautiana. Mimi sijadai Mnyika amethibitisha uhaini. Nimesema ushahidi wake una vipengele vinavyoweza kutumiwa na prosecution.

Ni kweli No Reforms, No Election haikuwa kauli ya Lissu, na Mnyika amesema mkutano uliandaliwa na Sekretarieti.

Lakini pia Mnyika amethibitisha Lissu alikuwepo, alizungumza, alisikia baadhi ya kauli, na kulikuwa na waandishi pamoja na nia ya ujumbe kufika kwa umma. Hivyo swali la mwisho ni prosecution itaweza kuunganisha facts hizo na vipengele vya uhaini? Hapo ndipo kesi inapozunguka.

Ndiyo maana nasema Lissu bado ana hatari ya kutiwa hatiani, si kwamba tayari amethibitishwa na Mnyika.
NIkisema wewe ni layman wa MEMKWA nitakuwa nakosea?
 
Haikuwa hoja kwamba uwepo wa mkutano na Lissu kuwepo haukujulikana.

Hoja yangu ni kwamba Mnyika ame confirm hayo akiwa shahidi wa upande wa utetezi, na pia amethibitisha mambo mengine yanayohusiana na mazingira ya shtaka, ikiwemo baadhi ya kauli na kwamba kulikuwa na nia ya ujumbe kufika kwa umma.

Hivyo nilisema ushahidi wake una baadhi ya vipengele vinavyoweza kutumiwa na prosecution, si kwamba ndiye aliyefanya Serikali ijue Lissu alikuwepo.
Ni hivi, hukumu tayari ipo imeshaandikwa na serekali, hapo wanapoteza muda. Lengo ni kuficha ukweli wa kupora chaguzi na kufanya mauaji, ili ionekane mkosaji ni mwingine. Usitake kuchomekea maelezo ya Mnyika kutaka ionekane ndio ushahidi ulipo wa kesi ya kubambika.
 
Hapo ndipo tunatofautiana. Mimi sijadai Mnyika amethibitisha uhaini. Nimesema ushahidi wake una vipengele vinavyoweza kutumiwa na prosecution.

Ni kweli No Reforms, No Election haikuwa kauli ya Lissu, na Mnyika amesema mkutano uliandaliwa na Sekretarieti.

Lakini pia Mnyika amethibitisha Lissu alikuwepo, alizungumza, alisikia baadhi ya kauli, na kulikuwa na waandishi pamoja na nia ya ujumbe kufika kwa umma. Hivyo swali la mwisho ni prosecution itaweza kuunganisha facts hizo na vipengele vya uhaini? Hapo ndipo kesi inapozunguka.

Ndiyo maana nasema Lissu bado ana hatari ya kutiwa hatiani, si kwamba tayari amethibitishwa na Mnyika.
Kutiwa hatiani atatiwa kwa maelekezo sio kwa ushihidi uliopo kwenye hiyo kesi. Hivyo usionyeshe eti kuna vipengele ambayo ndio mahakama inavingoja na imevipata kwa Mnyika, au ww ndio Katuga umekuja kuhadaa kuwa kuna kitu mahakama inaviona? Yaani hiyo mahakama haioni ushahidi wa uongo wa jamuhuri, ila inaona tu kwenye ushahidi wa Mnyika?🤣
 
Ndio, wako mahakamani, hilo nalijua.

Ninaposema ameisaidia Serikali namaanisha ushahidi wake umeipa prosecution baadhi ya vitu vya kuthibitisha: uwepo wa mkutano, Lissu kuwepo na kuzungumza, baadhi ya kauli, msimamo wa No Reforms, No Election na uwepo wa waandishi.

Hiyo haimaanishi Mnyika yuko upande wa Serikali.
Kwa mtazamo wangu, ushahidi huo unaongeza uwezekano wa Lissu kutiwa hatiani, ingawa bado si ushahidi wa kuthibitisha kila kipengele cha shtaka.

Ndiyo maana nikasema 6/10.
Yaani kwamba kuwepo na mkutano, waandishi wa habari na msimamo wa No reforms, no election ni UHAINI ?

Watu wengi hawajui maana ya UHAINI au viini vyake..

Na ndio maana maneno sijui kuvuruga Uchaguzi,. Kuzuia Uchaguzi sio UHAINI...

Watu wanahitaji Elimu juu ya UHAINI
 
Yaani kwamba kuwepo na mkutano, waandishi wa habari na msimamo wa No reforms, no election ni UHAINI ?

Watu wengi hawajui maana ya UHAINI au viini vyake..

Na ndio maana maneno sijui kuvuruga Uchaguzi,. Kuzuia Uchaguzi sio UHAINI...

Watu wanahitaji Elimu juu ya UHAINI

..kwangu mimi sio uhaini kwasababu hakukuwa na njama au mipango ya kuondoa serikali iliyopo na kusimika serikali nyingine kwa mabavu.
 
Umeanza kuharibu unaposifia Lozari aliyovaa mnyika.Huoni jappkua unatugawa wasomaji kwani sio Kila mtu humu ni mkatoliki au anavaa Lozari.
 
Malisa Godlisten Leo alikuwa safarini kutoka Marekani ambapo amekuwa kwa zaidi ya miezi tisa (9), tangu alipoenda kuiwakilisha nchi yetu kama mtanzania pekee aliyechaguliwa na Wizara ya Mambo ya nje ya Marekani kwenda kupata mafunzo ya uongozi. Fursa ambayo hujitokeza kwa watanzania wachache sana kama ilivyowahi kutokea kwa aliyekuwa Rais wa awamu ya nne Mhe. Jakaya Mrisho Kikwete.

Alipofika Nairobi- Kenya asubuhi ya leo, alishindwa kuendelea na safari kutokana na kuwepo kwa mgomo wa wafanyakazi unaondelea katika uwanja wa ndege wa Kimataifa wa Jomo Kenyatta. Hivyo aliamua kusafiri kwa usafiri binafsi mpaka Namanga ambao ni mpaka kati ya nchi yetu na Kenya ili kuingia nchini kupitia Arusha.

Aliwasili Namanga majira ya saa tisa(9) mchana na kwenda kwa maafisa uhamiaji ili kugongewa hati ya kusafiria (Passport) na hatimaye kuingia nchini kama utaratibu unavyotaka.

Baada ya kufika kwa maafisa uhamiaji hao, walichukua hati yake ya kusafiria na kumwambia kuwa haisomeki kwenye mfumo (system) hivyo wao hawana namna ya kufanya mpaka mkuu wao (in- charge) aje ndio anaweza kuona kwenye mfumo.

Kutokana na kadhia hiyo, na kwa kuwa aliambiwa Mkuu huyo hayupo kwa muda Malisa GJ aliendelea kukaa katika ofisi hizo za uhamiaji akisubiri Mkuu huyo kuja na kuhakikisha tatizo hilo linapatiwa ufumbuzi.

Cha kushangaza ilipofika saa moja jioni, alichukuliwa na gari ambalo si la Polisi jeupe Double Cabin na kupelekwa kituo cha Polisi Longido. Hata hivyo gari hilo halikukaa sana likaondoka kuelekea uelekeo wa Arusha.

Mpaka natoa taarifa hii hakuna taarifa kamili za aliko Malisa GJ na nini ni sababu ya kukamatwa kwake. Aidha simu zake zote zimezimwa tangu alipokuwa anatolewa Namanga.

Nitoe rai kwa Polisi na Uhamiaji kumwachia huru mara moja au kuhakikisha wanatoa taarifa kwa umma za aliko Malisa GJ na sababu ya kukamatwa kwake. Kama haitoshi kuhakikisha anapewa haki zake za kisheria ikiwemo kuonana na mawakili wake na haki ya Mawasiliano.

Dickson Matata (Wakili)
31/8/2026
Arusha-Tanzania.
 

Attachments

  • e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    e773c1bd-d6de-4bec-acb8-a6f6b8fa6d72.jpeg
    72.3 KB · Views: 5
Hao wahuni wasituone watanzania wehu, kusema " NO ELECTION" ni uhaini na kuchochea uasi tayari, we ni nani useme NO ELECTION? We ni tume ya uchaguzi au ni Rais wa nchi? Mamlaka hayo unayatoa wapi km si kwa kuhamasisha uasi na kufanya uhaini? Na kweli walifanikiwa kukinukisha tarehe 29 Oktoba 2025, Samia uwe strong hao wahuni wasikuchezee akili ndiyo waliopanga, kuratibu na kutekeleza yale mauaji.
Hata km atashinda kwa technicality za kisheria awekwe hata kizuizini au afunguliwe mashitakta mengine mauaji
Tafuta kazi ufanye uache uchawa.
 
Back
Top Bottom