Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Kumeanza kupendeza mwaka wa uhaini lazima tukaguane Elimu zetu sio Kitambi kikubwa ukiongea unakunja kunja Uso kumbe kidato hakuna 🤠🤠

Kama namuona Shemeji Heche wasiwasi kibao mana anajua niyeye ndio mlengwa wa
Katuga kazi anayo kutachangamka tu
Wameyataka wenyewe badala ya Maridhiano 🤠🤠🤠🤠🤠
Mnyika alishawahi kuwa "Tanzania One" jikague mwenyewe wewe uliwahi kuwa nani kati ya nafasi kumi za mwanzo kwenye mitihani ya kitaifa.

Historia inaonesha Mnyika aliacha chuo kikuu ili aijenge CHADEMA na siyo kwamba alikosa sifa za kwenda chuo kikuu. Waliosoma naye walishangazwa na uamuzi wake wa kuacha chuo badala yake aende kuijenga CHADEMA.

Sasa mnyika na yule mnayemuita "Dakta" unadhani wanalingana kwa lolote... Mnyika ni msomi.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 18.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba chama cha siasa kusajiliwa lazima kiwe na wafuasi?

MNYIKA: Napata shida kuwasemea, kwa sababu hao wanachama wanaweza kuhama wote.

NASSORO KATUGA: Nauliza kwamba ni sahihi kila chama lazima kiwe na wanachama wake?

MNYIKA: Siwezi kusemea vingine, kwa sababu kuna vyama vya mfukoni; siyo lazima viwe na wanachama kusajiliwa.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba vyama vyote vina itikadi kama CHADEMA?

MNYIKA: Siwezi kusemea vyama vyote.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba CHADEMA inatambua vyama vingine kuamini wanachokiamini?

MNYIKA: Sahihi.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba mwanachama wa CHADEMA yeyote lazima aiheshimu Katiba ya chama?

MNYIKA: Anapaswa, siyo lazima. Wapo wanaokiuka na wanachukuliwa hatua.

NASSORO KATUGA: Asiyeifuata anachukuliwa hatua?

MNYIKA: Asiyeifuata ndiyo anachukuliwa hatua. Sahihi.

NASSORO KATUGA: Mtu yeyote anayeamini Katiba ya CHADEMA anatakiwa kutokuamini anachokiamini mwanachama mwingine wa chama kingine?

MNYIKA: Sijaelewa swali. Vyama vingi siyo idadi ya vyama.

NASSORO KATUGA: Kwa mujibu wa Ibara ndogo ya 4 uliyotusomea, mwanachama wa CHADEMA akikataa kumpa mtu mwingine uhuru wa demokrasia, anakuwa amevunja haki ya mtu mwingine?

MNYIKA: Si kweli.

NASSORO KATUGA: Kama nilikusikia na kukuelewa, unasema tarehe 3 Aprili 2025 ulikuwepo katika mkutano?

MNYIKA: Ndiyo.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa nani alikuwa Mwenyekiti wa mkutano?

MNYIKA: Hapakuwa na Mwenyekiti wa mkutano ule.

NASSORO KATUGA: Kwa hiyo, mikutano ya CHADEMA haina Mwenyekiti?

MNYIKA: Siyo kila mkutano una Mwenyekiti.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa kama uliwaambia baadhi ya mikutano ya CHADEMA haina Mwenyekiti.

MNYIKA: Niliwaambia kuwa ulikuwa mkutano wa ndani.

NASSORO KATUGA: Ulisema kuna mikutano ya ndani na hadhara. Je, ule ulikuwa mkutano wa wapi kwa mujibu wa Katiba?

MNYIKA: Siyo kwa mujibu wa Katiba; ni kwa mujibu wa utendaji. Hutoona kifungu aina ya mikutano.

NASSORO KATUGA: Ule ulikuwa ni mkutano gani?

MNYIKA: Mkutano wa ndani.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti alikuwa na cheo gani?

MNYIKA: Mwenyekiti alikuwa ni Mwenyekiti vilevile kwa cheo chake.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 19

NASSORO KATUGA: Hiki chama chetu cha CHADEMA kinapowaita watia nia, hawa watia nia wanaenda kuongea na nani?

MNYIKA: Kuongea na chama.

NASSORO KATUGA: Nitakuwa sahihi kusema kwamba watia nia hawaendi kuongea na Mwenyekiti, Katibu Mkuu wala Naibu Katibu Mkuu. Wanaenda kuongea na nani?

MNYIKA: Wanaenda kuongea na viongozi wa chama.

NASSORO KATUGA: Hii kesi ya uhaini ya Mwenyekiti wetu, Tundu Antipas Lissu, ulishawahi kuiongelea hii kesi?

MNYIKA: Sijawahi kuitisha vyombo vya habari Makao Makuu kuiongelea.

NASSORO KATUGA: Ulishawahi kusema mashahidi wa Jamhuri kuwa ni waongo, kwamba kesi ni ya kubambika?

MNYIKA: Sijaelewa swali lako.

NASSORO KATUGA: Uliwahi kuiongelea hii kesi?

MNYIKA: Hapana. Nimesema Mwenyekiti siyo muhaini, lakini siyo kuiongelea kesi.

NASSORO KATUGA: Unaposema Mwenyekiti wetu siyo muhaini, unatoa ushahidi kwa mujibu wa maoni yako unavyomjua Mwenyekiti au shahidi?

MNYIKA: Kwa mujibu wa maoni yangu ninavyomjua Mwenyekiti.

NASSORO KATUGA: Ulisema wewe ni Mratibu wa vikao vyote?

MNYIKA: Hapana, mimi siyo Mratibu wa vikao vyote.

NASSORO KATUGA: Vikao vya Kamati Kuu anaratibu nani?

MNYIKA: Katibu Mkuu.

NASSORO KATUGA: Ni wewe umeratibu kikao cha tarehe 29?

MNYIKA: Juzi ni mimi.

NASSORO KATUGA: Kikao cha Kamati Kuu tarehe 29 Agosti ni kikao cha Kikatiba au kikao cha ndani?

MNYIKA: Katibu tu.

NASSORO KATUGA: Mwenyekiti wake anakuwa nani?

MNYIKA: Makamu Mwenyekiti, na Makamu Mwenyekiti kama Mwenyekiti hayupo.

NASSORO KATUGA: Baada ya kikao hicho, mlikubaliana kusema mliyokubaliana?

MNYIKA: Mimi nilikuwa nimeshaondoka.

NASSORO KATUGA: Lakini wewe ni mratibu.

MNYIKA: Sahihi. Ulisema kuratibu, ndiyo maana nikajibu niliondoka.

NASSORO KATUGA: Ni kweli mlitoa taarifa kwa umma? Waambie Waheshimiwa Majaji kama mlijadili hii kesi.

MNYIKA: Tulipokea taarifa ya kesi iliyopo Mahakamani kwamba Mwenyekiti amekutwa na kesi ya kujibu.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Kumeanza kupendeza mwaka wa uhaini lazima tukaguane Elimu zetu sio Kitambi kikubwa ukiongea unakunja kunja Uso kumbe kidato hakuna 🤠🤠

Kama namuona Shemeji Heche wasiwasi kibao mana anajua niyeye ndio mlengwa wa
Katuga kazi anayo kutachangamka tu
Wameyataka wenyewe badala ya Maridhiano 🤠🤠🤠🤠🤠
Katuga ndio unamwona ana akili sana za kuchallenge vichwa vya Cdm?
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

NASSORO KATUGA: Ni kweli taarifa yenu mlisema mmekubaliana kumtetea Mwenyekiti kwa nguvu zote?

MNYIKA: Sijaiona bado.

NASSORO KATUGA: Na bado unajiita Katibu Mkuu, ndiyo Mtendaji Mkuu wa Chama?

MNYIKA: Ndiyo, lakini ana wasaidizi wake kama mikono yake.

NASSORO KATUGA: Wasaidizi wake wanaweza kutenda mambo ya kichama bila Katibu Mkuu kujua?

MNYIKA: Wanaweza kwa baadhi ya majukumu.

NASSORO KATUGA: Ulisema ulipendekezwa na Mwenyekiti, jina lako?

MNYIKA: Ndiyo, nikathibitishwa na Baraza Kuu.

NASSORO KATUGA: Lakini juzi mlisema mmejadili kesi hii?

MNYIKA: Ni sahihi kuhusu kupokea taarifa ya kesi.

NASSORO KATUGA: Lakini ni kuhusu kesi hii?

MNYIKA: Sahihi.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba, unavyomfahamu Mwenyekiti na alivyokuteua, nitakuwa sahihi nikisema wewe ni shahidi mwenye maslahi?

MNYIKA: Hapana, siyo maslahi kwa namna unavyotamka wewe. Kuna Party Interest na Public Interest.

NASSORO KATUGA: Unaelewa anashitakiwa nini Mwenyekiti wako kuhusu uhaini?

MNYIKA: Uhaini wa kuchocheaisha maneno katika mtandao.

NASSORO KATUGA: Je, Tundu Lissu ana utii kwa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania?

MNYIKA: Sijui.

NASSORO KATUGA: Je, ni raia wa Tanzania?

MNYIKA: Ndiyo.

NASSORO KATUGA: Ulikuwa unafuatilia huo mkutano?

MNYIKA: Nilikuwepo.

NASSORO KATUGA: Unaweza kuwepo na usifuatilie?

MNYIKA: Nilikuwepo, naufuatilia.

NASSORO KATUGA: Ule mkutano wa ndani, watia nia wote walifika?

MNYIKA: Siyo wote. Kwa hiyo siwezi kujua nani hajafika.

NASSORO KATUGA: Ulisema mliwaita kwa sababu gani?

MNYIKA: Kuwapa maazimio ya chama kuhusu “No Reform, No Election” kutoka Bagamoyo. Na siku moja kabla walituma waraka, ndiyo wakaambiwa waje siku hiyo kusikia majibu yao.

NASSORO KATUGA: Mwenyekiti wa chama alialikwa na nani?

MNYIKA: Naibu Katibu Mkuu Bara ndiye aliyempigia simu.

NASSORO KATUGA: Ni kweli kwamba alimualika aje aongee na watia nia?

MNYIKA: Alimualika Mwenyekiti na viongozi wengine wa chama.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 21

NASSORO KATUGA: Shahidi, jibu swali langu.

MNYIKA: Alimualika Mwenyekiti.

NASSORO KATUGA: Katika ushahidi wako umeiambia Mahakama kwamba, mbali na kumualika Mwenyekiti, tulimuandikia risala.

MNYIKA: Hapana, sijasema.

NASSORO KATUGA: Ile risala Mwenyekiti aliyoitoa ilikuwa imeandaliwa na Secretariat?

MNYIKA: Hatukumuandikia risala.

NASSORO KATUGA: Unajua tofauti kati ya ajenda na risala?

MNYIKA: Risala haitolewi na Mwenyekiti; inatolewa na mtu mwingine, halafu Mwenyekiti anajibu. Mwenyekiti anatoa hotuba.

NASSORO KATUGA: Hiyo hotuba mlimuandikia nyinyi au alikuja nayo?

MNYIKA: Hatukumuandikia, kwa sababu inatokana na misimamo ya chama.

NASSORO KATUGA: Shahidi, katika hiyo hotuba ulisikia sehemu Mwenyekiti anasema Majaji ni Ma-CCM?

MNYIKA: Sikusikia.

NASSORO KATUGA: Ulisikia alisema Polisi wanaiba kura na vibegi mgongoni?

MNYIKA: Nilisikia.

NASSORO KATUGA: Ulisikia akisema tunaenda kuhamasisha uasi?

MNYIKA: Nilisikia.

NASSORO KATUGA: Ulisikia akisema tunaenda kukinukisha?

MNYIKA: Nilisikia.

MNYIKA: Lakini siyo kwa maana yenu nyinyi. Alifafanua anamaanisha nini.

NASSORO KATUGA: Kwa hiyo unasema alifafanua?

MNYIKA: Kwa mambo mahususi.

NASSORO KATUGA: Ulileta hapa Mahakamani?

MNYIKA: Nilileta kwa ushahidi wangu wa mdomo.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa Majaji, Katiba yetu ya chama inatambua demokrasia ya vyama vingi.

MNYIKA: Sahihi.

NASSORO KATUGA: Uchaguzi Mkuu upo kwa mujibu wa sheria?

MNYIKA: Uchaguzi halali.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Mnyika alishawahi kuwa "Tanzania One" jikague mwenyewe wewe uliwahi kuwa nani kati ya nafasi kumi za mwanzo kwenye mitihani ya kitaifa.

Historia inaonesha Mnyika aliacha chuo kikuu ili aijenge CHADEMA na siyo kwamba alikosa sifa za kwenda chuo kikuu. Waliosoma naye walishangazwa na uamuzi wake wa kuacha chuo badala yake aende kuijenga CHADEMA.

Sasa mnyika na yule mnayemuita "Dakta" unadhani wanalingana kwa lolote... Mnyika ni msomi.

Kufanya vizuri sehemu nyingi za Uchumi makusanyo ya TRA nk
Kufanya kwake vizuri kunafanya tumuamini CV zake

Angefanya vibaya tungepata Sababu za kutaka kujua Ukweli wa kichomo chake✍️
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 22

NASSORO KATUGA: Shahidi, upo timamu?

MNYIKA: Na wewe upo timamu?

NASSORO KATUGA: Siyo kazi yako kuniuliza maswali. Ukitaka, waombe Majaji niwe shahidi.

NASSORO KATUGA: Uchaguzi Mkuu wa Wabunge, Madiwani na Rais upo kwa mujibu wa sheria.

MNYIKA: Upo kwa mujibu wa sheria.

NASSORO KATUGA: Unajua kwamba Tanzania ina Katiba?

MNYIKA: Ndiyo.

NASSORO KATUGA: Uchaguzi Mkuu upo kwa mujibu wa Katiba au haupo kwa mujibu wa Katiba?

MNYIKA: Umewekwa kwa mujibu wa Katiba.

JAJI NDUNGURU: Tuandike nini?

NASSORO KATUGA: Swali jepesi sana, lakini hataki kujibu.

LISSU: (Anasimama) Wakili akisema hataki kujibu anakosea. Nimeandika hapa kwamba shahidi kasema uchaguzi unaitishwa kwa mujibu wa Katiba.

NASSORO KATUGA: Ananichukulia muda.

LISSU: Ninachomaanisha, Waheshimiwa Majaji, ameshajibu.

JAJI NDUNGURU: Kwenye cross-examination unaweza kuuliza swali hata mara nne.

LISSU: Kama tuna muda huo, tuendelee.

NASSORO KATUGA: Uchaguzi wa Madiwani, Wabunge na Rais upo kwa mujibu wa Katiba?

MNYIKA: Una-exist kwa mujibu wa Katiba.

NASSORO KATUGA: Haya, tuambie maana ya “exist” kwa Form Six yako.

MNYIKA: Umewekwa.

NASSORO KATUGA: Nitakuwa sahihi nikisema Mtanzania yeyote anaamini ana haki ya kushiriki uchaguzi?

MNYIKA: Ukiwa huru, haki na halali.

NASSORO KATUGA: Umetuambia uchaguzi mkuu umewekwa kwa mujibu wa Katiba?

MNYIKA: Ndiyo.

NASSORO KATUGA: Nitakuwa sahihi nikisema mtu yeyote Tanzania, wa chama chochote, ana haki ya kushiriki Uchaguzi Mkuu?

MNYIKA: Anayo haki ya kushiriki uchaguzi huru, wa haki na halali.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE
 
Upo sahihi! Wengi humu wana hasira na mama Abdul kiasi kwamba ukiandika kitu kinachohusiana nae hawatumii kichwa kufikiri wanahemka tu.

Ile siku waliposema ana kesi ya kujibu, ndo nilijua wamedhamiria kumfunga.
Ingekuwa ni rahisi kama ilivyodhaniwa wangeshafika mwisho, sisi hupanga yetu na Mungu naye ana mipango yake.
 
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

NASSORO KATUGA: Sijui, Waheshimiwa Majaji, kama jibu lake mmelipata.

LISSU: Waheshimiwa Majaji, hii submission kwa Majaji au ni examination? Kwani ameambiwa na Majaji, hamjasikia?

NASSORO KATUGA: Kwa hiyo, Mtanzania yeyote ana haki ya kushiriki Uchaguzi Mkuu?

MNYIKA: Ana haki ya kushiriki uchaguzi wa haki, huru na halali.

NASSORO KATUGA: Ni haki kwa mwanachama wa CHADEMA kuzuia Uchaguzi Mkuu uliowekwa kikatiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, wakati CHADEMA inaamini vyama vingi?

MNYIKA: Ni haki kama siyo halali. Utakuwa unazuiwa kwa njia za kidemokrasia.

NASSORO KATUGA: Ulikuwa umefafanua maneno ya “No Reform, No Election” kwamba ilikuwa chini ya Mwenyekiti nani?

MNYIKA: Siyo Mwenyekiti, ni Kamati Kuu ya CHADEMA.

NASSORO KATUGA: Ulisema Kiswahili cha “No Reform, No Election” ni nini?

MNYIKA: Bila mabadiliko, hakuna uchaguzi.

NASSORO KATUGA: Katika maneno ya “No Reform, No Election” kuna maneno “utahamasisha uasi”?

MNYIKA: Hakuna.

NASSORO KATUGA: Kwenye hayo maneno ya “No Reform, No Election” kuna sehemu yenye maneno “TUTAKINUKISHA”?

MNYIKA: Hakuna hayo maneno.

NASSORO KATUGA: “No Reform, No Election” kuna sehemu yenye maneno yanayosema tunaenda kuuvuruga huu uchaguzi?

MNYIKA: Kwenye hayo maneno hakuna, ila kuna maazimio mengine 10.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa kuhusu aliyozungumza Mwenyekiti siku ya tarehe 3 Aprili, ikiwemo kwamba alisema atazuia uchaguzi.

MNYIKA: Yapi hasa, mahususi?

NASSORO KATUGA: Ukirejea baadhi ya maneno aliyosema Mwenyekiti katika mkutano wa tarehe 3 Aprili.

MNYIKA: Niliyarejea.

NASSORO KATUGA: Ukiwa unayarejea hayo maneno hapa, ni kwa kuyaona siku hiyo au kuyasikia?

MNYIKA: Kwa kusikia.

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa Majaji, ushahidi wa maneno ni wa kusikia au kuona?

MNYIKA: Ulishasema ni layman, sifahamu.

NASSORO KATUGA: Mtu akitamka neno unaliona au unalisikia? Sasa napima akili yako.

MNYIKA: Unayasikia. Na mimi napima akili yako kama unaelewa majibu yangu.

NASSORO KATUGA: Wewe ulikuwa Sekretarieti, mlipowaita waandishi wa habari, mliwawekea kizuizi cha ama warekodi, warushe baadaye?

MNYIKA: Hatukuwawekea kizuizi.

NASSORO KATUGA: Chombo cha habari chochote kilichorusha moja kwa moja hakikuwa kimevunja makubaliano yoyote na nyinyi?

MNYIKA: Hakikuwa kimevunja makubaliano.

NASSORO KATUGA: Wakati mnawaita waandishi wa habari, mlikuwa na nia/maudhui ya kuhabarisha umma kwa kile mlichokusudia kusema siku ile?

MNYIKA: Ndiyo, “No Reform, No Election.”

NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa Majaji kama mliwapa hotuba ya Mwenyekiti kabla hao watu hawajaja.

MNYIKA: Hapana.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE UJUMBE UFIKE MBALI
 
Majaji wanaandika na kwa muda tulionao. Tutakwenda break na kurudi kwenye Cross Examination ya upande wa Jamhuri
Unafanya kazi nzuri sana , mkuu 'Mawele'.

Kidogo tu hilo la akina 'Fransco', usingelitumbukiza humo kwenye taarifa muhimu sana kama hii.
Haya maswala ya namna hii ndiyo yanayoongeza mitafaruku miongoni mwetu, hasa wakati kama huu.
Hatuwezi kuyakataa, kwa sababu ni sehemu ya urithi wetu; lakini tuzo kubwa ni Tanzania iliyo na mshikamano imara, ambayo ndiyo itatuwezesha kuyafanya hayo yote kwa utulivu..

Ni saa mbaya sana tuliomo wakati huu kama taifa; kwa hiyo ni lazima tuwe na uangalifu mkubwa na jambo lolote linaloweza kuchochea utengamano kati yetu.
 
Back
Top Bottom