Manyanza
Platinum Member
- Nov 4, 2010
- 22,269
- 58,563
WAKILI WA SERIKALI ANAMHOJI JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 16
MNYIKA: Hapana, nateuliwa na Baraza Kuu baada ya kuthibitishwa.
NASSORO KATUGA: Unatuchanganya tena. Hapo mwanzo umesema kwamba unapendekezwa na Mwenyekiti.
MNYIKA: Sahihi, lakini inathibitishwa na Baraza Kuu.
NASSORO KATUGA: Mbona unatuchanganya?
MNYIKA: Ukitaka kujua Katiba ya CHADEMA, ujue kwanza Katibu Mkuu anaondolewaje. Mwenyekiti hana uwezo wa kumuondoa Katibu Mkuu.
NASSORO KATUGA: Unajipa maswali yako.
NASSORO KATUGA: Nataka uniambie Kifungu cha 3(2)(v) cha Katiba kinasemaje.
MNYIKA: Naomba niruhusiwe kurefresh memory.
NASSORO KATUGA: Naomba apewe Katiba chini ya Kifungu cha 166.
NASSORO KATUGA: Ibara ya 3(2)(v), CHADEMA inaamini utu?
MNYIKA: Ndiyo.
MNYIKA: Wasomee, Waheshimiwa, Ibara ya 4(1): “Kushika dola kwa njia ya kidemokrasia ili kuleta maendeleo endelevu.”
NASSORO KATUGA: Kwa hiyo ni sahihi kusema kwamba dhumuni la CHADEMA ni kushika dola kwa njia ya kidemokrasia?
MNYIKA: Sahihi, ingawa siyo pekee.
NASSORO KATUGA: Kwa jinsi ilivyo, CHADEMA dhumuni lake ni kushika dola kwa njia ya demokrasia.
MNYIKA: Chama kina madhumuni ya kijamii, kiuchumi na kisiasa. Kushika dola siyo dhumuni pekee.
NASSORO KATUGA: Kushika dola ni dhumuni kuu.
MNYIKA: Siyo dhumuni kubwa.
NASSORO KATUGA: Waambie Waheshimiwa Majaji kiwango chako cha elimu.
MNYIKA: Kidato cha Sita.
NASSORO KATUGA: Kwa kuwa ni Kidato cha Sita, nipo sahihi kusema wewe ni layman wa sheria?
MNYIKA: Sijapita Law School, kwa hiyo ni layman.
NASSORO KATUGA: Kwa hiyo nipo sahihi nikisema huna uzoefu wa sheria wa kutoa maoni ya kisheria?
MNYIKA: Nimetoa kwa sababu ya uzoefu wa kisiasa na kibunge wa kutunga hizo sheria.
NASSORO KATUGA: Maoni uliyotoa wakati wa ushahidi wako yanatokana na uzoefu wako wa kibunge?
LISSU: Waheshimiwa Majaji, sijasikia shahidi akisema kwamba sijatoa maoni ya kisheria. Anamlisha maneno.
JAJI: Si shahidi atasema hivyo kwamba hajasema hivyo?
LISSU: Nasema hivyo kwa sababu Wakili haruhusiwi kumlisha shahidi maneno wakati wa cross-examination.
JAJI NDUNGURU: Ndiyo, shahidi aseme kwamba sikusema.
LISSU: Tukienda hivyo, maana yake mnanizuia niseme lolote ninapoona shahidi anawekewa maneno. Sidhani kama ni sahihi.
MAHAKAMA: IPO KIMYA KIDOGO BAADA YA OBJECTION YA LISSU.
JAJI NDUNGURU: Nadhani tuendelee.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI