TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 8
Mnyika: Ukiondoa Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu na Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche, alikuwepo.
Lissu: Nini kikaendelea?
Mnyika: Mara baada ya ziara kuendelea, Mwenyekiti akakamatwa tarehe 9 Aprili 2025, Mbinga, Ruvuma.
Lissu: Sasa turudi kwenye Mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, ambao ndiyo umeleta kesi hii.
Swali langu ni, vile ulivyosema mikutano hii ilikuwa utekelezaji wa vikao vya Chama, waeleze tofauti kati ya hoja zilizotolewa Kanda ya Nyasa, Kusini na huu wa tarehe 3 Aprili.
Mnyika: Hoja yetu ya mabadiliko ya Kisheria kuhusu sheria ya uchaguzi na sababu za mabadiliko hayo, na msimamo wa Chama kuhusu No Reforms, No Election, zilikuwa zilezile.
Isipokuwa kabla ya Mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, Katibu Mkuu nilikuwa nimepokea barua au waraka wa wanaojiita watia nia wakitaka Chama kibadili msimamo wa No Reforms, No Election.
Kwa hiyo, katika Mkutano wa tarehe 3 Aprili 2025, hoja hizo hizo zilizosemwa kwenye mikutano ya hadhara na mikutano mingine ya wadau zilitumika kutoa majibu juu ya msimamo wa Chama, Baraza Kuu la Chama na Mkutano Mkuu wa Chama juu ya No Reforms, No Election.
Lissu: Sasa nikurudishe katika maneno:
“Msimamo huu unaashiria uasi, ni kweli kwamba msimamo huu unaashiria uasi, tutasimamisha uchaguzi, uchaguzi huu tutauvuruga, tutauvuruga kwa sababu tunaenda kukinukisha vibaya.”
Waeleze Majaji kwamba uelewa wako ni nini.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hayo ni maoni. Huyu ni shahidi ameapishwa kutoa ushahidi wake.
Sasa hapa anaulizwa kuhusu maoni.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, sijui kama Wakili wa Serikali anaelewa swali nililouliza.
Nimeuliza kuhusu uelewa wake.
Aseme uelewa wake.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, hii ni oral testimony. Kifungu cha 67 kinazungumza kuhusu ushahidi wa opinion, kama huyo ana uelewa wa hicho anachoulizwa.
Yeye kama expert wa sheria angezungumza.
Huyu hapa anatakiwa kuzungumzia kama aseme amekiona au amekisikia.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, tusipoteze muda. Wacha niulize upya swali.
Lissu: Shahidi, ufahamu wako wa haya maneno ndiyo tunataka.
Mnyika: Haya ni maneno ya kisiasa ambayo tunatumia kuhamasisha umma ili umma uone uchaguzi una uozo mkubwa, unanuka, na umma uweze kukataa.
Uchaguzi uvurugike au kususia.
Ni hatua za kisiasa juu ya umma kususia uchaguzi usio halali.
Lissu: Asante.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama baada ya huo Mkutano wa tarehe 3 Aprili ulichukua hatua zozote kulijulisha Jeshi la Polisi juu ya maneno hayo.
Mnyika: Hapana, sikuwaeleza Polisi jambo lolote.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI