Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Kesi ya Uhaini: John Mnyika aendelea kutoa Ushahidi kumtetea Tundu Lissu Mahakamani leo Agosti 31, 2026. Kesi imeahirishwa hadi Kesho

Yaani anachofanya Lisu ni sawa na kumtega panya kwa kipande cha nyama ya kuku inayonukia vizuri. Nyama kaila na kujiona mshindi,kumbe ni mtego,sasa amenasa,ni mwendo wa kuponda kichwa,hakuna huruma.
Go Lisu.
Shukrani pia mleta update.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

Kesi inasomwa na Karani wa Mahakama: CRIMINAL SESSION, kesi namba Tundu Antipas Lissu dhidi ya Jamhuri.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake wa Serikali:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mwandamizi
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Kasara – Wakili wa Serikali

Waheshimiwa Majaji, sisi wote tunaiwakilisha Jamhuri na mshtakiwa yupo kizimbani.

Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi, sisi tupo tayari.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?

Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Shahidi namba mbili, karibu kizimbani.

Shahidi, nakukumbusha kuwa upo chini ya kiapo.

Mnyika: Shukrani.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba nikumbushe nimeshia wapi.

Jaji: Shahidi, uliishia wakati unasema mlidai mabadiliko ili uchaguzi ufanyike, lakini CCM na Serikali yake walikataa mapendekezo.

Mnyika: Sawa sawa.

Lissu: Shahidi, Sabhaheri.

Mnyika: Sabhaheri.

Lissu: Upo sawa sawa?

Mnyika: Nipo sawa sawa.

Lissu: Maana tunaonana Mahakamani tu.

Lissu: Naomba uelezee mambo ambayo yalikuwa katika hotuba yangu unayoyakumbuka.

Weka EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Afya njema Manyanza:Tupo tayari kukusikilizaa!
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 1.

Kesi inasomwa na Karani wa Mahakama: CRIMINAL SESSION, kesi namba Tundu Antipas Lissu dhidi ya Jamhuri.

Wakili wa Serikali Mkuu, Ajuaye Zegeli, anawatambulisha mawakili wenzake wa Serikali:

1. Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu
2. Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mwandamizi
3. Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu
4. Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali
5. Kasara – Wakili wa Serikali

Waheshimiwa Majaji, sisi wote tunaiwakilisha Jamhuri na mshtakiwa yupo kizimbani.

Shauri limekuja kwa ajili ya utetezi, sisi tupo tayari.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, upo tayari?

Lissu: Nipo tayari, Mheshimiwa.

Jaji Ndunguru: Shahidi namba mbili, karibu kizimbani.

Shahidi, nakukumbusha kuwa upo chini ya kiapo.

Mnyika: Shukrani.

Jaji Ndunguru: Tuendelee.

Lissu: Waheshimiwa Majaji, naomba nikumbushe nimeshia wapi.

Jaji: Shahidi, uliishia wakati unasema mlidai mabadiliko ili uchaguzi ufanyike, lakini CCM na Serikali yake walikataa mapendekezo.

Mnyika: Sawa sawa.

Lissu: Shahidi, Sabhaheri.

Mnyika: Sabhaheri.

Lissu: Upo sawa sawa?

Mnyika: Nipo sawa sawa.

Lissu: Maana tunaonana Mahakamani tu.

Lissu: Naomba uelezee mambo ambayo yalikuwa katika hotuba yangu unayoyakumbuka.

Weka EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Mungu wa mbinguni mjaa rehema na baraka simama na wale wanyonge wenye kuhitaji fadhila na msaada wako. Bali shusha moto, laana, mikosi na dhoruba mpaka vizazi vyao kwa wale wenye ujivuni na roho ya unyanyasi kuanzia namba moja mpaka hawa
Nassoro Katuga – Wakili wa Serikali Mkuu, Tawabu Issa – Wakili wa Serikali Mwandamizi, Job Mrema – Wakili wa Serikali Mkuu, Cuthbert Mbilinyi – Wakili wa Serikali, Kasara – Wakili wa Serikali.
Amina!
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 6.

Lissu: Baada ya Baraza Kuu la Chama kuridhia hayo maazimio, kitu gani kilitokea?

Mnyika: Tarehe 21 Januari 2025, niliwasilisha taarifa ya Baraza Kuu kwa Mkutano Mkuu juu ya utendaji wa Chama kwa kipindi cha miaka 5.

Na ndani ya taarifa hiyo, kama sehemu ya taarifa hiyo, nilipeleka mapendekezo ya Baraza Kuu kwa Mkutano Mkuu juu ya maazimio ya Mkutano.

Na kati ya maazimio hayo ni Mkutano Mkuu kupitisha uamuzi wa kutaka Tume ya Uchaguzi ipitishe mabadiliko hayo.

Azimio la kutaka mabadiliko ya Kikatiba na Kisheria kabla ya uchaguzi wa 2025, yenye kuwezesha kuwepo uchaguzi huru na haki.

Na kwamba bila mabadiliko hayo hakuna uchaguzi (No Reforms, No Elections).

Lissu: Shahidi, umeieleza Mahakama kuwa palikuwa na Mkutano wa Dharura wa Kamati Kuu, Mkutano wa Baraza na Mkutano Mkuu wa kutaka mabadiliko.

Waeleze Waheshimiwa Majaji, nani alikuwa Mwenyekiti wa vikao vyote hivyo?

Mnyika:
Kamati Kuu ya tarehe 2 Desemba 2024,
Kamati Kuu ya tarehe 19 Januari 2025,
Baraza Kuu la tarehe 20 Januari 2025,
na Mkutano Mkuu wa tarehe 21 Januari 2025.

Vikao vyote hivyo viliongozwa na Mwenyekiti wa wakati huo, Freeman Aikael Mbowe.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kitu gani kilitokea mara baada ya Mkutano Mkuu wa Chama kupitisha hayo maazimio?

Mnyika: Mkutano Mkuu ukiendelea na ajenda ya uchaguzi ambayo ilisimamiwa na Kamati ya Wazee na Mwenyekiti wa Uchaguzi.

Na Mkutano Mkuu ukiendelea hadi tarehe 22 Januari 2025.

Lissu: Kitu gani kilitokea katika huo uchaguzi?

Mnyika: Alichaguliwa ndugu Tundu Antipas Lissu na Makamu wote wawili.

Makamu Mwenyekiti Bara, ndugu John Wegesa Heche.

Na Makamu Mwenyekiti Zanzibar, ndugu Saidi Mzee Saidi.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Mkutano Mkuu wa Chama uliamua kitu gani juu ya utekelezaji wa maazimio yake?

Mnyika: Mkutano Mkuu uliamua kuanza mara moja utekelezaji wake mara baada ya uchaguzi wa Chama kufanyika.

Lissu: Baada ya Mkutano Mkuu, kilitokea nini?

Mnyika: Baraza Kuu la Chama lilikaa siku hiyo hiyo ya tarehe 22 Januari 2025, ambapo mimi, John Mnyika, nilichaguliwa kuwa Katibu Mkuu.

Na manaibu wake, Sam Golugwa, Naibu Katibu Mkuu Bara.

Na Naibu Katibu Mkuu Zanzibar, Ali Ibrahim Juma.

Na uteuzi wao ulithibitishwa na Baraza Kuu.

Lissu: Jambo gani lingine Baraza Kuu lilifanya?

Mnyika: Baraza Kuu vilevile lilipokea majina ya Mwenyekiti ya wajumbe wa Kamati Kuu wa kuteuliwa na kuthibitisha uteuzi wao.

Lissu: Baada ya vikao vyote hivi vya Chama kukamilika, je, ni vitu gani vilitokea katika utekelezaji wa maazimio?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE JOHN MNYIKA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 7.

Mnyika: Katika utekelezaji wa hayo maazimio, niliitisha retreat ya Kamati na vikao mfululizo vya Sekretarieti, Kamati Kuu na viongozi wakuu wa Chama, kuanzia tarehe 31 Januari hadi 4 Februari, ili kupanga utekelezaji wa No Reforms, No Election.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji mpango wa utekelezaji sasa.

Mnyika: Mosi, kutoa elimu kupitia mikutano ya hadhara ya wananchi.

Pili, tulipitisha mpango wa kukutana na wadau wengine wa uchaguzi, kama asasi za kiraia, viongozi wa dini, sekta binafsi na taasisi nyingine za kijamii.

Tatu, tulipitisha mpango wa kuzungukia vyombo vya habari na kukutana na wahariri wa vyombo vya habari.

Nne, tulipitisha mpango wa kujulisha Jumuiya ya Kimataifa na Kikanda.

Kukutana na viongozi wa Chama ambao hawakuwa sehemu ya uongozi wa Chama.

Kukutana na watu mashuhuri vilevile.

Na Sekretarieti ipewe jukumu la kutafuta njia nyingine za utekelezaji wa No Reforms, No Election.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, utekelezaji wa huo mkakati ulioupitisha ulikuwaje?

Mnyika: Mwenyekiti alianza ziara akiambatana na viongozi wengine.

Nakumbuka, kwa upande wa viongozi wa dini, alienda kukutana na Sheikh Issa Ponda.

Nakumbuka, kwa asasi za kiraia, alikutana na Tanzania Centre for Democracy.

Akaenda kukutana na Tanganyika Law Society.

Kwa watu mashuhuri, alikutana na Jaji Joseph Sinde Warioba (mstaafu).

Kwa upande wa kuwahusisha vyombo vya habari, tarehe 9 Februari 2025 alilihutubia Taifa kuhusu Mkutano wa Bagamoyo.

Na tarehe 2 Machi akakutana na wahariri wa habari Makao Makuu ya Chama.

Lissu: Na kuhusu Jumuiya ya Kimataifa ilikuwaje?

Mnyika: Nakumbuka alitembelea balozi mbalimbali. Sina uhakika na wengine, ila nakumbuka Balozi wa Marekani.

Tarehe 9 Machi 2025, akapokea barua ya Jaji Mtungi, Msajili wa Vyama vya Siasa, kwenda kueleza yaliyotokea Bagamoyo.

Tarehe 17 Machi niliongoza ujumbe wa Chama kwenda Ofisi ya Msajili.

Lissu: Wapi?

Mnyika: Ukitoka Chuo cha IFM kwenda Ikulu, jirani na Shule ya Msingi Bunge.

Lissu: Dodoma?

Mnyika: Hapana, Dar es Salaam.

Lissu: Kitu gani kilitokea kwa Msajili wa Vyama vya Siasa?

Mnyika: Akatuuliza kuhusu kampeni ya No Reforms, No Election.

Akatuuliza kama kampeni hiyo inakiuka sheria ya Vyama vya Siasa na mikutano yake inayoendelea nchi nzima.

Baada ya kumueleza kuhusu Mkutano wa Kamati Kuu wa Bagamoyo, akasema haoni shida yoyote ya Kisheria.

Na baadaye akatoa taarifa mbele ya vyombo vya habari tarehe 10 Aprili 2025 akiwa Dodoma, kwamba kauli mbiu ya No Reforms, No Election ni kauli mbiu ya kisiasa ambayo haikiuki sheria yoyote.

Lissu: Asante.

Sasa, Shahidi, hebu tubakie kidogo. Kwenye hicho kikao cha tarehe 17 Machi na Msajili, ulisema uliongoza ujumbe katika hicho kikao.

Nani mwingine alikuwepo?

Mnyika: Katika Ofisi ya Msajili alikuwepo Sisty Nyahoza.

Lissu: Siyo Shosti?

Mnyika: Sisty Nyahoza.

Lissu: Anhaa, nilisikia vibaya.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, utekelezaji wa hayo maazimio ya No Reforms, No Election kwa upande wa umma ulikuwaje?

Mnyika: Tulipanga ziara na Sekretarieti, awamu ya kwanza kwa Kanda ya Nyasa yenye mikoa ya Mbeya, Songwe, Iringa, Njombe na Rukwa, ambapo uzinduzi ulifanyika tarehe 23 Machi 2025, ambapo Mwenyekiti Tundu Lissu alikuwa mhutubiaji mkuu.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, hiyo ziara ya Kanda ya Nyasa iliwahusisha kina nani?

Mnyika: Ukiondoa Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu, ni Makamu Mwenyekiti Bara, John Wegesa Heche, na wajumbe wa Kamati Kuu ya Chama.

Lissu: Ziara hiyo ilimalizika lini?

Mnyika: Sina kumbukumbu sahihi, lakini ilidumu kuanzia tarehe 23 Machi hadi mapema Aprili, wiki ya kwanza ya mwezi Aprili, ambapo tulipanga kikao cha watia nia.

Lissu: Ulishaeleza Mahakama kuhusu maandalizi yako ya Mkutano huo wa tarehe 3 Aprili, na nataka baada ya tarehe 3 Aprili kitu gani kilitokea?

Mnyika: Tulipanga kuanza operesheni ya Chama awamu ya pili, Kanda ya Kusini.

Lissu: Ziara Kanda ya Kusini ilifanyikaje?

Mnyika: Sina kumbukumbu ya tarehe, ila mara baada ya kikao na watia nia, misafara ilianza kuondoka kuelekea Kusini, mikoa ya Lindi, Mtwara na Ruvuma, kati ya tarehe 4 na 5 Aprili. Sina kumbukumbu kamili.

Lissu: Kina nani walishiriki hiyo ziara?

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
Back
Top Bottom