TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 5.
Lissu: Wakati hayo ya maandalizi na mawasiliano yanafanyika, mimi nilikuwa wapi?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu na Makamu Mwenyekiti Bara John Wegesa Heche walikuwa katika mikutano iliyokuwa inaendelea Kanda ya Nyasa.
Lissu: Unaposema Kanda ya Nyasa unamaanisha nini?
Amani Sam Golugwa: Unajumuisha Mkoa wa Mbeya, Iringa, Njombe na Songea.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu, mimi nilishiriki kwa namna yoyote ile katika maandalizi na kutuma mialiko?
Jaji Ndunguru: Ungemwambia aeleze ushiriki wako, ukisema kama ni una-suggest majibu.
Lissu: Nisameheni kama imenikaa sana.
Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji ushiriki wangu katika maandalizi.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakushiriki katika maandalizi ya mkutano huo.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ushiriki wangu katika kuwaalika waandishi wa habari.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Tundu Antipas Lissu hakushiriki kuwaalika waandishi wa habari wala wajumbe.
Lissu: Sasa inadaiwa katika mashitaka yangu kwamba mimi, Tundu Antipas Lissu, ndiyo niliye waalika katika mkutano.
Wewe unasemaje?
Amani Sam Golugwa: Hayo madai yatakuwa ya uongo na upotoshaji.
Siyo ya kweli.
Tundu Lissu hakuhusika.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, uwepo wa waandishi wa habari katika mkutano huu.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika mkutano huu walikuwepo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali:
Wa televisheni,
wa magazeti,
wa online television,
pamoja na redio.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI