Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

Kesi ya Uhaini: Leo Mahakamani 03 September, Shahidi wa tatu Aman Sam Golugwa anaendelea kutoa ushahidi wake

TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 5.

Lissu: Wakati hayo ya maandalizi na mawasiliano yanafanyika, mimi nilikuwa wapi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Mwenyekiti Tundu Antipas Lissu na Makamu Mwenyekiti Bara John Wegesa Heche walikuwa katika mikutano iliyokuwa inaendelea Kanda ya Nyasa.

Lissu: Unaposema Kanda ya Nyasa unamaanisha nini?

Amani Sam Golugwa: Unajumuisha Mkoa wa Mbeya, Iringa, Njombe na Songea.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Makamu, mimi nilishiriki kwa namna yoyote ile katika maandalizi na kutuma mialiko?

Jaji Ndunguru: Ungemwambia aeleze ushiriki wako, ukisema kama ni una-suggest majibu.

Lissu: Nisameheni kama imenikaa sana.

Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji ushiriki wangu katika maandalizi.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakushiriki katika maandalizi ya mkutano huo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji ushiriki wangu katika kuwaalika waandishi wa habari.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, Tundu Antipas Lissu hakushiriki kuwaalika waandishi wa habari wala wajumbe.

Lissu: Sasa inadaiwa katika mashitaka yangu kwamba mimi, Tundu Antipas Lissu, ndiyo niliye waalika katika mkutano.

Wewe unasemaje?

Amani Sam Golugwa: Hayo madai yatakuwa ya uongo na upotoshaji.

Siyo ya kweli.

Tundu Lissu hakuhusika.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, uwepo wa waandishi wa habari katika mkutano huu.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika mkutano huu walikuwepo waandishi wa habari kutoka vyombo mbalimbali:

Wa televisheni,

wa magazeti,

wa online television,

pamoja na redio.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Hii akili ni ya kiwango cha juu kwa majibu ya huyu mtoa ushahidi na ya Mnyika yanafanana ya kutoshiriki kwa Tundu Lissu kwenye kuandaa huo mkutano kiasi ambacho kinafanya ionekane shitaka ni la uongo hapa Serikali imepigwa na kitu kizito
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA

SEHEMU YA 9.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Chama ni uhaini?

Amani Sam Golugwa: Kitendo cha kupinga Serikali siyo uhaini kwa mujibu wa sheria.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Vyama tayari ni kosa hata kwa sheria zingine zozote.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Chama siyo kosa hata kwa sheria zingine.

Lissu: Kuna maneno mengi sana yamesemwa Mahakamani humu juu ya “tunaenda kukinukisha vibaya sana.” Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako wa “tunaenda kukinukisha.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, tafsiri ya kawaida tu ni kutoa harufu, kukifanya kitoe harufu.

Lissu: Marashi au uvundo? (Anacheka.)

Lissu: Sasa, Shahidi, mtu akisema kwa maana ambayo umeisema, yanaitishiaje Serikali?

Amani Sam Golugwa: Sioni mahali popote kwa Serikali kutishika kwa maneno hayo.

Lissu: Kwa ufahamu wako, Serikali ya Jamhuri ya Muungano inatishikaje na maneno “tutasimamisha uchaguzi” na “tutavuruga uchaguzi”?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwanza hujataja neno “Serikali.”

Lissu: Sikiliza swali langu vizuri.

Serikali inatishikaje na maneno ya “tutavuruga uchaguzi”?

Amani Sam Golugwa: Sioni sababu ya Serikali kutishika.

Lissu: Sasa, Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na watu wake wote na vyombo vyake vyote wanatishikaje?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sioni kwa namna yoyote ile Serikali ikitishika.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, Serikali na maguvu yake yote inatishikaje na maneno kwamba “tutaleta uasi”?

Amani Sam Golugwa: Sioni ni kwa namna gani Serikali itatishika kwamba “tutaleta uasi.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA

SEHEMU YA 9.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Chama ni uhaini?

Amani Sam Golugwa: Kitendo cha kupinga Serikali siyo uhaini kwa mujibu wa sheria.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Vyama tayari ni kosa hata kwa sheria zingine zozote.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kitendo cha kupinga Serikali, Taasisi au Chama siyo kosa hata kwa sheria zingine.

Lissu: Kuna maneno mengi sana yamesemwa Mahakamani humu juu ya “tunaenda kukinukisha vibaya sana.” Waeleze Waheshimiwa Majaji ufahamu wako wa “tunaenda kukinukisha.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, tafsiri ya kawaida tu ni kutoa harufu, kukifanya kitoe harufu.

Lissu: Marashi au uvundo? (Anacheka.)

Lissu: Sasa, Shahidi, mtu akisema kwa maana ambayo umeisema, yanaitishiaje Serikali?

Amani Sam Golugwa: Sioni mahali popote kwa Serikali kutishika kwa maneno hayo.

Lissu: Kwa ufahamu wako, Serikali ya Jamhuri ya Muungano inatishikaje na maneno “tutasimamisha uchaguzi” na “tutavuruga uchaguzi”?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwanza hujataja neno “Serikali.”

Lissu: Sikiliza swali langu vizuri.

Serikali inatishikaje na maneno ya “tutavuruga uchaguzi”?

Amani Sam Golugwa: Sioni sababu ya Serikali kutishika.

Lissu: Sasa, Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji, Serikali ya Jamhuri ya Muungano na watu wake wote na vyombo vyake vyote wanatishikaje?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sioni kwa namna yoyote ile Serikali ikitishika.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, Serikali na maguvu yake yote inatishikaje na maneno kwamba “tutaleta uasi”?

Amani Sam Golugwa: Sioni ni kwa namna gani Serikali itatishika kwamba “tutaleta uasi.”

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU 10.

Lissu: Katika hayo maneno niliyokusomea, waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “tutaenda kuchoma vituo vya Mwendokasi.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna maneno yanayosema “tutaenda kuchoma vituo vya Mwendokasi.” Hakuna.

Lissu: Katika maneno niliyokusomea, waeleze Waheshimiwa Majaji maneno yanayosema “tutaenda kuchoma vituo vya kupigia kura.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna maneno “tutaenda kuchoma vituo vya kupigia kura.”

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno ya “tunaenda kupiga au kuwakata vidole.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, katika maneno niliyosomewa hakuna maneno ya kwamba. Hakuna.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako, uwepo wa maneno “tutaenda kuharibu mali, kuchoma magari na vitu siku ya uchaguzi.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna maneno yanayosema kuwa “tutaenda kuharibu mali” wala “kuchoma magari siku ya uchaguzi.”

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “tunaenda kuua siku ya uchaguzi.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna maneno “tunaenda kuua siku ya uchaguzi.”

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo umemsikiliza hotuba ya Jaji Mkuu Mstaafu Othuman Chande.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nimesikiliza hotuba.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, idadi ya watu walioawa.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zangu, ninakumbuka kumsikia Jaji Mkuu Mstaafu akitaja idadi ya watu waliouawa 518.

Lissu: Shahidi, waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo unakumbuka Jaji Mkuu kusema matukio yalipangwa na kuratibiwa.

Jaji Ndunguru: Hapo sasa umeshamtajia jibu, atasema ndiyo, yalipangwa na kuratibiwa. Hivyo nalifuta hilo swali.

Nassoro Katuga: Naomba lifutwe.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo Jaji Othuman Chande alitaja waliosababisha.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zangu, sikumbuki kama Jaji Othuman Chande alitaja waliosababisha.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo Jaji Othuman Chande alitaja sababu zilizosababisha machafuko kutokea.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nakumbuka Jaji Othuman Chande alitaja madai ya Katiba Mpya, masuala ya utekaji na watu kupotea, manung’uniko ya wananchi ya muda mrefu ambayo hayajakuwa yametatuliwa.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI.
 
Wao ndo wameuchagua aina ya mchezo, uwanja wa mechi na kufungua mageti, acha waicheze ngoma. Hii inafanya hata watu waliokuwa wanashangaa kwa nini Mh. Tundu Lisu ang'ang'anie kuishinikiza serikali ifanye mabadiliko ya kisheria juu ya uchaguzi wawe na uelewa wa msingi mkuu. Hapa hata ambaye alibaki na kiimani kidogo nao kanaondoka, ukijuklisha na yanayoendelea, itawawia vigumu huko mbeleni kupata kura halali kwenye boksi la kura. Wanajining'iniza kwa kitanzi chao wenyewe.
Sahihi.

Binafsi sikuwa nafahamu kuwa wapinzani kuomba kuonana na Rais aliye madarakani huwa wanapeleka ajenda za kutaka mabadiliko kwa maandishi.

Tumeaminishwa huwa wanakaribishwa ikulu kunywa chai ….
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 8.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika hayo maneno uwepo wa neno “Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hilo neno halipo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika maneno hayo niliyokusomea, uwepo wa neno “Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hilo neno nalo halipo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama katika hayo maneno niliyokusomea kuna maneno “Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hilo neno nalo halipo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika hayo maneno niliyokusomea, uwepo wa neno “Baraza la Mawaziri la Jamhuri ya Muungano.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hayo maneno ya Baraza la Mawaziri hayapo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji katika maneno niliyokusomea, uwepo wa maneno “Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hayo maneno ya Mkurugenzi Mkuu wa Mashitaka hayapo.

Lissu: Kwa kuwa wanasema nimetishia vyombo vya dola, waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “Jeshi la Polisi.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, maneno ya Jeshi la Polisi hayapo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “Jeshi la Wananchi (JWTZ).”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, maneno “Jeshi la Wananchi” hayapo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “Jeshi la Mgambo.”

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, neno “Jeshi la Mgambo” halipo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa maneno “Usalama wa Taifa,” kama yapo.

Amani Sam Golugwa: Maneno “Mkurugenzi wa Usalama wa Taifa” hayapo.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji maneno ya majeshi yoyote, kama yapo.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, maneno hayo hayapo.

Lissu: Sasa hizi tuhuma wewe unazionaje?

Amani Sam Golugwa: Ni tuhuma za uongo, za kutunga na za kisiasa, zenye lengo la kumrudisha nyuma Tundu Antipas Lissu kudai mabadiliko ya mifumo ya uchaguzi.

Lissu: Shahidi, kwa ufahamu wako, hivi mtu akisema “msimamo huu unaashiria uasi” anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa uzoefu wangu wa kisiasa—

Lissu: Kumbuka hapo mbele kuna jeshi linakusubiria. (Anawanyooshea kidole Mawakili wa Serikali.) Sasa wewe jichanganye.

Amani Sam Golugwa: Hakuna kosa lolote ambalo mtu atakuwa ametenda kwa kusema neno hilo.

Lissu: Shahidi, kwa ufahamu wako, mtu akisema “tutauvuruga uchaguzi” atakuwa ametenda kosa gani nchini?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna kosa lolote mtu atakuwa amelitenda akilisema neno hilo.

Jaji Ndunguru: Neno hilo lipo?

Amani Sam Golugwa: La “tutauvuruga uchaguzi.”

Lissu: Shahidi, mtu akisema “tutauzuia uchaguzi” anakuwa ametenda kosa gani katika nchi hii?

Amani Sam Golugwa: Kwa ufahamu wangu, mtu akisema “tutauzuia uchaguzi” anakuwa hajafanya kosa lolote katika nchi hii.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wako wa masuala ya uchaguzi, uwapo wa kosa la kuvuruga uchaguzi au kuzuia uchaguzi katika sheria zetu za uchaguzi.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sijawahi kuona kama ni kosa kwa kusema “tutazuia uchaguzi” au “kuvuruga uchaguzi.”

Lissu: Sasa, Shahidi, kuna neno limeletwa hapa kwamba uasi ni kitendo cha kuvunja sheria. Sasa waeleze Waheshimiwa Majaji kama kitendo cha kuvunja sheria ni uhaini.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, kuvunja sheria hakupelekei kuwa muhaini.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA


SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Lissu: Kumbuka hapo mbele kuna jeshi linakusubiria. (Anawanyooshea kidole Mawakili wa Serikali.) Sasa wewe jichanganye. 🤣
 
Kwa mara ya kwanza nilianza kumuona Golukwa kwenye uchaguzi wa urais TAL akiwa mgombea, Nilijua huyu ana kitu!

Vichwa ni vichwa tu jamani.

Halafu CDM kupitishwa kwenye moto mara kwa mara nadhani imewatengenezea a very thick skin, wana confidence za hatari hawa watu.
 
Kwa mara ya kwanza nilianza kumuona Golukwa kwenye uchaguzi wa urais TAL akiwa mgombea, Nilijua huyu ana kitu!

Vichwa ni vichwa tu jamani.

Halafu CDM kupitishwa kwenye moto mara kwa mara nadhani imewatengenezea a very thick skin, wana confidence za hatari hawa watu.
Usemacho ni sawa, mtu akipitishwa kwenye moto anakuwa bora kuliko yule ambaye hapitii hayo... Angalia wadada wa kazi huwa wanakuwa bora kuliko wadada wa mama mwenye nyumba.
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 11.

Lissu: Turudi kwenye mkutano wa tarehe 03 Aprili mwaka jana.

Wewe na wajumbe wa Sekretarieti kushiriki kufanya maandalizi yoyote yale. Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo kuna hatua zozote zimechukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi yako na wenzako katika Sekretarieti kwa kuandaa mkutano na kuwezesha.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna hatua zozote zile zilizochukuliwa na Jeshi la Polisi dhidi yangu na wenzangu wa Sekretarieti.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo uliyasikia hayo maneno yakitamkwa kwenye mkutano wa tarehe 03 Aprili mwaka jana.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, niliyasikia maneno haya yakitamkwa kwenye mkutano wa tarehe 03 Aprili mwaka jana.

Lissu: Kwa kuwa yanadaiwa kuwa ya kihaini, je, ulichukua hatua yoyote ya kuyariporti Jeshi la Polisi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, mimi sikuya-ripoti maneno haya.

Lissu: Na wote waliokuwa ukumbini, kuna yeyote aliye-yaripoti maneno hayo kwa Jeshi la Polisi?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna kiongozi wala mtu yeyote aliyekuwa ukumbini aliye-ripoti kwa Jeshi la Polisi.

Lissu: Unajua kuwa kunyamazia uhaini ni kosa kisheria?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, sifahamu kama kuna kosa la namna hiyo.

Lissu: Kuna kiongozi au mtu yeyote aliyekuwa katika mkutano wa tarehe 03 amekamatwa na Jeshi la Polisi kwa kosa la kunyamazia uhaini?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna mtu yeyote aliyeshtakiwa kwa kunyamazia uhaini.

Lissu: Umewahi kusikia kuna hatua zozote ambazo zimechukuliwa kwa kurusha matangazo ya uhaini au kusambaza maudhui ya—

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sijasikia Jambo TV wala Chanzo TV akichukuliwa hatua zozote kwa kurusha matangazo na kusambaza maudhui ya uhaini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwezekano wa mtu mmoja kutenda kosa la kutishia Serikali na kupanga uhaini.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, sioni uwezekano wa mtu mmoja kutishia Serikali na kupanga uhaini. Haiwezekani.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji iwapo maneno matupu ya kutamka kwa mdomo yanaweza kutengeneza kosa la uhaini.

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa ufahamu wangu, maneno matupu hayawezi kutengeneza kosa la uhaini.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji huo mkutano ulichukua muda gani?

Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, ni masaa 3.

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, Jambo TV na Chanzo TV walirusha kwa masaa mangapi?

Amani Sam Golugwa: Kati ya saa 1 hadi 2.

Lissu: Nakusomea maneno wanayonishtaki, halafu waeleze Majaji muda ninaoutumia kusoma.

(ANASOMA)

Lissu: Nimetumia muda gani?

Amani Sam Golugwa: Kama sekunde 26 hivi.

WEKA EMOJI KAMA UNASOMA

SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
 
TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI

SEHEMU YA 12

Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, kwa kumbukumbu zako, iwapo palikuwa na mazungumzo juu ya mfumo wa uchaguzi.

Nassoro Katuga: Naona anamsaidia.

Lissu: Basi Shahidi aeleze mwenyewe kile ambacho hakijaelezwa katika hii nusu dakika.

Amani Sam Golugwa: Hoja alizozungumza kuhusu mfumo wa uchaguzi Tanzania; matatizo ya uchaguzi yaliyopo kuanzia katika Katiba, yanayoathiri chaguzi zetu; kwenye sheria, kanuni na miongozo.

Alieleza kuhusiana na tume mbalimbali:
Tume ya Jaji Nyalali, Tume ya Jaji Kisanga na Tume ya Warioba.

Jinsi zilivyoeleza mapungufu yaliyopo katika mifumo yetu ya uchaguzi na mapendekezo ya tume zote hizi kuhusiana na nini kifanyike ili kurekebisha mifumo ya uchaguzi.

Kuhusu taarifa mbalimbali za waangalizi, waangalizi wa ndani wa chaguzi kuanzia mwaka 1995.

Waangalizi wa ndani aliwataja REDET na TEMCO, na alifafanua na kuelezea maoni ya waangalizi wa ndani kuhusiana na haja ya kuwa na mabadiliko katika mifumo ya uchaguzi ili kuwa na chaguzi huru na zinazoaminika.

Alifafanua pia kuhusu taarifa (report) za nje kutoka chaguzi za mwaka 1995, akiwataja SADC, Marekani, Jumuiya ya Ulaya, Jumuiya ya Afrika na mapendekezo yao kuhusiana na haja ya kuwa na mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.

Alizungumzia kuhusu uzoefu wa chama chetu kwenye chaguzi za Serikali za Mitaa za mwaka 2019.

Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2020.

Alizungumzia pia uzoefu wa marudio ya chaguzi ndogo za madiwani na Ubunge zilizotokea mwaka 2015, 2016, 2017, 2018, 2019 na kuendelea.

Alizungumzia kuhusu uchaguzi wa Serikali za Mitaa wa mwaka 2024.

Mazungumzo hayo yalikuwa ni uzoefu wa matukio ya ovyo ambayo chama, kwa maana ya wagombea wetu, tuliyapitia.

Hayo matukio ya ovyo ambayo yalikuwa yanafanywa na Wasimamizi wa Uchaguzi na wasimamizi wao ni pamoja na kuwaengua wagombea wa CHADEMA kihuni.

Wasimamizi wasaidizi wanakataa kupokea fomu za wagombea.

Lissu: Jambo lingine, ukiachia hayo mambo ya ovyo ya chaguzi za Serikali za Mitaa...

Amani Sam Golugwa: Matukio mengine ni mauaji...

Ajuaye Zegeli: Waheshimiwa Majaji, muda sasa ni saa 7 na dakika 5. Kama akiridhia, tunaomba tuhairishe kwa health break. Tukirudi tutaendelea.

Jaji Ndunguru: Mshtakiwa...?

Lissu: Mheshimiwa Jaji, nina less than one hour. Sidhani kama nitamaliza hilo one hour tukirudi, lakini naomba tu break, Shahidi akapate maji.

Na muda ni uleule wa saa 1 na nusu, niweze kufanya consultation na wasaidizi wangu.

Jaji Ndunguru: Kwa hiyo, Shauri linaahirishwa hadi saa 8 na nusu.

Tunatarajia utatumia hicho saa 1 ulichosema.

Shahidi utaendelea baadaye.

MAJAJI WANATOKA.

TUKUTANE SAA 8:30 MCHANA.
 
Golugwa ana kitu sana, ila naona anakosa utulivu, yaan km ana hamaki, inatakiwa atulie afu asiwe na papara wakati was kujibu. Mbona mnyika kasha safisha njia. Ni wao kutelezaaa tuu.
Kabisa yaani
 
Back
Top Bottom