Sasa huyu hapa kwenye picha ni nani, na kwa nini anaonyeshwa hapa.Leo September 3, 2026, Jana tuliishia Sehemu ya 337
Nina sababu ya kuuliza, na siyo nzuri.
Sasa huyu hapa kwenye picha ni nani, na kwa nini anaonyeshwa hapa.Leo September 3, 2026, Jana tuliishia Sehemu ya 337
Kwamba hata Jamhuri wanaogopa kumwita shahidi aliyeanzisha "Kampeni ya NO REFORM, NO ELECTION"; aje kutoa ushahidi mahakamani kuhusu uasi wa Tundu Lissu; hili pekee linashangaza sana.Wao ndo wameuchagua aina ya mchezo, uwanja wa mechi na kufungua mageti, acha waicheze ngoma. Hii inafanya hata watu waliokuwa wanashangaa kwa nini Mh. Tundu Lisu ang'ang'anie kuishinikiza serikali ifanye mabadiliko ya kisheria juu ya uchaguzi wawe na uelewa wa msingi mkuu. Hapa hata ambaye alibaki na kiimani kidogo nao kanaondoka, ukijumlisha na yanayoendelea, itawawia vigumu huko mbeleni kupata kura halali kwenye boksi la kura. Wanajining'iniza kwa kitanzi chao wenyewe.
Wamelikoroga na wanae upande wao kwa sasa/kimantiki, inabidi nyoka avuliwe gamba kwanza na apondwe kichwa. Kwa mantiki yao kikulacho kinguoni mwako Gaidi & Mhaini.Kwamba hata Jamhuri wanaogopa kumwita shahidi aliyeanzisha "Kampeni ya NO REFORM, NO ELECTION"; aje kutoa ushahidi mahakamani kuhusu uasi wa Tundu Lissu; hili pekee linashangaza sana.
Sasa utamnyonga vipi mtu ambaye hata hakubuni uasi wenyewe!
Yupo vizuri m/kiti wake mjanja angeshamsanua kama alivyofanya baadhi ya maeneoJamani nina wasi wasi na Golugwa, ni yuko vizuri ktk kutoa majibu, ila uwasilishaji wakw unanipa hofu, afu anakua km hajiaminii.
Basi mtazamo wangu unaona hivyo.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama tena.Ila Katuga, sijui huwa anapanick nini, ndio maana lissu ana mnyoosha tu. LOL
😂😂😂😂
ona hapa kwa mfano: kwamba hajui kuwa kesi Iko kwenye utetezi?Ila Katuga, sijui huwa anapanick nini, ndio maana lissu ana mnyoosha tu. LOL
😂😂😂😂
Mpuuzi huyu Katuga wao mbona wamemuingiza ishengoma!TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMANI GOLUGWA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 14.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwepo wa nia ya kuitishia Serikali ya Jamhuri ya Muungano katika mazungumzo yangu.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sioni nia ambayo ingepelekea kuitishia Serikali.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji kama iwapo haya maneno niliyoyazungumza kama ilikuwa mara yako ya kwanza kuyasikia.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, haikuwa mara ya kwanza. Nilishawahi kuyasikia ukiyazungumza.
Lissu: Waeleze, uliyasikia wapi?
Amani Sam Golugwa: Niliyasikia katika mkutano tuliouandaa Sekretarieti na Wahariri wote Tanzania kupitia Jukwaa lao la Tanzania Editors Forum.
Lissu: Unakumbuka tarehe?
Amani Sam Golugwa: Mpaka nijikumbushe kidogo.
Katika mkutano ule uliokuwa unaongozwa na Mwenyekiti wa TEF, uliyasema.
Siku uliyokutana na Viongozi wa Dini ya Kiislamu (Shura ya Maimamu) mbele ya kiongozi wake, Issa Ponda.
Niliyasikia maneno hayo ukiyazungumza.
Nilisikia katika mkutano wa Legal and Human Rights Centre mbele ya kiongozi wao, Massawa.
Nilikuwapo na niliyasikia uliyasema.
Nilisikia maneno hayo mbele ya Mzee Waziri Mkuu Mstaafu, Jaji Joseph Warioba.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, tulikutana na Mzee Warioba wapi?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, tulikutana na Mzee Warioba ofisini kwake.
Nilikuwapo na niliyasikia.
Lissu: Nilikuwa nasambaza maneno ya uhaini?
Amani Sam Golugwa: Haukuwa unasambaza uhaini, bali mabadiliko kwenye mifumo ya uchaguzi.
Ili mabadiliko yatokee kabla ya uchaguzi wowote kufanyika.
---
Lissu: Baada ya tarehe 09 Aprili mwaka jana, baada ya mimi kukamatwa, ni mambo gani yalitokea kwa chama na nyie viongozi?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, chama kilifungiwa kesi na viongozi wa chama mbalimbali.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji, nini kilikutokea wewe mwenyewe?
Amani Sam Golugwa: Tarehe 13 Mei 2025 nilikuwa nasafiri kuelekea Ubelgiji.
Safari ambayo nilikuwa naenda kwenye mikutano kuwakilisha chama katika Umoja wa Vyama vya Kidemokrasia Duniani.
Lissu: Kifupi chake kinaitwaje?
Nassoro Katuga anasimama.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, tunaona ushahidi unatolewa kinyume na kifungu cha 156.
Sasa hivi tunaletewa safari na baadaye atatueleza habari ya ndoa.
Kifungu hiki kinalazimisha ushahidi must relate to the issue.
Relation yake na uhaini ni nini hapa?
Tunarudi katika irrelevant facts.
Watuambie, hicho kina relevance gani?
Tunaomba walete utetezi unaohusiana na kesi.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, wakili wa Serikali anapenda kutoa mifano ya ovyo kabisa.
Mfano kwamba shahidi alioa na kuhusuiana na CHADEMA, nitautoa.
Ushahidi wa DW2 ni kampeni ya Jeshi la Polisi kunisakama mimi na kuwasakama viongozi wangu na chama changu.
Kesi hii, kwa mujibu wa ushahidi tulioutoa, ni utetezi dhidi ya sisi tunaonewa kwa mashitaka ya uongo.
Kwa hiyo, anachokisema shahidi juu ya kilichomtokea ni relevant.
Kifungu cha Sheria ya Ushahidi 7, 8 na 9, Relevance of facts.
(Anasoma kifungu cha 09.)
Waheshimiwa Majaji, hili swala la Polisi kuwakamata viongozi wa CHADEMA—
Leo Tundu Lissu, jana Mbowe na juzi Dr. Slaa.
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naona hajajibu kifungu cha 156, ame-concede.
Lakini huo ushahidi wa kukamatwa ni fact kwa upande wa utetezi, siyo kesi.
Lissu: Kwani sisi tunatoa ushahidi wa nini? Si utetezi?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama tena.
MAJAJI WANATETA.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Hata kama ni wewe ungehangaika mkuu, ameaminiwa na wakubwa zake alafu anaona ugali wake unaharibiwa mbele yake na mbele ya wakubwa zakeKatuga ana hangaika sana
Mpuuzi huyu Katuga wao mbona wamemuingiza ishengoma!
Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama tena.
Ametambua kilichomfanya anyanyuke, hakin maana mbele ya mahakama, anaamua kukaa kinyonge.
ona hapa kwa mfano: kwamba hajui kuwa kesi Iko kwenye utetezi?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa Majaji, naona hajajibu kifungu cha 156, ame-concede.
Lakini huo ushahidi wa kukamatwa ni fact kwa upande wa utetezi, siyo kesi.
Lissu: Kwani sisi tunatoa ushahidi wa nini? Si utetezi?
Nassoro Katuga: Waheshimiwa, basi tuendelee, lakini Mahakama ikiona wanazidi, tuna haki ya kusimama
Najifunza kupitia kesi hii, ukiwa CHADEMA hupaswi kuwa na akili ya kudeka na tegemezi, unapaswa kuwa ngangari na unayejua kujieleza vizuri na kujisimamia.TUNDU LISSU ANAMHOJI SHAIDI WAKE AMAN GOLUGWA MAHAKAMANI
SEHEMU YA 16
Lissu: Waeleze Waheshimiwa, hii kamata kamata maana yake nini?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, ni kutudhoofisha na kuturudisha nyuma katika harakati za kisiasa.
Lissu: Waeleze Waheshimiwa, ufahamu wako kuhusu kukamatwa kwangu na Jeshi la Polisi.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nina kumbukumbu ulikamatwa ulipokuja kuwatetea wanachama wetu, wewe na Dr. Slaa.
Nina kumbukumbu ulikamatwa ulipoenda Mbeya katika Siku ya Vijana Duniani.
Nina kumbukumbu ulikamatwa ulipomuita Magufuli dikteta uchwara.
Lissu: Katika kumbukumbu za matukio ya mimi kukamatwa, waeleze Majaji kumbukumbu yako ya mimi kutiwa hatiani kwa makosa niliyokamatwa nayo.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, sina kumbukumbu yoyote kwamba umeshawahi kutiwa hatiani kwa kosa lolote.
Lissu: Umenifahamu kwa muda gani?
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, nakufahamu kwa muda wa miaka 20.
Lissu: Leo sasa nashitakiwa kwa kosa la uhaini. Waeleze Waheshimiwa Majaji uwezekano wa mimi kuwa muhaini wa nchi yangu.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, kwa namna ambavyo nimekufahamu, wewe ni mtu mwema sana.
Umejitoa sadaka kuwatetea Watanzania.
Kesi zote ulizopitia na mashitaka...
Jaji Ndunguru: Unajibu swali gani? Wewe jibu swali.
Amani Sam Golugwa: Namuelezea Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Kwa nini CV yake? Si alishatoa hapa Mahakamani?
Lissu: Waeleze Waheshimiwa Majaji uwezekano wa mimi kuwa muhaini wa nchi yangu.
Amani Sam Golugwa: Waheshimiwa Majaji, hakuna uwezekano wa wewe kuwa muhaini.
Lissu: Waheshimiwa Majaji, nimemaliza maswali kwa shahidi huyu.
WEKA EMOJI KAMA UNASOMA
SHARE ZAIDI UJUMBE UFIKE MBALI
Asante sana Manyanza kazi yako ni njemaMAHAKAMA IMEISHIA HAPA KWA LEO TUKUTANE KESHO
Jaji Ndunguru: Upande wa Mashitaka.
Ajuaye: Waheshimiwa Majaji, kwa kuwa muda umeisha, tunaomba Mahakama ihairishe kesi hadi kesho kwa ajili ya maswali ya dodoso.
MAJAJI WANATETA.
Jaji Ndunguru: Mshtakiwa, unasemaje?
Lissu: Sawa, Mheshimiwa Jaji.
Jaji Ndunguru: Shauri linapangwa kusikilizwa kwa upande wa utetezi kuendelea kuulizwa maswali ya dodoso hapo kesho saa 3:00 asubuhi.
MAJAJI WANATOKA.
TUKUTANE KESHO ASUBUHI.
MUWE NA JIONI NJEMA